Watendaji Wengi Wa Serikali Wametimuliwa Kazini Na Rais Magufuli Kwa Makosa Ya Wizi, Uzembe Kazini, Ufisadi, N.K, Maoni Yangu Ninampa Rais Magufuli Asiishie Kuwafuta Kazi Bali Aende Mbele Zaidi Kwa KUWAFILISI MALI ZAO ZOTE ILI KUFIDIA HASARA WALIOISABABISHIA SERIKALI KWA KIPINDI CHOTE WALICHOKUWA WANAFISADI NCHI HII HADI WAALIM WAKOSE KULIPWA MADAI YAO. Pili, Namuomba Apite Pale Feri UTUMISHI Kuona Madai Ya Walimu Yanavyoshughulikiwa Naona Ataondoka Na Mtu Pale. Tatu Uje Na Kwenye Halmashauri Huku Uone Waalimu Hadi Sasa Hawajapata Barua Zao Za Madaraja Wakisingizia Et Mitihani Ya Necta Ndo Maana Walim Hawajapandishwa Madaraja Utafikiri Mitihani Hy Imejitokeza Kwa Dharula Wakati Ilijulikanika Wazi Kabisa Kwanini Hawakuziandaa Mapema Hz Barua Za Madaraja? Hao Wote Mh Rais Timua Kazi Ni Wazembe Kazi Yao Ni Kuning'iniza Tai Na Kufuga Vitambi Tu, TIMUA KAZI HAO WAKALIME MALIMAO