Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Ndo mana walihakiki vyeti. Hata kwa walioonekana kuwa ni wachapakaz. Kwani ndo mara ya kwanza kukamatwa kwa wauza unga? Achen kujitoa akili... Hao ni wanafiki Hakuna mapambano na wauza unga ni unafiki tu
 
Haya ni maoni yangu ambayo ni matokeo ya kinachotokea nchini juu ya matendo ya wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa.

Nafasi hizi zimedhalilishwa kuanzia utawala wa awamu ya 4 na hasa sehemu ya pili ya utawala wa awamu ya 4, Utawala wa mzee Kikwete. Nafasi hizi mbili ni nafasi muhimu sana. Umuhimu wake unatokana na madaraka waliyonayo juu ya raia wengine. Ni madaraka makubwa na muhimu. Nafasi hizo ni vizuri kabisa zikashikwa na watu wazoefu, watu wa busara.

Tatizo ktk awamu ya 4 waligeuza nafasi hizi zikawa ni nafasi za urafiki, nafasi za vijana. Ni kosa kubwa kufanya nafasi muhimu kiasi hicho kugeuzwa kuwa ni nafasi za kujifunzia uongozi. Ni vibaya mtu atoke chuoni, akiongoza vikundi vya umoja wa vijana CCM ghafla unampa kuwa mkuu wa Wilaya. Unampa kuwa mkuu wa mkoa.

Rais Magufuli pia ameingia madarakani kwa mtindo huo huo! Tunaomba mabadiriko. Kwa mtindo huu hatutafika. Nafasi hizi zisiwekwe kuwa ni nafasi za mafunzo kwa vijana. Ni nafasi za heshima. Wapewe watu wanaostahili kupewa heshima hata kwa umri tu! Narudia, siyo sahihi kuzifanya kuwa nafasi za vijana kujifunza uongozi, ni nafasi za watu wanaojua uongozi.
 
Mkuu amekosa busara,yeye mwenyewe ameamuwa kuidharirisha taasisi yake ya uteuzi na waliomchagua kwa ujumla. Bashite yeye kasifiwa, kalitia maji tembo, leo mkuu anaona aibu kumwondoa mteule. Ameonyesha kukosa hekima na busara kwa kushindwa kuvifanyia kazi vitendo vya ovyo vya wazi alivyofanya Bashite. USHAURI Leo unalea donda mwishoe ni kupata KANSA.
 
Huyo unayemuita Nashite naamini ni huyo Paulo Makonda. Huyo mbona aliteuliwa na Kikwete kuwa mkuu wa Wilaya? Tena baada ya kumkaba Warioba. Kwa wakati ule tulipoona vile, tukaamini alitumwa! Obviously siyo na Magufuli.
 
Habari ndugu, na jamaa!

Kama tunavyoshududia udhaifu wa mheshiwa Pombe Magufuli, kushabikia na kupigia debe, anachofanya RC Makonda.

Tumeshayasikia mengi, Makonda ni useless katika nafasi aliyonayo, makonda alitakiwa awe mlinzi au FFU, maana hana uwezo wa kuwaongoza watu wanaojitambua, cheo hicho cha kuwa RC, ni madaraka yaliyomzidi hana capacity hiyo wala mipango ya kusimamia maendeleo ya kitaifa.

Tunajua wazi kabisa, hawa watu wanalindana

Huo ni ushamba, na ufinyu wa kufikiri,RC Makonda hana job description, Makonda hajui anafanya nini, hili swala la vyeti, mheshimiwa Rais wewe ndiye uliyeanzisha ukaguzi wa vyeti feki serikalini, sasa iweje Daudi Bashite anaachwa, je hiyo ni haki sawa? mbona wengine unatumbua, hapo umeshindwa na nini? Bado anavamia kituo cha Clouds tena kwa kutumia mitutu ya bunduki.

Rais Magufuli, unachemsha hebu utathimini uongozi wako.

Makonda ameanzisha kikundi cha kigaidi cha kutaka kujitawala kama nchi hii ni ya kikabila!
 
"Mkuu wa mkoa angelikuwa Mushi,angeondoshwa siku ile ile bila viatu wala nguo.
 
