Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Mheshimiwa rais tunakuomba utuletee mahakama hii ni muhimu sana iwepo. Naomba uanze na wale walio fisadi taifa wakiwa viongozi na badaye kusema baada ya kutoka madarakani kuwa hakuna walichokuwa wakikifanya bali kutuibia na kulipwa mishahara bure. Hawa ni wahujumu uchumi no.1 ni vema washitakiwe bila huruma.
 
Tatizo ni mtangulizi wake kaacha virusi kila kona hasa vya madawa ya kulevya ningekuwa masolex ningeshughulikia huo mtandao kwanza
 
kwa namna kazi zilivyo nyingi na ngumu ni kama nchi hii haikuwa na uongozi wa juu wa nchi kwa muda mrefu.
 
Dr. Mahiga ameiwakilisha Tanzania kwa weledi na uzalendo wa hali ya juu. Anauwezo wa kusaidia Taifa kwenye wizara ya mambo ya nje. Mh. Rais taifa litafaidika vya kutosha chini ya Dr. Mahiga.
 
Dr. Mahiga ameiwakilisha Tanzania kwa weledi na uzalendo wa hali ya juu. Anauwezo wa kusaidia Taifa kwenye wizara ya mambo ya nje. Mh. Rais taifa litafaidika vya kutosha chini ya Dr. Mahiga.

sikuhizi hawa madiaspora tumeshaanza kuwastukia, prof.tibaijuka katupiga hela na matusi juu, dr.balali nae katukomba hazina. prof.muhongo vilevile katupiga na kebehi juu. Mzee wa vijisenti anatumia utaalamu wa havard kutulengesha. hebu tukomae na hawa hawa jamaa zetu wa kibongo kwanza.

Ila kuna ka hali Fulani sijui kama atakuwa amekaacha, kule Somalia alishutumiwa unywaji wa pombe na kushika makalio wa dada, na inasemekana ndo sababu ya kutimuliwa Somalia. Kuna party moja alionekana akicheza mziki katika hali ya kuzidiwa na kinywaji na alicheza huku kamshika kiuno mdada wa kizungu.

Hili jembe linajitosheleza tumpe tu vijana wa kufanyanao kazi.
 
Kama kuna sheria ama kanuni mbaya zenye kuendekeza ubinafsi na kujipendelea kwa wabunge wetu na kwa upande mwingine kuwapendelea ndugu, rafiki, jamaa na hata nyumba ndogo zao ni sheria ya viti maalum kwa wanawake na pili, sheria ya wabunge kulipana posho za vikao.

Chukulia ni fedha kiasi gani inatumika kuwagharamia wabunge 121 ambao hawakutokana na kura ya moja kwa moja na mwananchi ambaye tunaamini ndiye bunge hili liko kwa ajili yake.

Jenga hisia pia kwamba kuna vijana wa kike wa umri wa miaka 24 ambaye hajawahi kukifanyia lolote chama anateuliwa kuwa mbunge wa viti maalum kwa sababu tu ni ndugu wa m/kiti wa chama wa mkoa au kwa sababu tu ni hawala wa kiongozi fulani wa juu wa Chama, wakati huo huo wanaachwa akina mama wenye sifa waliovipigania, kuvitetea na kuvijenga vyama miaka na miaka.

Malalamiko ya wanachama wa vyama vya CCM na CDM baada ya uteuzi wa wabunge wanawake wa viti maalum, umedhihirisha kuwepo kwa upendeleo ama kukosekana kwa utaratibu maalum wa vyama kuwapata wabunge hao.

La pili, ninalomwomba mhe Rais alifute wakati wa utawala wake ni ulipanaji wa posho za vikao wanazolipana kila siku wanapokaa kwenye vikao vyao vya bunge wakati wanalipwa mshahara kutokana na hilo.

Ni gharama sana kuwalipa wabunge zaidi ya 390 posho ya sh. 300,000 kila siku na bado wakimaliza miaka mitano unawaaga na kiinua mgongo cha sh 230,000,000 kila mmoja. Huu kama zi ufisadi wa wazi ni nini?
 
Rais kazi yake kufuta sheria ndio maana tunachagua wabunge aina ya kibajaji hatujui kazi za mbunge ni nini na kazi ya Rais ni nini.
 
Hilo lazima liende sambamba na uandaaji wa mswada wa sheria itakayoweza kuwezesha hivyo vitu kufutika, muombe Rais awe na utashi huo wa kisiasa, kwa hakika utakuwa nim utashi mzuri sana
 
Rais kazi yake kufuta sheria ndio maana tunachagua wabunge aina ya kibajaji hatujui kazi za mbunge ni nini na kazi ya Rais ni nini.

Mara nyingi ktk bunge letu miswada mingi hupelekwa na serikali baada ya kuandaliwa na kujadiliwa na baraza la mawaziri chini ya uwenyekiti wa Rais.
 
Kama ungepata nafasi ya kushauri serikali ya awamu ya5. Katika eneo la 1.Kuinua kipato cha wananchi
2.Elimu
3.Ajira
4.Afya
5.Usafiri
6.Michezo
7.Kilimo
8.Rasilimali (Dhahabu, Almasi gesi n.k)
9.Ulinzi na Usalama.
Au lolote ambalo unadhani litasababisha kututoa Tanzania na wananchi wake wote kwa ujumla kuwa na maisha mazuri afya na kipato bora. ungeishairi nini?

TAFADHALI TANGULIZA UZALENDO MBELE
-----------------------------------------------
NATAMANI KUONA MABADILIKO YA KWELI KWA RAIA WOTE WA TANZANI. MASHARIKI MPAKA MAGHARIBI, KUSINI HADI KASKAZINI.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Mara nyingi ktk bunge letu miswada mingi hupelekwa na serikali baada ya kuandaliwa na kujadiliwa na baraza la mawaziri chini ya uwenyekiti wa Rais.
naona hujamuelewa Ngongo
Rais kazi yake si kufuta Sheria za Bunge na wala kuwaingilia (lipo katika Mihimili mitatu)
na akifanya Mchezo Wabunge wanaweza kumfuta yeye kwa kutokuwa na Imani naye na Uchaguzi ukarudiwa tena ndani ya muda wake wa utawala.
kweli viongozi wengi wa vyama wanaweka vipozeo vyao kwenye viti maalum, huwezi kulaum chama kimoja kwani hata Bunge la Katiba kuna Mkiti alienda na Mkewe
 
Dhibiti mianya ya Rushwa na Imarisha shilingi. Tupate hela za kujenga viwanda vidogovidogo kama vya kukamua juice, matunda ya wakulima yasiharibike. Ajira zitakuja.
 
Ningeshauri aboreshe huduma za maji na umeme. Tanzania tuna vyanzo vya maji lukuki kuliko hata Afrika kusini. Haya maji ya madumu, wananchi wanunue maji ili kupika suala hili linaongeza ukali wa maisha
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom