Hivi karibuni mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia ameonekana kuchukua maamuzi na kutoa kauli zenye kuyumba na kuchanganya umma kwa kiwango kikubwa kiasi cha kuacha gumzo kubwa kwa wananchi mitaani na mitandaoni.
Wachambuzi wa mambo wanaelezea kuwa ugumu wa mambo unaomfikia rais samia leo hii ni kwa sababu ya mambo yafuatayo:
1. Rais alianza madaraka yake kwa mguu mbaya
Wachambuzi wanasema kwa mujibu wa ibara ya 51 kipenge cha 2 cha katiba ya Jamhuri ya muungano, Mara tu baada ya kuapishwa kuwa rais, rais alitakiwa ndani ya siku 14 apeleke jina la waziri mkuu bungeni likapigiwe kura, wachambuzi hao wanasema hata kama angetaka angeweza kulirudisha jina la waziri mkuu huyuhuyu aliyeko sasa, lakini kwa bahati mbaya hakufanya hivyo kitu kinachowafanya watu wahoji hata uhalali wa serikali yake mwenyewe kwa mujibu wa katiba
2. Mgongano wake na Spika Ndugai umeugawa umma
Kiufupi asilimia kubwa ya wananchi wanasapoti kauli ya Ndugai kuwa deni la Taifa linazidi kukua kwa kasi na wananchi wanahofu licha ya wataalamu kujaribu kulielezea kuwa bado ni himilivu. Hata hivyo hasira na vicheko vya wananchi kutokana na kadhia iliyomkumba Ndugai imetokana na madhambi ya Ndugai ya nyuma na wala si kauli yake ya kuonyesha kutopendezwa na nchi kukopa.
3. Kubadili baraza kisha kujaribu kuwafurahisha aliowatumbua barazani
Mwanzo rais aliwaambia wananchi kuwa anakusudia kubadili baraza jwa sababu kuna watu wana ambition za 2025, mara tu baada ya kuwatumbua akaanza kutafuna maneno yake mwenyewe kuwa baadhi ya aliowatumbua ni watu muhimu sana anawahitaji afanye nao kazi, Wananchi wakashikwa mshangao kuwa ina maana wale watatu waliobaki, wawili wakiwa wahamiaji kutoka vyama vya upinzani ndo walitaka kumng'oa 2025?-wananchi wamegoma kukubaliana na hii kitu
4. Kesi ya Mbowe
Wananchi bado wanafuatilia kwa umakini kesi ya Mbowe, hii kesi ugumu wake wanaihusisha na rais kumhukumu Mbowe jinai wakati wa Interview yake na BBC kabla hata mahakama haijatoa hukumu. Kwa hiyo wananchi wanaichululia kesi ya Mbowe kama "Jambo la Rais"
5. Kauli tata ya kuwaambia wateule wake kuwa hata kama wanakula lakini wasivimbiwe ilimradi tu wajipimie.
Hii kauli imechukiza wananchi mno, ile hasira ya wananchi dhidi ya ufisadi imewaka tena. Watu walitaka kusikia kauli yenye mamlaka ya rais ikikemea ulaji na siyo kuwaambia kuwa walaji anawajua, na kwamba anajua wanakula ila sasa wajipimie, wasivimbewe. Wananchi wanahisi rais hana zeal, au mkazo wa kupiga vita ufisadi
6. Ishu ya katiba mpya
Kuna concensus ya kijamii inajengeka kwa kasi nchini kuwa sababu kubwa ya matatizo yetu nchini ya kiuongozi na hata maendeleo yanapata sababu ndani ya katiba ya sasa. Na kuna kutokuamini hatua za kisiasa za raisi kutumia chombo cha msajili wa vyama cha timu ya kuchakata maazimio ya kikao baina yake na baadhi ya vyama. Raia wengi wana amini suala la katiba mpya kwa asilimia kubwa linahitaji utashi wa rais na wanangoja wauone, kwa hiyo rais alitambue hili.
7. Conclusion
Wananchi wanataka rais arudi ktk. njia kuu, yaani arekebishe mambo na makosa ya kimaamuzi, kikauli aliyoyafanya, otherwise imani yao kwake inapungua siku baada ya siku