Hopefull Tanzania tunaweza tukajivunia kwa kuwa na raisi bora kwa africa nzima na raisi anaefanya kazi kwasababu ya masilahi ya wananchi
Wengi wanatamani kuwa na rahisi kama huyu lkn tunamshukuru Muumba kwa kutupa sisi wana zake, katika kipindi hiki kifupi tumeona mtazamo tofautitofauti wa raisi

MAZURI YA MAGUFULI
-watoto kusoma bure

-ufisadi umebaki ndoto

-watumishi wa serikali wamekuwa wafanyakazi wa wananchi na hakuna ubepali baina ya watu

-shirika la ndege lilikuwa limekufa na hakukua na mafanikio ya kulifufua hivi punde sasa hivi tunaona soon litapata safari adi za kwenda marekani

-flyover za dar zinatililika soon dar itabadirika kabisa interms of barabara

-mawaziri na wafanyakazi wa serikali wamerudisha heshima kwa raisi (kuogopeka i mean). Ko inakuwa vigumu kwao kuiba maana kuiba ni makubaliano

Ahadi za muheshimiwa kubwakubwa alizohaidi ambazo hajaanza kuzifanyia kazi ni milion50 kila kijiji. Na i believe soon zitakuja kwetu maana ni kama mikopo na si kugawa

CHANGAMOTO ANAZOZIPATA

-kutokutumia kauli za kubembeleza kwenye mikutano

-maisha kuwa magumu kwa baadhi ya watu kutokana na kupungua kwa utumiaji ovyo wa kwa baadhi ya watu

-kutokumtoa makonda kwa baadhi ya scandle

HITIMISHO NA MAONO YANGU
Kwa uongozi huu uliopo naweza kusema hakuna raisi bora na mwenye maono kama huyu jamaa mpaka sasa ukiachana na jitiada za nyerere.
Sema watanzania wamezoea kuponda kusikokuwa na sababu na kutokuwa na hoja
Ni virahisi mtu kuanza kutukana kama mlevi ila ni vigumu sana mtu kuwa na hoja
Mabepali wengi walizoea kula hella na kuishi bila kusumbuliwa katika nchi hii
Leo hii wakikaa wakaamua kudanganya wananchi kwa mipango mitakatifu watu nao uingia mtegoni na kuwafata, waga najiuliza2 na kushangaa maana nawaonaga kama wehu

Inshort ni watu wanaponda kwa mambo ya kijinga ambayo hayana faida kwa nchi na kusahau mambo ya msingi,leo hii ukitukana bila hoja utaonekana wa maana kuliko kusifia na hoja. Leo hii watu wanaponda kisa raisi habembelezi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kuna watu wanatamani ufisadi urudi eti ili maisha yawe marahisi, seriously?????????

Tukitulia kama wananchi tukamsaport raisi tutafika mbali
Ila tukiendelea kupiga kelele kwa mambo ya kipuuzi na kimbeambea hatutafikambali maana ata maisha yako hutoweza kuyaendesha mwenyewe
 
Nafikiri shida hazipo kwenye ukoo wenu tu, sisi wengine huku hoi. Hongera mkuu kwa kutokuona ugumu wa maisha.
 
Binafsi, nampongeza sana Rais Dr. Magufuli kwa msimamo.
Siyo rais awe mtu wa kulialia; ndivyo kiongozi anapaswa kuwa thabiti.

Kwa sababu, kama sivyo Watz mnaweza sema Rais asipande gari atembee kwa miguu kwa sababu wengi wa watanzania hawana magari.
 
Binafsi, nampongeza sana Rais Dr. Magufuli kwa msimamo.
Siyo rais awe mtu wa kulialia; ndivyo kiongozi anapaswa kuwa thabiti.

Kwa sababu, kama sivyo Watz mnaweza sema Rais asipande gari atembee kwa miguu kwa sababu wengi wa watanzania hawana magari.
Ngoja nyumbu wachukie, miradi mikubwa ya maendeleo tunaiona, nyie kalieni majungu tu, mtashtuka 2020 hiyo hapo halafu sisi tutaamua nani alitutumikia ipasavyo.
 
His Excellence The President of the United Republic of Tanzania, Mr. Dr. John Pombe Joseph Magufuli aka Ngosha, bulldozzer, the terminator.
KAZA BUTI baba, watanzania tupo nyuma yako, WATANZANIA WOTE tulikuwa tunataka rais wa tofauti kama wewe, Mungu mkubwa here you are.
Chapa kazi mkuu, asiekuelewa akasage chupa anywee na maziwa mtindi.
 
Ha ha haaa, hapo kwenye chupa....nakumbuka kauli za Gwajima..sasa zamu yao asiyependaaaaaaa......!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…