Miaka miwili sasa Tangu Raisi achaguliwe.
Kuna nambo mengi yamepita kwenye kipindi hiki ambayo yamegawanya maoni ya wengi.
Kuna ambao wanaona ni Chanya na wengine kuona kama ni muendelezo ule ule wa chama tawala waliofanya kwa zaidi ya miaka 50.
Watanzania wengi wana imani ya kukombolewa kiuchumi na Raisi huyu Na yeye amejigamba kwamba atawavusha watu kwenda kwenye nchi ya asali na Maziwa.
Maoni nitayaelekeza kwenye mfumo wa kodi.
Uingereza:
Nilichojifunza kwa hawa wakoloni wetu ni kwamba kampuni kubwa huwa zinalipa corporation tax kidogo. Mfano Uber, Macdonalds, Google etc. Hawa Mabwana wakubwa wanalipa tax kidogo sana, ila wanaajiri watu wengi sana.
Mfano: Uber ana madereva 40,000 jijini London. Kwa Wastani Dereva wa Uber
Watumia lita kati ya 80 hadi 100 za mafuta, iwapo serikali inachukua senti 40 Pound kwa kila Sasa ukichukua 40,000*80*0.40*52 = £66,560,000 wastani kwa mwaka, hii ni kwenye ushuru wa mafuta ya petroli tu. Hapo bado kuna Tyre, vipuri, oil n.k
Madereva wanalipa wastani kati ya £100 na £200 income tax kwa wiki. 40,000*100*52 = £208,000,000.
Hapo unaona Uber inaweza kuwa inalipa very low Corportion tax ila indirect wanaiingizia serikali ya Uingereza zaidi ya Milioni 270 za Pound kwa mwaka.
Hapa kwetu:
Msimu uliopita kulikuwa na kampuni zilizokuwa zinasafirisha mizigo kwa ndege UK to TZ. TRA walikuwa wanalipisha mizigo kwa kilo. Mimi nilikuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni.
Kwa mawazo ya haraka hataka unaweza kusema tulikuwa tunalipa kodi kidogo, lakini tulikuwa tunaingiza zaidi ya kilo 1000 kila wiki hapa nchini, mizigo yetu mara nyingi ilikuwa bi Perfum, Make UP, Vipuri vya magari n.k
Wastani wa kodi ilikuwa ni kwenye 2m to 3m a week. Kwa sababu tulikuwa tunalipa kodi kidogo na sisi tukawa tunawacharge wateja zetu shipping kidogo na wao wanawacharge wateja zao kidogo.
Sasa awamu ya 5 ilivyoanza TRA wakabadili mfumo, badala ya kilipa kwa kilo wakawa wanatulipisha kwa Thamani ya mzigo. Hii ikafanya bishara iwe ngumu ngumu kwa sababu kodi ikatoka kwenye 2/3 mil na kuwa 7/8. Wateja zetu ilabidi wapandishe bei ya bidhaa zao mara 3 ili kukava cost zetu.
Mwisho wa siku sisi sote tumefunga Biashara. Tulikuwa na wateja 10 ambao walikuwa na Wastani wa wafanyakazi wa 3. Sisi tulikuwa na vijana kama 10 walikuwa wanatusaidia kusabaza mizigo.
Hapo unaona Swissport na TRA wanepoteza 3/4 mil a week na vijana kama 40 wamepoteza Ajira. Wenye nyumba 10 wanakosa kodi, halmashauri zinakosa kodi, Tanesco inakosa pesa. Kuna gari tulikuwa tumeikodi kusambazia mizigo mwajari wake anakosa pesa, mafuta, vipuri n.k
Tunakuomba mhe Raisi usaidie kuangalia suala hili la Kodi, Mtu unaweza kuwa unalipa initial kodi ndogo lakini biashara unayoifanya inaweza kuwa na inaingiza pesa nyingi Serikalini na pia ina mchango mkubwa kwenye jamii.