1. Program ya Bima ya afya katika ngazi ya jamii ilivyoanza kutekelezwa ni wilaya ya Igunga chini ya Mkuu wa Wilaya wakati huo Elibariki Kingu alitekeleza program hiyo kwa asilimia 100.
2. Kati ya wilaya iliyofanya vizuri katika kuwawezesha vijana hasa kwenye miradi ya kilimo (vitunguu, mbogamboga). Ni wilaya ya Igunga chini ya Elibariki Kingu ilikuwa ni wilaya bora. Mpaka Mh. Rais Jakaya Kikwete alienda kutembelea mradi huo.
3. Ni wilaya ya Igunga chini ya Elibariki Kingu vijana walipata fursa na kupata mikopo na kujishughulisha na ufiatuaji wa matofali ya Hydroblocks.. Kingu alifanikiwa kutafuta wafadhili wa kuwapa vijana mikopo na mashine husika..
4. Kingu alifanikiwa kufungua fursa za kibiashara kwa vijana hao. Ambao kwa sasa SACCOS ya vijana hao ina fedha zaidi ya million 872..
5. Kingu alifanikiwa kuwawezesha wakina mama kwa kuwatafutia wafadhili kutoka China na Uganda ili wawape mafunzo na nyezo za kujihusisha na ufugaji na kilimo cha kisasa. Ikiwa ni pamoja na kuwapa mbegu za hybrid..
Infact, kwa miaka miwili mfululizo 2012, 2013. Wilaya ya Igunga ilikuwa ni bora iliyotunukiwa cheti cha ubora. Na mkuu wa wilaya wa wakati huo Elibariki Kingu alitangazwa kuwa mkuu wa wilaya aliyefanya vizuri katika kutekeleza majukumu yake..
Kwa sasa Kingu kashinda ubunge wa jimbo la Singida Magharibi. Ni wazi kama Magufuli anataka vijana wachapakazi, waliopikika moja wao ni Elibariki kingu. Rais Magufuli, Kingu atakuwa msaada kwako sana. Na hasa ukianza naye kwa nafasi ya unaibu for the future atakuwa potential katika hii nchi...
Ni mtiifu, mchapakazi na ana rekodi ya kuwa DC bora kwa miaka 2 mfululizo... Huu ndio muda wa kufanya kazi na vijana kama hawa, ambao ni asset katika Taifa... !