Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Kiongozi huja ulizotoa ni za msingi mno kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu.Wataalamu wakodi hebu angalieni mfumo wa kodi zetu ili kuweza kuwasaidia wananchi na serikali pia
 
Kweli suala la kodi wamekurupuka na kuharibu uchumi mzimaa....mfumo mzima wa biashara umekufa!!!!
 
Wanatoza kodi ya kufa mtu matokeo yake wameua biashara nyingi nchini na hali hii kama itaendelea sidhani kama TRA wataweza kukusanya hata 300 billions kwa mwezi.

Kweli suala la kodi wamekurupuka na kuharibu uchumi mzimaa....mfumo mzima wa biashara umekufa!!!!
 
Miaka miwili sasa Tangu Raisi achaguliwe.
Kuna nambo mengi yamepita kwenye kipindi hiki ambayo yamegawanya maoni ya wengi.

Kuna ambao wanaona ni Chanya na wengine kuona kama ni muendelezo ule ule wa chama tawala waliofanya kwa zaidi ya miaka 50.

Watanzania wengi wana imani ya kukombolewa kiuchumi na Raisi huyu Na yeye amejigamba kwamba atawavusha watu kwenda kwenye nchi ya asali na Maziwa.


Maoni nitayaelekeza kwenye mfumo wa kodi.

Uingereza:

Nilichojifunza kwa hawa wakoloni wetu ni kwamba kampuni kubwa huwa zinalipa corporation tax kidogo. Mfano Uber, Macdonalds, Google etc. Hawa Mabwana wakubwa wanalipa tax kidogo sana, ila wanaajiri watu wengi sana.

Mfano: Uber ana madereva 40,000 jijini London. Kwa Wastani Dereva wa Uber
Watumia lita kati ya 80 hadi 100 za mafuta, iwapo serikali inachukua senti 40 Pound kwa kila Sasa ukichukua 40,000*80*0.40*52 = £66,560,000 wastani kwa mwaka, hii ni kwenye ushuru wa mafuta ya petroli tu. Hapo bado kuna Tyre, vipuri, oil n.k

Madereva wanalipa wastani kati ya £100 na £200 income tax kwa wiki. 40,000*100*52 = £208,000,000.

Hapo unaona Uber inaweza kuwa inalipa very low Corportion tax ila indirect wanaiingizia serikali ya Uingereza zaidi ya Milioni 270 za Pound kwa mwaka.


Hapa kwetu:

Msimu uliopita kulikuwa na kampuni zilizokuwa zinasafirisha mizigo kwa ndege UK to TZ. TRA walikuwa wanalipisha mizigo kwa kilo. Mimi nilikuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni.

Kwa mawazo ya haraka hataka unaweza kusema tulikuwa tunalipa kodi kidogo, lakini tulikuwa tunaingiza zaidi ya kilo 1000 kila wiki hapa nchini, mizigo yetu mara nyingi ilikuwa bi Perfum, Make UP, Vipuri vya magari n.k

Wastani wa kodi ilikuwa ni kwenye 2m to 3m a week. Kwa sababu tulikuwa tunalipa kodi kidogo na sisi tukawa tunawacharge wateja zetu shipping kidogo na wao wanawacharge wateja zao kidogo.

Sasa awamu ya 5 ilivyoanza TRA wakabadili mfumo, badala ya kilipa kwa kilo wakawa wanatulipisha kwa Thamani ya mzigo. Hii ikafanya bishara iwe ngumu ngumu kwa sababu kodi ikatoka kwenye 2/3 mil na kuwa 7/8. Wateja zetu ilabidi wapandishe bei ya bidhaa zao mara 3 ili kukava cost zetu.

Mwisho wa siku sisi sote tumefunga Biashara. Tulikuwa na wateja 10 ambao walikuwa na Wastani wa wafanyakazi wa 3. Sisi tulikuwa na vijana kama 10 walikuwa wanatusaidia kusabaza mizigo.

