Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Maji bado ni tatizo kubwa nchini. Suluhu ni kuimarisha hiyo wizara na kuwajibisha wazembe...
 
Eti ivunjwe...hahaaaaa, we sema ipewe kipaumbele tu, maji ni hitaji muhimu sana kwa maisha, na kila nchi dunia nzima ina wizara ya maji kwa taarifa yako.
 
Umesoma wapi?
Mto Nile unaanzia Jinja nchini Uganda ila Bonde lake linaanzia sehemu nyingi ikwemo Tanzania, Burundi, Rwanda, Kenya, DRC na kwingine.

Ukishataja Ziwa Victoria huna haja ya kutaja Mto Nile. Katika Tanzania hatuna jina linaloitwa mto Nile ila tuna Taasisi ya Kimataifa inayosimamia Bonde la Mto Nile ambapo Ziwa Victoria ni sehemu ya Bonde hilo.
 

Kwaiyo inamaanisha kuna source ya mto nile na pia kuna uwezo wakutafuta chanzo cha maji pale?
 
Eti ivunjwe...hahaaaaa, we sema ipewe kipaumbele tu, maji ni hitaji muhimu sana kwa maisha, na kila nchi dunia nzima ina wizara ya maji kwa taarifa yako.

kwa ufahamu wako wizara ya maji kazi yake nini..
 
Ishu ni kwa serikali kuipa kipaumbele kwa kuwapa bajeti ya kutosha kufanya uwekezaji wa kutosha. Je unafahamu mitambo ya Ruvu Juu na Ruvu Chini ilijengwa lini?
 
The Nile has two major tributaries, the White Nile and Blue Nile. The White Nile is considered to be the headwaters and primary stream of the Nile itself. The Blue Nile, however, is the source of most of the water and silt. The White Nile is longer and rises in the Great Lakes region of central Africa, with the most distant source still undetermined but located in either Rwanda or Burundi. It flows north through Tanzania, Lake Victoria, Uganda and South Sudan.
 
Wizara imelala sana. Huku iringa gharama ya kuunganisha maji ni kubwa kuliko umeme. Wizi mtupuu idara ya maji iringa na wizara ipo
 
Kwa taarifa yako Mto Nile unaanzia ziwa victoria ndani ya nchi ya Uganda. Acha ubishi soma
mto nile unaanzia rwanda, burundi na congo kijeografia hakuna mto unao anzia ziwani. maji ya mto kagera yanayopita ziwa victoria haya changanyiki na maji ya ziwani yana pita ziwani kama mto
 
Nchi yoyote inayotaka kuendelea lazima iwe na dira ya maendeleo, uongozi mzuri na watu wazalendo kwa taifa lao. Taifa letu kwa muda mrefu limekua tegemezi kwenye jumuiya za kimataifa na kwa kiasi kikubwa tegemezi kwenye bajeti ya maendeleo. Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi na amani surprisingly hatua za maendeleo zimekua hazilingani na mibaraka hii aliyotupatia mwenyezi Mungu.


Nchi nyingi za Afrika ikiwamo Tanzania zimekua zikilalamikiwa kwa kuendekeza anasa na matumizi yasiyokua ya lazima., matumizi makubwa ya serikali yasiyoendana na ukuaji wa uchumi na uhalisia wa hali ya kiuchumi ni moja ya mambo yanayorudisha nyuma maendeleo ya nchi kwa pesa nyingi za serikali kwenda kwenye matumizi yasiyo ya lazima na pesa kidogo kuelekezwa kwenye shughuli za maendeleo.

Tunaitaji Tanzania yenye viongozi wazalendo na wenye uchungu wa kuona nchi yao inabiga hatua za maendeleo. Mh. Dr, John Pombe Magufuli toka achaguliwe kuwa Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameonyesha dhamira ya dhati ya kubadili mwelekeo wa Taifa letu kwa kubana matumizi. Maamuzi mbalimbali aliyoyafanya toka aingie Ikulu ya Tanzania ni yamuelekeo wa kizalendo na yakupigia mfano. Kwa mfano, kusitisha safari za nje, kuelekeza pesa za sherehe za wabunge kwenda kununua vitanda katika hospitali ya muhimbili, yote haya ni maamuzi ya kizalendo. Baadhi ya watanzania wamekua wakipuuza juhudi hizi, kwa mtu mwenye kulipenda taifa lake hana budi kumuunga mkono Rais wetu ili aweze kufanya maamuzi makubwa zaidi kama vile kufumua sheria ya manunuzi ambayo imekua chanzo cha kupoteza mapato makubwa ya serikali na kudhibiti rushwa.


Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Mbariki Rais wetu.
 
Mahakama ya ufisadi ianze na zike billion zilizolipwa makandarasi hewa wizara ya Ujenzi, kivuko feki cha 1978 kwa billion 8 , mabehewa mabovu, wezi wa Escrow, EPA
 

Bunge si mali ya Rais,hapaswi hata kwa sekunde moja kuliingilia. Ule ni Mhimili Huru, kama ilivyo Executive na Judiciary. Bunge ndilo lenye wajibu wa kuisimamia Serikali,ila si Serikali kulisimamia Bunge! Jukumu ulilompa unamwonea tu.
 
Inakuaje mfanya kazi aliyeamua kutumia pikipiki kama usafiri wake wa kumuwahisha kazini aambiwe akate kibari cha kuingia mjini.mfano mimi nina barua inayoonyesha kuwa ni mfanyakazi nimeajiriwa na pikipiki ninayotumia ni kwa ajili ya kuwahi kazini lakini wakamataji hawataki kuelewa .
 
Lipia kwanza hiyo pikipiki yako kodi kama kuna MTU atakusumbua
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…