ushauri huu naomba umfikie mh Raisi na pia nitatoa ushauri kwa ukawa nikiwa mtanzania mwenye fikra tofauti kabisa wanasiasa wa kizazi hiki.
USHAURI WA KWANZA
Mh Raisi nimesoma magazeti mengi ya leo tar 30/7/2016 mengi yakizungumzia mikutano ya chadema au ukawa yenye kauli mbiu ya UKUTA,kinachopambishwa na magazeti ni kama kuonekana kuna vita kati ya utawala wako na wapinzani au ukawa.
Niseme hivi,ukawa inaundwa na watanzania,na wewe mkuu wa nchi ni mtanzania,polisi na vyombo vyetu vya dola ni watanzania na wao pia,na wale watakao pata madhara kwa fujo zitakazo ni watanzania pia,sasa basi waache wafanye mikutano yao kwa amani na uwape vyombo vya ulinzi wakawalinde watimize wajibu wao kisheria na kikatiba,lakini kwa upande mh Raisi cha kufanya ni kimoja watanzania tuna njaa na kero nyingi mno ambazo hazitatuliwa kwa mikutano ya ukuta wala kumsema mtu fulani,kwa maana hiyo basi Waagize MADC NA MARC wakupe mahitaji muhimu matatu ya wilaya zao na mikoa yao,matatu muhimu.
wakisha kupa weka mikakati ya kiutawala,nikiwa na maana kwamba kila mkoa au wilaya ukuta utakapo pelekwa wewe utawapa kazi halmashauri na taasisi za serikali kutimiza moja ya mahitaji muhimu ya wananchi,mahitaji yetu hayaishi leo ila yapo muhimu kama afya,maji na elimu,sehemu za biashara.
hakuta kuwa na haja ya kuwatumia polisi kuzuia mikutano hiyo kwa nguvu kubwa ila utapambana nao kwa kuwatekelezea mahitaji muhimu ya wananchi hayo ambayo utakuwa umepewa na madc au marc wako.
Pambana nao kwenye utekelezaji wao waache waongee ila vitendo vitawajibu.
USHAURI WA PILI.
Ukawa siasa za kupoteza pesa kuzunguka nchi nzima kujijenga zimepita na wakati,ila mtaweza kujijenga tu pale mtakapo acha kuwa na fikra za kinafki na uchoyo.
wakati umefika sasa badala ya kuzunguka na UKUTA pelekeni wataalamu wenu wakatafute masoko ya bidhaa zetu au bidhaa zinazo zalishwa kwenye mikoa mliopata madiwani,wabunge na Mamaeya ndani na nje ya nchi mkishirikiana na serikali,Fatilieni viwanda vilivyopo kwenye maeneo yenu kama wanafata sheria zetu za uwekezaji kwa ufasaha,huku mkiangalia na ushirikishwaji wa WATANZANIA kwenye uzalishaji hapo kiwandani mtakua mmewasaidia sana watanzania.leteni wawekezaji wawekeze mtakumbukwa kwa uzalendo wa nchi na mtakauwa na uwezo hata wa kupewa nchi.fanyeni mambo ya maendeleo yapo mengi,michango ya mikutano yenu pelekeni hosptal au mkajenge zahanati.
watanzania wanahitaji maendeleo na si fujo wala maneno mengi mdomoni.
yule yule Zubedayo_mchuzi mzee wa kuzunguka na kutembea umbali mrefu.