Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Wana JF naomba niwasilishe amri hii kama ujumbe kwa Magufuli, hili sio ombi kutoka kwetu sisi, mwaka 2020 hatutahitaji aje atushawishi au kutueleza nani tumpigie kura awe Rais, Mbunge au Diwani maana mchezo huu ameuanzisha mwenyewe na kwakuwa hataki kusikiliza hisia zetu tulio mfikisha hapo alipo sasa tumesimama na kusema kuwa asije kutuelekeza wala kutushawishi nani wa kumpigia kura maana akija tu basi atakuwa amekosea na atakuwa ameharibu aache tu tunajua wenyewe jinsi ya kujiamulia maana hatuhitaji atuletee hisia zake na ushawishi wake maana si yeye anayetuletea chakula na nguo, asituelekeze wapi pa kupigia kura tutapajua wenyewe tuna akili timamu.
Alipiga pushup#2020 sjui ataruka kifrogfrog au
2020 ni mwendo wa kukaziana tu

Ova
 
Wana JF naomba niwasilishe amri hii kama ujumbe kwa Magufuli, hili sio ombi kutoka kwetu sisi, mwaka 2020 hatutahitaji aje atushawishi au kutueleza nani tumpigie kura awe Rais, Mbunge au Diwani maana mchezo huu ameuanzisha mwenyewe na kwakuwa hataki kusikiliza hisia zetu tulio mfikisha hapo alipo sasa tumesimama na kusema kuwa asije kutuelekeza wala kutushawishi nani wa kumpigia kura maana akija tu basi atakuwa amekosea na atakuwa ameharibu aache tu tunajua wenyewe jinsi ya kujiamulia maana hatuhitaji atuletee hisia zake na ushawishi wake maana si yeye anayetuletea chakula na nguo, asituelekeze wapi pa kupigia kura tutapajua wenyewe tuna akili timamu.

Wewe na nani mkuu?
Upande upi mkuu?
Tanzania hii yenye watu takriban milioni hamsini au?

Pima upepo kwanza kama unaweza,pia 2020 sio wiki ijayo!!
36dcb7e5b3a853e6adc70485d7920695.jpg
 
kila nikikaa nafikilia mambo mengi juu ya raisi wangu JPM kwanini asichukue baadhi ya mambo kwa JK mfano angeruhusu kuongea na wananchi mwisho wa mwezi tukawa tunampa kero zetu na hata kumuuliza maswali.
je wewe binafsi unge muuliza swali gani raisi JPM?
 
kumcopy jk ni sawa na kupangiwa na ukumbuke yeye si mtu wa kupangiwa..........halafu mambo ya kuongea kwa upole vile huku anasoma kwa teleprompter sio ishu!!!
 
  • Thanks
Reactions: Luv
kumcopy jk ni sawa na kupangiwa na ukumbuke yeye si mtu wa kupangiwa..........halafu mambo ya kuongea kwa upole vile huku anasoma kwa teleprompter sio ishu!!!
Huo mtindo wa hotuba za kila mwezi ulianza na mkapa...jk aliendeleza tu
 
kumcopy jk ni sawa na kupangiwa na ukumbuke yeye si mtu wa kupangiwa..........halafu mambo ya kuongea kwa upole vile huku anasoma kwa teleprompter sio ishu!!!
waambie kabisa mkulu hataki kupangiwa, hawakumsindikiza kuchukua fomu alienda mwenyewe halafu wasije wakafikiri wana uhuru kiasi hicho
 
Kila siku anaongea, Sema akiongea siku yako wewe unayemsikiliza inakuwa imeharibika kabisa
 
Habari wanajamvi.....

Nimekaa chini na kujitafakari tangu awamu hii ya tano ya Mh Magufuli kuingia madarakani hadi Leo hii naandika haya bado sijapata majibu ya tafakari langu juu ya awamu hii ya Tano...

Kwanza swali ni je wasaidizi wa Rais huwa wanaandaa hotuba ya Rais pale panapotokea Mh Rais ana mkutano???

Je kama jibu ni hapana pale ikulu wanafanya kazi gan???????

Je Kurugenzi ya mawasiliano ikulu inafanya kazi gan?

Je niku-post taarifa ya kutengua na kuteua na kuapisha tu?? kazi ya kurugenzi ya mawasiliano ikulu ni hyo tajwa hapo juu tu?