Hapo unaona Swissport na TRA wanepoteza 3/4 mil a week na vijana kama 40 wamepoteza Ajira. Wenye nyumba 10 wanakosa kodi, halmashauri zinakosa kodi, Tanesco inakosa pesa. Kuna gari tulikuwa tumeikodi kusambazia mizigo mwajari wake anakosa pesa, mafuta, vipuri n.k

Tunakuomba mhe Raisi usaidie kuangalia suala hili la Kodi, Mtu unaweza kuwa unalipa initial kodi ndogo lakini biashara unayoifanya inaweza kuwa na inaingiza pesa nyingi Serikalini na pia ina mchango mkubwa kwenye jamii.
Hakuna hoja hapo ni kutafuta huruma tu na nyie ndiyo mlikuwa mnakula na watumishi wasiokuwa waaminifu wa TRA.

Taarifa ya TPA ni kuwa mizigo imepungua Bandarini lakini makusanyo ya mapato yameongezeka na wewe ni mmojawapo wapo wa mliojiondoa wenyewe ktk biashara.

Wafanyabiashara makini wataendelea na biashara zao na wafanyabiashara wababaishaji wanaondoka wenyewe.
 
Hoja yako kuhusu kulinda biashara kama vyanzo vya kodi au mapato ni nzuri sana tena inahitaji tafakari.

Hoja ya kutoza kodi kwa kupima uzito ni ya ovyo sana. Hii ilikuwa inaumiza serikali na baadhi ya watu walio ingiza vitu vizito ambavyo vina thamani ndogo.
Kwa upande mwingine viliwafaidisha sana wale wanaoleta vitu vyepesi lakini vina thamani kubwa sana.

Nafikiri hata huko U.K. ulikowasifia au kuwatolea mfano kodi zao hazitozwi kwa kuangalia uzito bila kujali thamani ya kitu.
 
Hakuna hoja hapo ni kutafuta huruma tu na nyie ndiyo mlikuwa mnakula na watumishi wasiokuwa waaminifu wa TRA.

Taarifa ya TPA ni kuwa mizigo imepungua Bandarini lakini makusanyo ya mapato yameongezeka na wewe ni mmojawapo wapo wa mliojiondoa wenyewe ktk biashara.

Wafanyabiashara makini wataendelea na biashara zao na wafanyabiashara wababaishaji wanaondoka wenyewe.
 
Kutoza kodi kwa kupima uzito bila kuangalua thamani ni biashara kichaa.

Chukulia mfano boksi lililojazwa iphone 7 lingetozwa kodi ndogo kuliko jingine lenye ukubwa sawa limejazwa betri za gari za acid. Wakati vitu vilivyomo vikienda kuuzwa huyu mwenye box la iphone 7 angepata faida mara 60 zaidi ya mwenye boksi la betri.

Serikali zilizopita zililala usingizi mzito na walipo amka ilikuwa wanakumbuka kwenda kuomba misaada tu, mwisho tukaambiwa tuwe tuna oana jinsia moja ili tupewe misaada.
 
Hakuna hoja hapo ni kutafuta huruma tu na nyie ndiyo mlikuwa mnakula na watumishi wasiokuwa waaminifu wa TRA.

Taarifa ya TPA ni kuwa mizigo imepungua Bandarini lakini makusanyo ya mapato yameongezeka na wewe ni mmojawapo wapo wa mliojiondoa wenyewe ktk biashara.

Wafanyabiashara makini wataendelea na biashara zao na wafanyabiashara wababaishaji wanaondoka wenyewe.

Sawa, TPA wakipato kimeongezeka.

Lakini kwingine kipato kimeshuka.

Imagine zilikuwa zinaingia contena 100 kwa mwezi. Kusafirisha utahitaji malori 100, madereva 100, utingo 100, Diesel etc. Kwenye hizo labda Serikali inapata bil 1.

Sasa hivi unapitisha ma contena 50, ila maana nusu ya malori hayana kazi, nusu ya madereva hawana kazi, utingo, Diesel, Insurance, Road Lincence, Mama ntilie pia atauza chakula nusu, faini barabarani zitakuwa kidogo. Ni mlolongo mrefu sana.

Kingine cha kuangalia, Dereva akipata Mshahara matumizi yake yana athari moja moja mtaani. Atanunua chakula, Sokoni, ataenda bar, atalipa kodi ya nyumba anayokaa, n.k

Na Serikali ikipata mapato yake, itaendelea kuwalipa wale wale wafanyakazi wake aliokuwao nao kwa zaidi ya miaka 50. Hakuna wafanyakazi wapya ataoajiri kwa sababu shughuli zimepungua, pia Serikali inaoelekeza pesa yake kwenye miradi ambao ni future lakini wengine hawaielewi. Ndio ile watu wa Nape walimuuliza maana ya Bombardier.

Natumai hoja yako nimeijibu.
 
Hoja yako kuhusu kulinda biashara kama vyanzo vya kodi au mapato ni nzuri sana tena inahitaji tafakari.

Hoja ya kutoza kodi kwa kupima uzito ni ya ovyo sana. Hii ilikuwa inaumiza serikali na baadhi ya watu walio ingiza vitu vizito ambavyo vina thamani ndogo.
Kwa upande mwingine viliwafaidisha sana wale wanaoleta vitu vyepesi lakini vina thamani kubwa sana.

Nafikiri hata huko U.K. ulikowasifia au kuwatolea mfano kodi zao hazitozwi kwa kuangalia uzito bila kujali thamani ya kitu.

Kihusu kupima uzito:
Hii ilikuja kutokana na aina ya mzigo tuliokuwa tunaleta.

Wateja zangu walikuwa ni hawa wanaouza nguo na vipodozi. Pia na mmoja likuwa specialist ya European Cars.

Sasa Tungesema kila nguo waipe value na kuitoza kodi inamaana kila t shirt ingelipiwa shs 2000/3000 kodi tu. Sasa wewe mtaani ungeipata kwa gharama ya juu zaidi.

Na process hiyo ya kufungua kila box ku value kila t shirt, ufungue file , uprint karatasi , ingewa cost TRA muda na gharama kubwa kuliko kugeneralise kwa kilo. Mzigo mmoja wa kg 1000 ungewachukua si chini ya wiki hadi 3. Pia kama unavyojua Server za TRA zinakuwa down mara kwa mara.

Na sio kwamba walikuwa wanaangalia kwa nje, mzigo ulikuwa unapitia keenye scan kwanza, wakijitisdhisha kama ni vitu vile vile vya kila siku mzigo unapita.
 
Rais Magufuli, nakuomba na kukusihi sana katika nia zako njema za kuiletea maendeleo Tanzania, Punguza Hasira, Kiburi na Ujuaji. Ukifanya hivyo utafanikiwa.
 
Kwanza nikupongeze kwa jitihada zako za kulitumikia taifa.

Leo nimependa pia nitumie fursa hii kukumbusha kwamba muda wa urais ni miaka mitano au kumi tu!

Hivyo basi usisahau kujiwekea hazina yako huku mtaani pindi utakapostaafu. Hazina ninayoongelea ni kuwa na utu, kutenda haki, kuepuka kudhalilisha na kunyanyasa wengine ili kujipatia sifa binafsi, kuepuka kulipiza kisasi kwa wale usiowapenda n.k.

Kumbuka yale uwatendeao wenzako sasa kwa kuwa tu una madaraka ya kufanya hivyo ujue ndivyo hivyo hivyo utskavyotendewa siku haya madaraka uliyonayo yatakapokoma.

Mh rais, achana na wapambe kama kina bashite na wengineo wanaokudanga eti unaweza kujiongezea muda wa kutawala eti kwa sababu unapendwa sana. Mh rais, kwa hali halisi ya nchi yetu na sociodemographic characteristic zake hutoweza kamwe kujiongezea muda wa utawala wako. Labda kama umeamua kuiweka nchi rehani!

Kwa kuzingatia hayo basi, makushauri uzingatie ushauri huo hapo juu ili muda wako ukiisha uendelee kufurahia maisha ya kustaafu kwa raha mustarehe.
 
Mji wa mwanza ni mji wa pili Tanzania unaokuwa kwa kasi ya ajabu. Hivi sasa kumeanza kuwa na Tatizo la traffic Jam hasa mida ya asubuhi na Jion.

Sioni kuwa ni busara serkal kusubiri mpaka Tatizo liwe kubwa ndyo solution Itafutwe. Ni vyema Mh Rais utuletee mabasi ya mwendo kasi hata matano tu ili tuanze kuyazoea mapema.
9b332242959f3fc08c61a994197414ef.jpg


MWART.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom