Mhe Rais , Mama yetu, umekuwa msikivu muda wote, umekua ukitatua matatizo ya Watanzani pale yanapojitokeza bila kumuonea mtu aibu.
Mhe Rais, tupia jicho Tanesco, Tanesco hii bado ni jipu kubwa, Ile Tathimini ya Wakurugenzi wa Halmashauri kupimwa kwa utendaji wao iende mpaka kwa Mawaziri na Wakurugenzi wa Taasisi nyinginezo.
Walifukuza kitengo cha habari sijui kama wao ndio walikuwa Wanahusika na kuhakikisha umeme haukatiki. Watanzania wana taka umeme wa uhakika na sio mtoa habari wa umeme kukatika.
Ni aibu kwa umeme kukatika zaidi ya Mara kumi kwa siku, mfano kwa Wakazi wa Goba centre umeme unakatika kila baada ya Dakika moja na Manager wa Tanesco Wilaya yupo anasubiri mpaka Mheshimiwa Rais aje..
Ni muda muafaka sasa Wakurugenzi, manager wote wapimwe kwa output