Mheshimiwa rais najua kuwa unalo tatizo la kutosikiliza ushauri ila naamini walau utasikiza mara hii moja. Ni hivi, najua kuwa unatamani sana ufanye jambo ambalo vizazi na vizazi vitakukumbuka na kukusifu. Tatizo ni kuwa hadi sasa hujaamua ni jambo lipi ufanye.
Mheshimiwa mkapa atakumbukwa kwa uwanja mpya na daraja la mtwara.
mheshimiwa kikwete atakumbukwa safari zake za nje na pia kuweza kuunganisha Tanzania yote kwa barabara za lami.
Mheshimiwa wewe hadi sasa unakazana kung'ata kuliko uwezo wa mdomo wako kutafuna. Mara mgambo wasisumbue mama ntilie,mara wakuu wa mkoa watengeneze madawati, mara mahakama ya mafisadi, mara fly over, mara daraja busisi, mara kufagia, mara boti ziwa victoria, mara mahakama ya mafisadi, mara kuhamia dodoma.....list is endless.
Pamoja na utitiri huu wa mambo hakuna hata moja lililokamilika hivyo yote yataishia kuwa ubatili tu!
Ushauri wangu ni kuwa hebu achana na yote hayo....wewe kazana na jambo moja tu lililo ndani ya uwezo wako kama vile kuhakikisha usafi unafanyika kisawasawa na watu wanaoga kila siku.