Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Mzinifu hupata wazinifu wenzie ... Kwani yeye anauadilifu upi? Anajua amewekwa madarakani kwa style ya wizi wa kura ...
Sio siri kuwa CCM ni chama kilicholea na kuhifadhi ufisadi nchini.

Kupata mtu mwadilifu ndani ya CCM ni sawa na kocha kutafuta wachezaji wa kusajili MOI.

Chama kilihangaika kumpata mgombea urais mwadilifu kikakosa kikabidi kumpata mwenye nafuu kidogo,na kumnadi kwa pesa nyingi za kukufuru, na kufanikuwa kumchagulusha.

Sasa tujiulize huyo waziri mkuu na mawaziri wasio na kashfa ndani ya chama chetu watapatikanaje?

Nimesikia majina yanatajwatajwa lakini yote yana madoa ya ufisadi. Subiri wateuliwe uone jinsi watu watakavyoanza kuweka hadharani madudu yao.
 
Mi nadhani mtulie tu kampeini zimekwisha pengine msubili 2020.
 
Anne Kilango tena...yani katika watu wote umeona huyo mama anafaa? Namshauri raisi atumie nafasi zake 10 kuteua watu makini kumsaidia, Kilango sio mmoja wao.
 
Atamchagua Lema ili amtumie kwa ziara za kushtukiza za kulala magerezani
 
Chini ya CCM watanzania wameteseka na kunyanyasika sana ila nashangaa watanzania hawa bado tu wanawapa kura zao.

Mkosamali,popote ulipo, maneno yako Bungeni kuhusu watanzania nitayakumbuka daima.
 
Anne Kilango tena...yani katika watu wote umeona huyo mama anafaa? Namshauri raisi atumie nafasi zake 10 kuteua watu makini kumsaidia, Kilango sio mmoja wao.
Nitashangaa sana huyu anayetajwa na vijana wa bavicha kama Dr mihogo asipokuwemo, labda akatae mwenyewe.
 
aisee magufuli amechukua nchi ikiwa na matatizo mengi sana,
kikubwa wanachi wote tumuunge mkono ktk harakati zake na tumuombee kwa Mola amjaalie atimize ahadi,, tumpe muda Dk JPM atimize kauli mbiu ya "Hapa Kazi Tu!"
 
Unadhani wote tungekuwa na akili za kuipigia makofi CCM kama nyinyi huyo Magufui angeakuwa na hii kasi?

Unadhani bila Magufuli kuzomewa kwenye kampeni angeshutuka?

Jiulize mbona alipokuwa waziri hii kasi ya leo haikuwepo?

Jiuluze kama upinzani ungekuwa na nguvu uliyonayo leo hii Magufuli na wenzake serikalini wangejimilikisha nyumba za serikali?

Unadhani Magufuli angebadilika kama wote tungeimba CCM?

Kwa akili zenu hata kama CCM ingempitisha mtu tofauti na Magufuli mmengacha kuipa kura?

Hata kama Ukawa ingemsimsmisha mtu tofauti na Lowassa wewe ungeipa kura ukawa?

Acheni ujinga wenu na hata huyu Magufuli bado tunaendelea kumuangali na akibadilika na sisi tunambadilikia ingawa nyinyi naamini hata akija kuzembea mtaendelea tu kumpigia makofi kisa katoka CCM.

We unashangaza sana!

Siku hizi huyu Mzee Mwanakijiji sielewi uwezo wake umeenda wapi?
 
Last edited by a moderator:
Sawa...
Lakini kwa upande mwingine tunaangalia waziri au viongozi kwa ujumla wawe mfano kwa walio chini yao.
Wawe mfano katika kuchapa kazi lakini pia katika kubana matumizi ya fedha za umma.
Naamini kabisa sio mawaziri peke yao wana kazi nyingi, wapo watendaji wengi chini yao na pengine wengi wana kazi nyingi kuliko mawaziri.
Na naamini pia waziri mchapa kazi anaweza kuwa productive vya kutosha akiutumia mda wake akiwa ofisini vyema.
Lakini kama ni suala la kuutumia mda wa safari basi sio vibaya waziri akaonyesha mfano wa uzalendo kwa kuajiri dereva wake kama ulivyoajiri wewe...

Tuko pamoja kwenye hilo.
 
Hii ni mbaya kama nina bifu na boss si namlipua tu
Magufuli anajua wizi wote.
Bandari stay tuned..

Hiyo njia itafanya wachapakazi wote ndo wapigwe chini.Siku zote wafanyakazi wa umma Tanzania hawapendi kazi wanaenda kazini na kutoka muda wanaotaka.Ikitokea boss akawa anawakaba basi anachukiwa balaa.Sasa kama boss wafanyakazi hawampendi halafu unawapa njia hiyo atapona?Isije kuwa kama enzi zile watu waliambiwa wapige kura wauwaji wa albino na vikongwe mtu anaenda kumpigia mtu kura kwa kuwa ana bifu naye.Serikalini kuna mfumo mzuri tu wa inteligensia na wanajua kila kitu usione wako kimya.
 
Rais wangu Dr. John, pombe Joseph Magufuri, muziki wako unaelekea kukolea naona gita la rizimu limetulia ongeza gita la solo ili muziki ukolee vizuri, tunaomba ubadirishe wafanyakazi kwenye BWAWA la pesa pale WIZARA YA FEDHA na idara zake ukianza na TRA NA HAZINA. Hili ndilo gitaa linalotengeneza muziki, pia kata safisha mitambo chakavu yote ya kurekodia kwani muziki haufiki vizuri kwa walengwa, kuna studio ndogo ndogo hapo kati kati nazo zinaongonzwa na baadhi ya watendaji wakubwa tena wengine ni wakubwa km mibuyu kuyakata unahitaji cheso mpya. mfano kuna mIbuyu pale TRA, BANDARI, DAWASCO, TANESCO, USALAMA WA TAIFA, POLISI NA NK.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom