Wanabodi,
Amani iwe kwenu!
Tangu kuchaguliwa kwa Rais wa awamu ya tano,tumeshuhudia akiendeleza matukio km ilivyokuwa wakati wa kampeni.
Rais wetu anataka kujaribu kuendesha nchi kwa matukio,sina hakika sana ya kitakachotokea baadae ingawa ningeomba tupate matokeo chanya zaidi kwa kile anachokifanya.
Kuna wakati naona km ni mwendelezo tu wa sinema za ccm! Kuthibitisha hili,ndo maana natamani Rais wangu afanye ziara ya kushitukiza ktk wizara ya ujenzi ambayo yeye alikuwa boss huko. Baada ya hapo atakuwa ametushawishi wengi kwenda na kasi yake. Vinginevyo,huu nao utakuwa muendelezo wa push-up.
Nawasilisha!