Wanaukumbi.
Viwanda hivyo vilianzishwa karibu mikoa mingi ya Tanzania Bara kama vile vya kuchambua pamba na kuzalisha bidhaa zitokanazo na pamba na katani.-Viwanda vingine ni vile vya korosho na kahama na kile cha chuma kilichokuwa mkoani Kilimanjaro.
Ingawa viwanda vingi kati ya hivyo havifanyi kazi kwa sasa lakini maono ya mwalimu yalikuwa mazuri kwani alilenga kumkomboa mkulima kwa kuhakikisha malighafi anayozalisha inanunuliwa kwa bei nzuri na viwanda hivyo na kisha kutumika kuongeza samani kwa kuzalisha bidhaa aina mbalimbali.
Tanzania ya Nyerere ilikuwa na viwanda vya ku-assemble malori ya Scania na matrekta ya Valmet huko Kibaha na kiwanda hicho kwa sasa kingekuwa na umuhimu sana katika mpango wa KILIMO KWANZA.
Baadhi ya viwanda vilivyoasisiwa na mwalimu ni pamoja na General Tyre, NDC-STAMICO, shirika la reli na mahoteli yakeATC,NMC,NASACO,THB,POSTA NA SIMU,KILTEX,NAFCO,TPH, Sungura textile, Mang'ula,--Machine tools, Chakula barafu, Elimu supply, Mtava, Tanganyika Packers,- Narco, Dafco, TPC, TPDC, Bush treaker hotels, Kamata ,NMC, RTC, Tanesco,- Meco, Tameco, Mwatex , Kibaha Cashewnut Factory na vingine vyote vya korosho, Hotel kama Embassy, Agip, Kauma,Bora, Ufi, Iringa retco-mbeya retco, RTC, Pamba injinia na Tanita, Sigara na Uda.
Mashirika, mashamba, mabenki na vyanzo vya uchumi aliyoacha na au kutaifisha Nyerere havikuendelea/ havitoendelea kwa sababu tu, havikuwa, havina waendeshaji wenye kina cha muono wa kibiashara, kiviwanda, kijamii bunifu.-Ingawa viwanda vingine vilibinafsishwa kuanzia awamu ya pili ya Alhaji Hassan Mwingi na awamu ya tatu ya Benjamin Mkapa, lakini hadi leo havifanyi kazi na vile vilivyohai vinafanya shughuli zingine na si uzalishaji uliokuwa umelengwa.Vingine vimegeuzwa maghala ya kuhifadhia bidhaa.-Tanzania iliwahi kuwa na viwanda vingi na vya namna mbalimbali ambavyo lengo lake kubwa lilikuwa ni kutengeneza uwezo wa ndani wa taifa kuzalisha bidhaa mbalimbali ili kutosheleza kwa kiasi kikubwa mahitaji ya ndani ya nchi.-Lakini, kubwa zaidi katika mawazo ya Mwalimu na waasisi wa taifa letu lengo lilikuwa ni kutengeneza kile ambacho tunakiita "nguvukazi" (manpower) ya ndani ili kuchukua nafasi mbalimbali zilizokuwa zinashikiliwa na wageni.
Katika kufanya hili miaka ya mwanzo tukajitahidi sana kuwapa nafasi watanzania kushika nafasi mbalimbali za uongozi katika makampuni na mashirika mbalimbali yale ambayo tuliyajua kuwa ni "mashirika ya umma".-Hata baada ya yale yaliyoitwa mabadiliko ya uchumi bado viwanda vingi vilikufa au kudumazwa wakati kinadharia na kihalisia kumekuwa na ongezeko kubwa la watanzania wenye ujuzi na uzoefu kuliko wale walioanza baada ya Uhuru.-Ni kwa namna gani katika uchumi huu mpya bado tunaweza kufufua baadhi ya viwanda hivyo na kutafuta namna mpya ya umiliki wa viwanda vya umma kama kwa kutumia mtindo wa hisa za mojwa kwa moja kwa wananchi na taasisi binafsi za wananchi.-Serikali inaweza vipi kutengeneza mazingira yanayoweza kuboresha uendeshaji wa viwanda hivi aidha kwa mtindo wa private-public patnership au mtindo wowote ambao utahakikisha wamiliki wanapata faida, kizalishwacho ni cha ubora wa kisasa na vile vile ni endelevu.