Wakuu!
Tumeshuhudia Wizara hii katika awamu zote za awamu ya Tatu na nne ikiwa ndio Wizara iliyoitangaza sana nchi katika kashfa mbali mbali za ufisadi mkubwa uliozifanya hadi nchi wahisani kuwa na shaka na uendeshaji wa nchi na hasa udhibiti wa mapato ya ndani ya Taifa.
Kwa kuwa Magufuli amejitanabaisha kuwa ni Mtu wa kazi, Muadilifu basi ili kuliondolea taifa na udhia wa kuingia kwenye kashfa kubwa kubwa za Ufisadi ni vema Wizara hii ikawa chini ya Ofisi ya Rais ili tushuhudie ufanisi uliotukuka kwa kufaidi rasilimali zetu kama vile Gesi, Madini mbali mbali na mafuta pale yatakapo anza kuchimbwa.
Kwani kwa hali ya sasa hakuna Waziri yeyote atakaye kabidhiwa Wizara hiyo ambaye ataweza kumaliza salama kwani ni wazi Wizara hiyo ndio kimbilio la CCM kujipatia fedha kiujanja ujanja hivyo Wizara hiyo ikidhibitiwa kikamilifu CCM watajipanga vema kutumia vyanzo vyao vya fedha vya halali na hivyo nchi kuendelea vema na kuondokana na mgao wa umeme usio na mwisho kila mwaka.
Nadhani kule Nigeria, Waziri wa,Fedha ni Rais Mwenyewe ingawa siyo directly, ni pia wazo langu Wizara ya Fedha ikawa chini ya Ofisi ya Rais!