Si ushauri mzuri. Mimi sikubaliani nawe..
Awe anahutubia wakati wowote anaoona yeye mwenyewe inafaa na hususani kama ana jambo la kusema...
Nionavyo mimi ni kuwa, ipo kasoro kubwa ya hotuba zake nyingi, ya kusema baadhi ya mambo ambayo hapaswi kuyasema hadharani mbele ya subordinates wake...
Mfano leo ktk hotuba yake kwa ma - RAS na RC amesema kitu ambacho kina- expose udhaifu wake na walio chini yake wanaweza kuutumia kumwingiza mkenge ktk baadhi ya maeneo ktk utawala wake...
Alisema "....baadhi yenu (aliowateua) siwajui vizuri, lakini nitaendelea kuwaelewa kidogo kidogo..."
This is untimely statement and it was absolutely not required to be said there in public like that even if it is true..!!
Hii inatupa maswali sana sisi huku nje. Maana kama humjui vizuri mtu uliyemteua wewe mwenyewe na kumpa jukumu nyeti la uRC au uRAS au Uwaziri nk, ikawaje ukamteua...??
Tukumbuke kuwa wengi wa maRC au RAS wanaongoza mikoa mikubwa yenye wakazi (population) wengi na rasrimali nyingi kuliko idadi ya watu wote ambao Rais wa nchi ya Zanzibar yote anaowaongoza...!
Huwezi kulinganisha mathalani mkoa wa DSM, Mwanza, Arusha, Mbeya nk na nchi ya Zanzibar yote kwa idadi ya watu na rasrimali zilizopo ktk kila mikoa hii...
Nasema hivi kwa sababu, RC au RAS ni mtu muhimu na mwenye wajibu na jukumu nyeti na kubwa sana ktk utawala wa nchi hii. Uteuzi wao lazima uwe very carefully scrutinized...
Sasa Rais kukiri hadharani hawajui kwa undani baadhi ya wateule wake hawa inatia shaka kidogo...