Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Ajaribu kukaa na wabunge wa chama chake awape neno juu ya uzalendo na kujadili mambo yenye tija c kukubali kila ktu kletacho na serikali.
kupunguza urasimu ktk bandari, na utalii ili kuweza kufanksha lengo la HAPA KAZ Tu.
 
Ingekuwa jambo la busara ungemuomba apige chini malipo kwa Dola (fedha ya kigeni) hapa tz hii inachangia kuipoteza shilingi balaa!
 
kijana katupwa nje na ESCROOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO.
rais akiwakamata mafisadi wote nje na ndani ya chama bila kujali ana wadhifa gani au alikuwa nani nitamfananisha na Malaika,maana hakuna tembo awezaye kuvunja mkonga wake.
 
aje Dodoma awasaidie hawa wanaoomba barabarani hata kwa kuwafungulia kituo tuu au kuwa anawapa pension ya kila mwezi coz naona wananchi wameanza kuwanyanyasa kwa kigezo si wamemchagua wakaombe pesa chichiemu
 
Rais wetu habari yako, ombi langu ni moja

Kuna tabia imeanza kukithiri na kushika kasi malipo mengi kufanyika kwa dola hapa nchini kuna baadhi ya huduma haziruhusu malipo kwa shilingi.

Mfano kwenye malipo ya mapango ya biashara na
baadhi ya shule (private schools) na mahoteli ya nafanyika kwa dola naamini matumizi ya fedha za kigeni hasa dola kwenye huduma nyingi za ndani yanachangia kudidimiza thamani ya shilingi na uchumi wetu kwa ujumla.

Tafadhali kemea hili jambo walau shilingi yetu ijinafasi
 
Itakuwa vizuri sana ila mleta mada huenda hujui pia causes za thamani ya fedha kupungua,
 
Ni wazo zuri sana...badala ya kununua gari V8 ya milioni 280, bora wachukue rav 4 mpya ya ml 60...na hizo savings/cost-cutting haziishii kwenye manunuzi tu...automatically, inapunguza na gharama nyingine mfano spare za rav 4 ni chini zaidi ya spare za v8...utumiaji wa mafuta wa rav 4 uko chini zaidi ya v8 and so on and so forth.
 
aje Dodoma awasaidie hawa wanaoomba barabarani hata kwa kuwafungulia kituo tuu au kuwa anawapa pension ya kila mwezi coz naona wananchi wameanza kuwanyanyasa kwa kigezo si wamemchagua wakaombe pesa chichiemu

Hahaaa zile milioni 50 zitawasaidia
 
Secta ya bunge kitengo cha huduma na haki za mbunge kilichokuwa chini ya Chenge kilipangia bunge masulufu makubwa mno na bado wabunge kwa makusudi au kwa utovu wa adabu walikuwa wanaona haziwatoshi.

Mfano posho za kuhudhuria bunge ni shs 300.000 bado wabunge walikuwa wanaona hazitoshi ziongezwe chini ya Chenge

Mh. Rais kubana matumizi ya serikali iangalie sana secta hii ya bunge

Pia ninakuomba usitishe mikopo ya mashangingi, waheshimiwa wabunge wanunue RAV 4 au NOA kwa hela zao kwa sababu majimbo yamegawanywa na kuwa madogo yanayoweza kufikika kilaisi na usafiri huo.

Mh Rais fanya kazi ya ubunge iwe ngumu lli uchaguzi ujao wanachi wasiikimbilie

Ushauri huu pia nimekutumia kwa e.mail tafadhari naomba unijibu kama kutakuwa na ugumu katika utekelezaji wake

KIFUPI: Bunge linamega sehemu kubwa sana ya keki ya Taifa, serikali ya awamu ya tano liipunguze keki hiyo.
 
maeneo mengi hapa nchini hasa hotel wanakataa malipo kwa kutumia shilingi na wengi wao ndio wale waliochangia kampeni za chama naamini jp hana uwezo wa kukatataza hili, ukizingatia yeye mwenyewe amebebwa hadi hapo alipofika!
 
Nzuri hiyo sasa tunatakiwa kufanya kazi...hata kutoa ushauri ni sehemu ya kazi
 
eti wengine wanaita pesa ya madafu badala ya kujenga uchumi,mimi namfagilia sana Rais Mkapa.
 
Upinzani gani? Mbona agenda us ufisadi ilizikwa rasmi na Ukawa baada ya kumpokea fisadi mkuu na kumsafisha kwa jiki lakini bahati mbaya haikuwa kali sana. Sina uhakika kama ili expire au vipi. Hakuna mpinzani yeyote atakayesema kuhusu Ufisadi akaeleweka kilichobaki ni Unafiki na kutafuta ulaji
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom