Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Wadau, namuomba sana Mh Rais Magufuli wakati huu ambao anaunda safu yake ya uongozi, aachane kabisa na wachumia tumbo na wanafiki wanaojipendekeza aina ya Polepole, please Mh Rais kaa nao mbali sana hawa watu, usiwafikirie hata u DC.
 
mchawi mkabidhi mtoto,
mwache ampe Polepole u-DC tuone kama ofisi ni camera za TV stations.
 
Hakuna suluhu kwa wezi wa kura... CCM haina uhalali wa kutawala nchi hii ....
 
Enyi ukawa msimuharibie rais magufuli mipange yake kwa kutaka kukomoa watu. Na yeye anakili yake msidhani yeye ni mjinga hafahamu wachapa kazi ktk serikali ya kikwete iliyomaliza muda wake.
 
Mkuu naomba serikali yako ya awamu ya 5 ikamilishe suala la kuifanya Dodoma makao makuu ya nchi. Tuuache mji wa Dar kuwa wa kibishiara tu ili kupunguza fujo za barabarani.
 
Ianze kwanza Ikulu ihamishiwe Dodoma,,,aanze kuonesha mfano kwa kuhamia rasmi dodoma
 
Dodoma mtabaki na hospitali ya milembe tu ndio inawafaa.
 
Ukawa msione vyaelea, ... Hayo mnayomsimami Magufuri mngemsimamia hivyo hivyo Mbowe asingewachanganya kama karanga
 


Je waliotaka Lowasa awe Rais? Hivi sura yetu tungeiweka wapi jamani dunia ingetushangaa!!!
 

Hujachana na siasa za majitaka tu? Nilijua umeshanza ile kazi yako kubwa,
 
Kama kuna kero wanayopata wafanyabiashara ni vizuizi visivyo vya lazima barabarani. Vizuizi hivi vimekuwa miradi ya maaskari wakinyanyasa wananchi pindi wanapopita kwenye hivi vizuizi. Mfano hai ni kizuizi kilichopo eneo la KIRUMI Mkoa wa Mara. Wafanyabiashara wanaopeleka mifugo yao nchi jirani wakiwa na vibali vyote wakifika kwenye kizuizi cha Kirumi basi wanasumbuliwa sana na bila kuacha chochote huwezi kupita. Juzi nimepita pale naona kizuizi hicho kimeondolewa lakini nadhani ni suala la muda tu muda siyo mrefu kitarudishwa. Kizuizi kingine ni kile kilichopo mpakani mwa Simiyu na Mara pale karibu na Ndabaka Gate hapa pia wafanyabiashara wanasumbuliwa sana. Chonde chonde Mhe. Rais tulikupigia kura tukifahamu kuwa utakomesha dhuluma dhidi yetu tunakuomba sana tusaidie tumeteseka muda mrefu.
 
Hii ni ombi ya watanzania tuliyowengi baada wizara hii kuongozwa na wizara kibao inayowachanganya watendaji m.f kuna tamisemi wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi mara jinsia na watoto ni full vurugu match.

Aidha ukaguzi wa shule ipewe kipaumbele kwa rasilimali watu na fedha kuinusuru elimu nchini.
 
Ushauri wangu/Mapendekezo yangu:

1. Bw. Magufuli apunguze papara. Ana muda wa kutosha sana wa kuhakikisha kila maamuzi anayofanya yanazingatia taarifa sahihi na tathmini ya kutosha.

2. Njia thabiti ya kuboresha utendaji serikalini ni "civil service reform". Mfumo wa utumishi wa umma unahitaji kufumuliwa. Mpango wa kupandisha watu vyeo kwa utaratibu wa mserereko hauna nafasi katika dunia ya leo. Hakuna maana kuwa na watu 25 wanaofanya kazi inayoweza kufanywa na mtu mmoja. Utaratibu wa Rais kuteua watendaji katika nafasi mbalimbali ni kulea uzembe. Weka ushindani katika kupata watu wa kujaza nafasi mbalimbali. Hakuna sababu ya Rais kuteua Mkurugenzi wa Hospitali ya Muhimbili. Huko ni kulea uzembe. Serikali ihakikishe inakuwa kwenye nafasi ya kugombea wafanyakazi wazuri na sekta binafsi. Mtu achague kufanya kazi serikalini badala ya Vodacom. Inawezekana.

3. Mawaziri/watendaji waakuu serikalini wasiwe na hisa/maslahi kwenye biashara ambazo wana wajibu wakuzisimamia kama regulators. Huwezi kuwa Waziri wa Mawasiliano wakati una maslahi binafsi kwenye kampuni za simu. Huwezi kuwa Waziri wa Maliasili wakati una maslahi binafsi katika makampuni ya utalii. Huwezi kuwa Waziri wa Nishati au Bosi wa TPDC wakati una maslahi binafsi kwenye makampuni ya mafuta. Na athari za mambo haya zilikuwa bayana kwenye utawala uliopita.

4. Embrace spirit ya kuwa na "lean government". Cheo cha Naibu Waziri na Naibu Katibu Mkuu havina maana. Vina lengo la kuongeza nafasi kwa ajili ya "washkaji". Vivyo hivyo, vyeo vya Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya havina maana. Kama una nia ya kututoa hapa tulipo, futa vyeo hivi. Usisubiri Katiba Mpya maana hatutaipata.

5. Nyumba za Serikali ziliuzwa kwa utaratibu ambao si halali. Unafahamu vizuri jambo hili. Anzisha mchakato wa kurudisha nyumba hizi serikalini, wewe mwenyewe ukianza kurudisha nyumba ulizonunua/ulizojigawia. Utajipatia heshima kubwa nchi hii ukitekeleza jambo hili.

6. Kujaribu kupunguza "inbreeding of ideas"/contamination, chagua mawaziri wapya kabisa. Yeyote ambaye alipata kuwa waziri asipate nafasi kwenye baraza lako la mawaziri. Ukirudisha mawaziri wazoefu, watakukwamisha. Walishazoea uzembe. Ni afadhali kuanza na "newbies', utaweza kuwa-shape unavyotaka. Kina Wassira, Membe, Mwakyembe etc watakusumbua.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…