Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Pitia mikataba yoote!; ile ya kifisadi ivunje! ondoa wabunge woote wa viti maalum; pesa itakayo patikana iwekezwe kwenye elimu ya vijana wetu...
 
Katika baraza lake la mawaziri, tashtushwa sana iwapo waziri mkuu hatokuwa MWAKYEMBE na waziri wa nishati hatokuwa Prof. MUHONGO.
Hawa jamaa ni wasaidizi wa rais muhimu sana kwenda na kasi yake.
LUKUVI apewe wizara ya uchukuzi akashughulike na wizi pale.
Mambo ya nje, JANUARI MAKAMBA,
Spika, Zungu
Fedha, MIGULU.

Mlizowea enzi za JK kupiga kampeni zenu na ikawa hivyo, hapa mmenoa. Na kama Magufuli angenisoma vyem hao wote mnaowapigia chepuo humu wasionekane maana tunao wengi wenye uwezo zaidi ya hao. Muhongo yes lqkini Harison ninamashaka na mamvo fulani kama ya kule kaskazini.
 
1.TRA wapewe malengo monthly kwa kuanzia 1.5 trillion kwa mwezi by 2016 iwe 2 trillion kwa mwezi ingawa pia unaweza commission study kujua how much is TRA suppose to collect monthly.
2.Bandari ya dsm iboreshwe kwa ukifuatilia na kuzifanyia kazi kwa nini watu huikwepa na kutumia ya Mombasa.
3.Kodi zilipwe na watu wote wakubwa kwa wadogo kuna vigogo hawalipi kodi pia wabunge nao walipe PAYEE
4.Simamia TRL na Tazara wasafirishe mizigo ya kutisha kuzilinda barabara zetu
5.Bandari ya Mtwara na TANGA ziendelezwe kama mbadala wa Dsm.
6.Fast track matumizi ya gesi ya Mtwara majumbani ili kuokoa mazingira ie kuni na mkaa matumizi yapungue kama sio kwiaha.
7.Umeme wa mkaa kule Kyela na Ngaka uanze kama plan B ya gesi na pia ule wa Maji tuachane nao ili Maji yatumike kwa litigation in full.
8.Kilimo cha umwagiliaji kitiliwe mkazo na kilimo chote kwa ujumla wake kitiliwe mkazo maana watz wengi wako uko ie soko LA uhakika mbolea na pembejeo mda mwafaka.
9.Mgodi wa chuma uanze ili kuweza tumia kwenye uzalishaji wa vitu vinavyotumia chuma kama malighafi
10.Fufua viwanda vilivyokufa kama Tanganyika packers general tyre Mbeya textile zzk urafiki etc
11.PAYEE ipungue kama ilivyokuwa ahidi
12.Mawaziri wapewe mikataba
13.Utalii uendelezwe kuanzia kuhakikisha tembo na faru na wanyama wengine wanalindwa,kufungua safari za anga kwa kufurai ATC pia charges zetu ziangaliwe kwa national parks as kuna watu wanataka Tz kwenda Masai Mara kisa rates zetu ziko juu hasa foreigners
Nilipata point zingine ntaongeza
 
Watanzania wengi wamekuwa na mhemko mkubwa wa kutaka kuona Rais JPM akiunda na kulitangaza baraza lake la mawaziri mapema.

Mimi, kwa mawazo yangu niko kinyume chake, nilikuwa nashauri mhe Rais aende mwendo mdogo mdogo hata ikimchukua miezi mitatu kukamilisha kabineti haina shida, mradi ajiundie baraza la mawaziri lililo bora, asifanye haraka anaweza kubandika hata mijitu ya ovyo ovyo kama alivyofanya mtangulizi wake alipojiteulia baraza lililokuwa na mawaziri na manaibu 69 na likawa ni la kukarabatiwa na kuvunjwa vunjwa kila mara.

Mheshimiwa Rais, anajua mambo mazuri hayataki haraka, na kwa sababu anatakiwa achague mawaziri kutoka miongoni mwa wabunge, ambao wengi wao ni wapya ambao kiutendaji hawajui aachwe afanye mambo yake taratibu atawapata tu mawaziri walio bora asiturudishie tena ile mizigo ya Kikwete.
 
Watanzania wengi wamekuwa na mhemko mkubwa wa kutaka kuona Rais JPM akiunda na kulitangaza baraza lake la mawaziri mapema.

Mimi, kwa mawazo yangu niko kinyume chake, nilikuwa nashauri mhe Rais aende mwendo mdogo mdogo hata ikimchukua miezi mitatu kukamilisha kabineti haina shida, mradi ajiundie baraza la mawaziri lililo bora, asifanye haraka anaweza kubandika hata mijitu ya ovyo ovyo kama alivyofanya mtangulizi wake alipojiteulia baraza lililokuwa na mawaziri na manaibu 69 na likawa ni la kukarabatiwa na kuvunjwa vunjwa kila mara.

Mheshimiwa Rais, anajua mambo mazuri hayataki haraka, na kwa sababu anatakiwa achague mawaziri kutoka miongoni mwa wabunge, ambao wengi wao ni wapya ambao kiutendaji hawajui aachwe afanye mambo yake taratibu atawapata tu mawaziri walio bora asiturudishie tena ile mizigo ya Kikwete.

Hatamie nakuunga mkono, nadhani aanze na mawaziri wachache, aanze na waziri mkuu waziri wa fedha waziri wa ulinzi na waziri wa mambo ya ndani badae asubirishie kidogo.
 
Unda tume maalum ya kuchunguza uhusiana kati ya viongozi wa umma na ujenzi wa kutisha wa majumba kila kukicha nchi nzima.
Tume hiyo iweke kumbukumbu zinazoonyesha ni kiongozi gani anayemiliki utajiri mkubwa na rasilimali nyingi nchini na kama analipa ushuru au la.
Hii itaepusha watumishi wa umma kuiibia serikali na kujilimbikizia mali.
Kuna watumishi wa kada ya kati kwenye idara mbali mbali ambao ni mabilionea kwa ufisadi na wanafumbiwa macho kwasababu tu sio wanasiasa. Tume iwachunguze wote nchi nzima kubaini kuwa kiongozi mmoja ana nyumba ngapi,miradi kama mabaar magesti na malori au mabasi mangapi na amezipataje mali hizo.
 
Matumizi ya dollar ktk mihamara (transactions ) yafutwe hapa nchini. Kuna hii kampuni ya Dstv - Multichoices Tanzania malipo yao ni kwa dollars ndio maana malipo yao kwa mwezi ktk "packages " zao huongezeka kila mara of which ni mzigo kwa wateja wake.
 
MH Rais, Naomba sisi watumishi Wa umma tuliomba kuuziwa nyumba za TBA za mabwepande, turuhusiwe kulipa asilimia kadhaa ya bei ya kuuza, tuhamie then tupangiwe kiasi cha kulipa kwa mwezi. Tulipe kiasi hicho tukistaafu au umri Wa kukopa PSPf ukifika tumalizie deni
TBa wametuambia tukope benki tuwalipe taslim wanayotaka. Kukopa benki mtumishi Wa umma ili kununua nyumba ya kuishi ya serikali ni kujitia umaskini. PSE mhe sikia kilio chetu watumishi Wa umma tunaolipa kodi nyumba za kupanga huku tukitafuta pesa ya kununua taslim ya m70, m68, m50. MH mtumishi muadilifu Wa kawaida hawezi kuwa Na hizo millions taslim za kulipa
 
Mheshimiwa Rais angalia tena tofauti kubwa ya Mishahara ya watumishi Wa umma. Wale Wa serikali kuu wasiozalisha au kukusanya mapato Na wale Wa Executive agencies. Fringe benefits zina tofauti kubwa. Kuna watumishi wamekuwa matajiri kwa Mishahara minono Na posho humo hump serkalini wengine wakiishi kama hayawani. Tafadhali mheshimiwa tofauti hii ifanyiwe kazi
 
MH Rais, Naomba sisi watumishi Wa umma tuliomba kuuziwa nyumba za TBA za mabwepande, turuhusiwe kulipa asilimia kadhaa ya bei ya kuuza, tuhamie then tupangiwe kiasi cha kulipa kwa mwezi. Tulipe kiasi hicho tukistaafu au umri Wa kukopa PSPf ukifika tumalizie deni
TBa wametuambia tukope benki tuwalipe taslim wanayotaka. Kukopa benki mtumishi Wa umma ili kununua nyumba ya kuishi ya serikali ni kujitia umaskini. PSE mhe sikia kilio chetu watumishi Wa umma tunaolipa kodi nyumba za kupanga huku tukitafuta pesa ya kununua taslim ya m70, m68, m50. MH mtumishi muadilifu Wa kawaida hawezi kuwa Na hizo millions taslim za kulipa
 
Nina muomba Rais aunde Baraza la mawaziri dogo kama la awamu ya kwanza hii ni kutokana na uchumi wetu ulivyo hivi sasa .,...
 
ninachoweza kumshauri mh.rais magufuli ambao pia ni ushauri au agizo nililopewa na Mungu Ni:

>watanzania Wamekua Wakinunua Hotuba Ya Rais Wao
>watanzania Wamekua Wakinunua Bunge La Kwao,ambapo Wana Haki Ya Kuckiliza Na Kujua Kinachoendelea Ili Waweze Kushauri Na Kutoa Maoni Vzr. Hii Imetokana Na Kubadili Mfumo Kutoka Analog Kwenda Digitali Ambao Umepelekea Hata Chanel Za Ndani Kupata Mpk Ulipie Wkt Kipato Cha Mtanzania Bado Kipo Chini.

Hivyo Ushauri Au Agizo, Ni Kuamuru Kampuni Zenye Ving'amuzi, Chanels Zote Za Ndani Itv, Tbc, Chanel10, Eatv, Clouds, Startu Ziwe Buree Kabsa Na Mtu Akitaka Chanel Zile Zingne Ndio Alipie.
 
1. Program ya Bima ya afya katika ngazi ya jamii ilivyoanza kutekelezwa ni wilaya ya Igunga chini ya Mkuu wa Wilaya wakati huo Elibariki Kingu alitekeleza program hiyo kwa asilimia 100.

2. Kati ya wilaya iliyofanya vizuri katika kuwawezesha vijana hasa kwenye miradi ya kilimo (vitunguu, mbogamboga). Ni wilaya ya Igunga chini ya Elibariki Kingu ilikuwa ni wilaya bora. Mpaka Mh. Rais Jakaya Kikwete alienda kutembelea mradi huo.

3. Ni wilaya ya Igunga chini ya Elibariki Kingu vijana walipata fursa na kupata mikopo na kujishughulisha na ufiatuaji wa matofali ya Hydroblocks.. Kingu alifanikiwa kutafuta wafadhili wa kuwapa vijana mikopo na mashine husika..

4. Kingu alifanikiwa kufungua fursa za kibiashara kwa vijana hao. Ambao kwa sasa SACCOS ya vijana hao ina fedha zaidi ya million 872..

5. Kingu alifanikiwa kuwawezesha wakina mama kwa kuwatafutia wafadhili kutoka China na Uganda ili wawape mafunzo na nyezo za kujihusisha na ufugaji na kilimo cha kisasa. Ikiwa ni pamoja na kuwapa mbegu za hybrid..

Infact, kwa miaka miwili mfululizo 2012, 2013. Wilaya ya Igunga ilikuwa ni bora iliyotunukiwa cheti cha ubora. Na mkuu wa wilaya wa wakati huo Elibariki Kingu alitangazwa kuwa mkuu wa wilaya aliyefanya vizuri katika kutekeleza majukumu yake..

Kwa sasa Kingu kashinda ubunge wa jimbo la Singida Magharibi. Ni wazi kama Magufuli anataka vijana wachapakazi, waliopikika moja wao ni Elibariki kingu. Rais Magufuli, Kingu atakuwa msaada kwako sana. Na hasa ukianza naye kwa nafasi ya unaibu for the future atakuwa potential katika hii nchi...

Ni mtiifu, mchapakazi na ana rekodi ya kuwa DC bora kwa miaka 2 mfululizo... Huu ndio muda wa kufanya kazi na vijana kama hawa, ambao ni asset katika Taifa... !

Mh Rais watu wa jinsi hii ni muhimu sana kuwapa nafasi ili vipaji vyao vikaisaidia nchi.

Naongezea kuangalia hawa wakuu wa wilaya na wakurugenzi wengi wao ndiyo wakwamishaji wakubwa wa miradi ya maendeleo maana wamekaa ki maslahi binafsi na ki itikadi ya vyama. Kwa heshima na taadhima tumia vijana wabunifu na wenye uthubutu kama Kingu ili maendeleo yetu yasonge mbele kwa uhakika na uharaka unaitakikana. Kwa rasilimali tulizonazo ni aibu kukuta wilaya yenye umasikini Tz.

Mh Rais TAMISEMI uifumue na kuiunda upya ili iitwe wizara ya Kilimo na maendeleo vijijini. Hii itasaidia kukusanya nguvu za kutosha kuipeleka vijijini ambapo kilimo ndiyo ajira number 1; pia itaondoa migongano kati ya wizara hii na ile ya kilimo na mifugo...kilimo ni agriculture yaani kinahusisha mazao, mifugo, samaki na misitu ambapo utaona watendaji wote hao wapo TAMISEMI.... Sasa ukiwaweka chini ya wizara moja ukatofautisha kurugenzi zake utaua wizara nyingi na hivyo kupunguza ukubwa wa serikali wakati huo huo kuongeza tija jatika utendaji na maendeleo. Mh Rais sera ya hiyo wizara na utejelezaji wake ipo tayari na kama utashawishika basi ukiwaona baadhi ya viongozi wa chadema wa mwaka jana watakupatia. Haina hati miliki iliandikwa bure kwa faida ya watanzania wote. Huhitaji hata kuuliza wewe chukua kinachoendana na mawazo yako na yale yasiyofaa achana nayo.
 
Maudhui ya huu uzi nikumwombea mama Anna hisani au ni kwaajili ya ushauri kwa mh.pombe?manake siwaelewi kabisa
 
Dada Yangu Kipenzi Mimi Sishauri Apewe Cheo Chochote Kwani Hata Kikwete Tulimwomba Ampe Cheo James Mbatia Lakini Nadhani Uliona Shukrani Yake Kwake Kwa KUMTUKANA. Huruma Ya Kikwete Ndiyo IMEMUHARIBIA. Hako Ka Mama Hakatakuwa Na Tofauti Ya MNAFIKI ALIYETUKUKA Mbatia.

Akili za ccm bwana? Yaani mlitaka mbatia awe mnafiki kisa kapewa ubunge wakuteuliwa? Sisi tuliopita seminary nyeusi ni nyeusi nyeupe ni nyeupe,usitufundishe unafiki
 
Kama unaamini katika uwazi kwenye serikali yako, kuna jambo unaweza kujifunza kutoka Kenya

Michakato ya tender zote zinazotolewa katika ngazi yeyote ya serikali huwekwa wazi kwenye mtandao wa serikali ambapo kila mtu anaweza kusoma.

Hii inahusisha kutangazwa tender, wazabuni walioomba, wazabuni walioteuliwa kwa ajili ya mchujo na sababu zake, na mzabuni aliyepatiwa tender na vigezo vilivyotumika.

Kwa kiasi kikubwa hii hupunguza malalamiko na upendeleo kwenye suala la mikataba ya tender
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom