Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Hao ulio wataja ndio wahusika na waanzilishi wa hayo matatizo huko zanzibar,dawa ni moja tu tanganyika iache kuivamia zanzibar kwa majeshi na vifaru iwape zanzibar mamlaka yao yaliyoporwa mwaka 1964.
 
Hao ulio wataja ndio wahusika na waanzilishi wa hayo matatizo huko zanzibar,dawa ni moja tu tanganyika iache kuivamia zanzibar kwa majeshi na vifaru iwape zanzibar mamlaka yao yaliyoporwa mwaka 1964.

Hivi kitufe cha LIKE kimeondolewa siku hizi? Pata BIG LIKE Mkuu Bobwe2
 
Last edited by a moderator:
Kama ni ishu ya majority basi hafai maana tz watu 45.3m kachaguliwa na 8m hapo majority iko wapi?

Akishakuwa rais si wa chama bali wa watz wote hata yy alisema.Haimanishi kwamba ushauri wa ccm ndo ausikilize.mbona hizo safari mlisema zina faida leo amezkata mnasifia mnatofauti gani na uch..i wa mwanamk akiinama unageuka akikaa unagruka.
 
Mheshimiwa Rais, kwa tabia yetu ilivo ni HERI ukapiga marufuku mradi huu unaoanzishwa wa 'KUIJADILI' hotuba yako uliyoitoa bungeni. Watu wafanye kazi tu badala yake.
 
Magufuli, haya yote unayofanya ni tisa, kumi tunataka kuona waliochota mabilioni ya Escrow kupitia benki ya Stanbic wakikamatwa na kufikishwa mahakamani.

Maazimio ya Bunge teyari yapo,sasa shida iko wapi?

Hela za Escrow tunazihitaji.

Alafu na BOT je?
 
Nadhani mwacheni kwanza ashughulikie yanayoendelea kwanza kisha ndo arejee viporo/past
 
sasa ni wakati muafaka Kwa rais magufuli kulifufua shirika la ndege la la tanzania.ni aibu kwakweli hadi leo tanzania ina kandege kamoja tu ukilinganisha na kenya wenye ndege 50 zinazofanya safari zake karibia dunia nzima
 
Na wa Richmond pia.

wote waliotajwa ama kujidhuru Richmond na Escrow alale nao mbele kwa mbele.
 
Acha afanye kazi kwa alivyopangilia sio wewe unavyompangilia...

Sasa unauliza BOT, ulitaka kote huko atembee ndani ya siku moja tu?? Juzi alikuwa pale, leo wako Bandari kesho au kesho kutwa bila shaka watafika huko unakosema..

Nimekuja kugundua UPINZANI WA TANZANIA ni kutiana ujinga tu na kutafuta sababu za kipuuzi puuzi.. MAGUFULI mimi ni CHADEMA damu damu lakini nime'appreciate speed uliyoanza nayo na nimeonaa nia yako ni kushughulika haswa.. Cha msingi ni kuongeza bidii tu, Hapa lazima tuwape moyo Rais na Waziri Mkuu kwa kazi waliyoianza. Kuwavunja moyo au kuleta majungu hakutasaidia chochote..
 
Hbr zenu uwaungwana,

Sisi huku wilaya ya Nyasa ile habari ya hapa kazi tu haipo kabisa kwanini nasema hivyo sasa yapata miezi mitatu tulijaza fomu za mikopo benki cha kushangaza fomu zote zimekwama kwa mkurugenzi wilaya ya Nyasa.

Tumefuatilia majibu tunayopewa mara ya kwanza tulikuwa tunaambiwa system mbovu sasa tunaambiwa password imepotea hivyo wameshindwa kuingiza makato. Sasa tunakwenda mwezi wa tatu wafanyakazi wote wilaya ya Nyasa hatuelewi nini hatima ya maisha yetu na ndiyo maana nikasema hapa kazi tu Nyasa haipo.
 
Kamati ya Rais ya Kusimamia mashirika ya Umma (SCOPO) ambayo majukumu yake yalikuwa ni pamoja na kuchunguza na kuidhinisha miundo ya mashirika na miundo ya utumishi, kuchunguza na kuidhinisha mishahara na marupurupu ya wafanyakazi wa mashirika ya umma baada ya kupata idhini ya Msajili wa Hazina.

Katika miaka ya 1990, mashirika mengi ya umma yalikuwa yakiendeshwa kwa hasara na hivyo kutegemea ruzuku kutoka Serikalini. Kufuatia hali hiyo, mwaka 1992 Serikali ilitunga Sheria ya Mashirika ya Umma kwa lengo la kuyapa uhuru zaidi kwa kuamua, kupanga na kuendesha shughuli zao kwa misingi ya kibiashara, hususan katika mazingira mapya ya ushindani na ulegezaji wa masharti ya biashara. Katika mwaka 2002 Sheria ya Msajili wa Hazina ?The Treasury Registrar (Powers and Functions Act Cap. 370)? ilirekebishwa kutokana na mabadiliko katika mfumo wa usimamizi na uendeshaji wa Mashirika ya Umma. Tarehe 31 Disemba, 1992 Serikali ilivunja iliyokuwa SCOPO ambapo baadhi ya shughuli zake zilihamishiwa Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Lakini kwa sasa inaonekana ipo haja ya kuirudisha scopo kutokana na mashirika mengi kuendeshwa kifisadi ikiwemo kujipangia mishahara minono na marupurupu yasiyoendana na kazi wanazozifanya.

Scopo mpya ihusishe pia makampuni ya kigeni ambayo yamekuwa yakilipa wafanyakazi wa kigeni mishahara minono ukilinganisha na ya watanzania wenye sifa zilezile huku yakiwa hayako tayari kulipa kodi kwa kisingizio yanapata hasara na yakilazimishwa yanafunga biashara na kuhamia nchi nyingine.
 
Ngoja tumalize huku kwanza then tunakuja huko halmashauri/ wilaya zote
 
Hicho kisije kuwa kitengo cha watu flani flani
kupiga ganji ya pembeni.
 
Nimesikiliza hii hali ya upotevu wa makontena zaidi ya mia 3 na ukwepaji wa kodi uliofanywa bandarini. Hii ni baada ya hotuba ya Rais ambayo alionyesha msimamo wake na maeneo yaliyokithili kwa rushwa na ufisadi.

Ukiangalia madaraka ya Rais ni makubwa sana, watu wote tulistahili kuogopa kujihusisha na ufisadi wa kiwango hiki wakati huu ambao wengi hawajaelewa muelekeo wa serikali, lakini nafasi ya Rais imeshuka kiwango ambacho sasa waliokwisha nufaika na udhaifu uliopita hawaamini kwamba Rais ana nguvu za kutosha kuwapoteza kabisa ktk biashara zao.

Nahisi ndiyo maana bado wanafanya haya yote tena kwa kushirikiana na wateule wa Rais.

Naomba sasa Rais aachane na mtindo wa kuwasimamisha kazi. Weka watu gerezani kwa makosa ya kipuuzi kiwango hiki ili wakutane na kesi wakiwa ndani.
 
Mlianza kwa kusema Rais Magufuli hawezi kufanya lolote kwa sababu ni wale wale, kwa sasa mmeanza tena kumpangia afanye nini baada ya kuzijibu hoja zenu ndani ya wiki mbili ambazo zilikuwa hazina mantiki kutokana na historia ya utendaji wake.

Kaeni pembeni muangalia movie za Rais Magufuli akifanya kile wapiga kura wengi walimtaka, hata Roma haikujengwa kwa siku moja!
 
Waliosimamishwa leo;
1. Wanaisaidia polisi(maana yake watabanwa na polisi hadi kusema ukweli).
2. Hati zao za kusafiria zimechukuliwa.
3. Mali zao zinachunguzwa uhalali wake
Hata hivyo, pesa zilizopotea zitafutwe na kurejeshwa serikalini..
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…