Kamati ya Rais ya Kusimamia mashirika ya Umma (SCOPO) ambayo majukumu yake yalikuwa ni pamoja na kuchunguza na kuidhinisha miundo ya mashirika na miundo ya utumishi, kuchunguza na kuidhinisha mishahara na marupurupu ya wafanyakazi wa mashirika ya umma baada ya kupata idhini ya Msajili wa Hazina.
Katika miaka ya 1990, mashirika mengi ya umma yalikuwa yakiendeshwa kwa hasara na hivyo kutegemea ruzuku kutoka Serikalini. Kufuatia hali hiyo, mwaka 1992 Serikali ilitunga Sheria ya Mashirika ya Umma kwa lengo la kuyapa uhuru zaidi kwa kuamua, kupanga na kuendesha shughuli zao kwa misingi ya kibiashara, hususan katika mazingira mapya ya ushindani na ulegezaji wa masharti ya biashara. Katika mwaka 2002 Sheria ya Msajili wa Hazina ?The Treasury Registrar (Powers and Functions Act Cap. 370)? ilirekebishwa kutokana na mabadiliko katika mfumo wa usimamizi na uendeshaji wa Mashirika ya Umma. Tarehe 31 Disemba, 1992 Serikali ilivunja iliyokuwa SCOPO ambapo baadhi ya shughuli zake zilihamishiwa Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Lakini kwa sasa inaonekana ipo haja ya kuirudisha scopo kutokana na mashirika mengi kuendeshwa kifisadi ikiwemo kujipangia mishahara minono na marupurupu yasiyoendana na kazi wanazozifanya.
Scopo mpya ihusishe pia makampuni ya kigeni ambayo yamekuwa yakilipa wafanyakazi wa kigeni mishahara minono ukilinganisha na ya watanzania wenye sifa zilezile huku yakiwa hayako tayari kulipa kodi kwa kisingizio yanapata hasara na yakilazimishwa yanafunga biashara na kuhamia nchi nyingine.