Nimejiuliza sana hadi leo sijapata jibu kwa sababu mwendo ni ule ule,

Mh Rais wetu ana nia njema kabisa na Nchi hii,anajaribu kurudisha misingi ya Taifa letu katika mstari ulionyooka,anajaribu kuleta fursa za maendeleo kama Vile amaweza kununua Ndege ambazo zitawaletea kipato Taifa na hatimaye mwananchi/wananchi,amethubutu kutoa elimu bure ingawa ina changamoto zake,

Anajaribu kuboresha miundombinu ya barabara zilizoharibika na pengine kuweka baadhi ya barabara lami...

Anajaribu kuisimamia miradi ya maendeleo kwa kuonesha ukali wake ili wasaidizi wake waweze kutekeleza miradi ya maendeleo....

Amethubutu kuanzisha ujenzi wa FLY OVER jiji la Dar es saalam ili kupunguza msururu/foleni ya magari kwenye jijj letu la Dar es salaam ambalo ndo jicho la TANZANIA,

Amethubutu kujenga hostel ya wanachuo katika chuo kikuu cha Dar es saalam UDSM wadogo zetu watasoma kwa raha bila kuhangaika KWA WALE WALIOSOMA UDSM WANAFAHAMU NENO "KUBEBANA"tumehangaika sana lakn wadogo zetu watapata neema na waitumie vizuri...

Vitu anavyovifanya ni vingi sana siwezi kuvitaja vyote YOTE TISA KUMI NI KWAMBA utavifanya vyote lakin UKIKOSEA TU MMOJA BASI inakula kwako nalo ni KUMINYA UHURU WA KUJIELEZA,UHURU WA KUPATA NA KUTOA HABARI POPOTE PALE NI JAMBO LA MSINGI SANA KULIKO KITU CHOCHOTE DUNIANI wacha watu waongee,waseme uwasikilize,uwachambue chukua wazo lao nzur la kujenga lifanyie kazi naamini utakuwa na amani siku zote katika maisha yako wala hutokosa amani hata siku moja moyoni mwako,LAKINI ukiwapuuza na kujiona wewe ndo mwenye "SAY" ya mwisho utapata sana shida....

Wape Uhuru watu waseme naamini watakusaidia.....

Kurugenzi ya mawasiliano ikulu mshaurini Rais awe anatuhutubia kila mwisho wa Mwezi na kutuambia lipi alilofanya na lipi analotarajia kulifanya kwa kuwatangazia umma,TANZANIA ni kubwa sana ukienda kijijini baadhi ya wananchi hawajui kabisa kama Rais kanunua ndege,hawajui kabisa kama Rais amezindua mradi wa kujenga "FLY OVER"katika jiji letu la DAR ES SAALAM,baadhi ya wananchi huko vijijini amabao pengine watoto wao hawasomi pengine bado wadogo hawajui kama Mh RAIS anatoa elimu bure,baadhi ya wananchi huko vijijini hawajui kama MH RAIS kawajengea watoto wao HOSTEL pale UDSM baadhi ya wananchi huko vijijini hawajui kama MH RAIS umeagiza ndege zingine

Tulitegemea wananchi wafahamu haya kupitia HOTUBA YA MH RAIS KILA MWISHO WA MWEZO maana wataji-tune mapema kwamba MH RAIS atalihutubia taifa kila mwisho wa mwezi na watakusikiliza kweli kweli....

Pia kurugenzi ya mawasiliano ikulu mshaurini Mh Rais aache kutoa HOTUBA za kukejeli umma,kuwadharau,hotuba iliyojaa vitisho,hotuba ambayo haiwavutii wananchi wake kusikiliza,hotuba iliyojaa chuki,hotuba ya kudhalilisha wananchi wake hadharani,HII ITASAIDIA PALE AMBAPO KURUGENZI YA MAWASILIANO IKULU ITAMWANDALIA MH RAIS HOTUBA,lakini niliwahi kusikia Mh Rais akisema wanaweza kuandika uwongo kama hilo ndo sababu JE HAMUWEZI KUM-FACE MH RAIS NA KUMWULIZA ANACHOTAKA KUHUTUBIA AKAWAAMBIA NA THEN MKAANDA HOTUBA NZURI ILIYOJAA BUSARA BILA KUONGEZA MANENO MENGINE????

Kurugenzi ya mawasiliano ikulu mkiweza kufanya hivo,KUANDAA HOTUBA YA RAIS NA RAIS KUHUTUBIA TAIFA KILA MWISHO WA MWEZI KWA HOTUBA ILIYOJAA HALI YA UNYENYEKEVU NAAMINI WANANCHI WATEENDELEA KUMUUNGA MKONO KWA 100% tofauti na ilivyo sasa......

Nawasilisha.....

Moderator naombeni msiuondoe huu Uzi naombeni kila mmoja ausome then tujadili kwa BUSARA
 
KAMA NINGEKUWA PRESIDA MIMI......... [emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]
■Ningeongoza na sio kutawala
■Ningesikiza zaidi kuliko kusema
■Ningejenga daraja watu wanifikie na sio ukuta niwazuie
■Ningewapa kipaumbele wenye mawazo tofauti (chanya) nami ili tuwe na uongozi wa pamoja
■Umasikini nisingeuona ndio utakatifu
■Ningewapa wananchi maneno ya faraja na sio kuwakebehi (wapige mbizi, vilaza, mashetani n.k)
■Ningewafanya wasaidizi wangu (mawaziri, wakuu wa mikoa n.k) watende kazi kwa weledi wao na sio kujipendekeza na kuiga ili niwasifu
■Ningekaa mbali na mambo yoyote yanayoweza kupelekea imani za kidini kuingia ktk mitafaruku (kuwanyima wengine uhuru wa kusema na wengine kupewa vya zaidi)
■Ningeendeleza mazuri ya watangulizi wao na kurekebisha walioposhindwa kufikia malengo bila KUWADHARAU ■Ningelishika kwa tahadhari kundi la vijana wasomi wa vyuo vikuu
■NISINGEACHA KUKIPENDELEA CHAMA CHANGU LAKINI NINGETUMIA Akili Kubwa WAPINZANI WASIPIGE MAYOWE
■NINGEWAPA SEMINA WABUNGE NA MAWAZIRI WAACHE KUONGEA MAMBO YA KITOTO MBELE YA WATU WAZIMA (Bungeni)
■Ningeruhusu uhuru wa kuona bunge live na uhuru wakukosolewa TUKIKOSEA, NISINGEKUWA UNTOUCHABLE
■Ningetumbua majipu mpk viini
■Ningeomba ushauri kwa yaliyonishinda (sukari, wanafunzi/elimu, demokrasia n.k)
■NINGERUHUSU WASHAURI WANGU WANISHAURI NA SIO MIMI NIWASHAURI WAO

°
°
°
°
[emoji767]Lawrence Eliakim
a82530730049a3ad32dcc2fc1e2cf412.jpg
 
Bahati mbaya wewe siye na sijui kama ndoto unazo.
Umemmaliza jamaa kiakili lkn
 
Kwa rangi ya mkanda wako wewe lazima utakua na ubashite tu
 
- Watu wapo mtaani wana vyeti OG.

- Watu wapo maofisini wana vyeti FEKI.

- Watu wapo maofisini hawafanyi kazi.

- WATU WAPO MTAANI WANATAKA KAZI.

#########SHIDA!!!!!!!!!!!
[bold]WAPO[/bold]
 
Mheshimiwa naandika kwa kifupi ;

Ukitaka kufanikiwa kuleta mageuzi makubwa kwenye mashirika kama Air Tanzania, TANESCO, General Tyre, Twiga Bancorp n.k tumia CEO's wenye vipaji. Duniani kote CEO's wenye vipaji ni watu wanaosakwa, wanaibwa ikiwezekana, na wanalipwa vizuri sana, na hakika wanaleta mageuzi makubwa;

Mfano tu kidogo kwa hapa Tanzania;

1. Dr. Charles Kimei - Ameweza kuitoa Benki ya Ushirika na maendeleo vijijini hadi kuwa CRDB ya leo. Fuatilia uone mageuzi makubwa yaliyofanyika
2. Nehemiah Mchechu - Kafuatilie uone ameitoa wapi NHC na sasa iko wapi
3. Ludovick Utouh - Fuatilia ujue OCAG ilikuaje kabla na baadaye aliiacha wapi.(e.g UN)

Nina mengi ya kuandika lakini niishie hapo, kwa kuwa mkubwa haandikiwi mengi, kwani unayo mengi tayari. Fuatilia duniani kote. Pata wakuu wa taasisi 'talented', hata ukiwa na board yenye watu wenye uzoefu na hizo PhD au vyovyote vile lakini 'talented CEOs' ndio mpango mzima(ila uwaache wafanye kazi sio kuwaingilia).

NB:

Kuna 'talented CEOs' ambao hawajawa CEOs bado, wengi tu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom