Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Sio fitina .Ni jinsi ya kuona Kama raisi anaweza kusaidia wakulima kupata soko bila kupata hasara.Nafikiri si lazima Magufuli,hata waziri wa viwanda akisha chaguliwa anaweza kuweka mazingira mazuri kwa kuongea vizuri na mwenye kiwanda.Mbona Bhakressa mtu Powa Sana ?Utakuta usumbufu ni hawa waajiriwa tena wakiwa Wahindi ndo wasumbufu na dharau na kupenda kulalia wauzaji wakitafuta Sifa kwa Bhakressa.

Mkuu upo vema sana umeelewa nini kimeongelewa
 
Toka Suala La Ving'amuzi Limeingia Nchini Watanzania Wengi Wameshindwa Kulipia Gharama Ili Kupata Hata Chaneli Zetu Za Ndani.

Hivyo Ninakushauri Mh.Rais Kutoa Agizo Kwny Kila Kampuni Za Ving'amuzi Kuonyesha Bure Chaneli Zote Za Hapa Nchini Ili Kutoa Fursa Kwa Watanzania Kupata Habari Na Taarifa Za Nchi Yao Kwa Uhuru.

Watu Wengi Wameshindwa Kulipia Na Kufanya Idadi Ya Watu Wasioweza Kupata Habari Kuongeza Hata Mijini.

Atakaetaka Chaneli Zingne Zote,basi Atalipia.
 
Wanaukumbi.


Viwanda hivyo vilianzishwa karibu mikoa mingi ya Tanzania Bara kama vile vya kuchambua pamba na kuzalisha bidhaa zitokanazo na pamba na katani.-Viwanda vingine ni vile vya korosho na kahama na kile cha chuma kilichokuwa mkoani Kilimanjaro.

Ingawa viwanda vingi kati ya hivyo havifanyi kazi kwa sasa lakini maono ya mwalimu yalikuwa mazuri kwani alilenga kumkomboa mkulima kwa kuhakikisha malighafi anayozalisha inanunuliwa kwa bei nzuri na viwanda hivyo na kisha kutumika kuongeza samani kwa kuzalisha bidhaa aina mbalimbali.

Tanzania ya Nyerere ilikuwa na viwanda vya ku-assemble malori ya Scania na matrekta ya Valmet huko Kibaha na kiwanda hicho kwa sasa kingekuwa na umuhimu sana katika mpango wa KILIMO KWANZA.

Baadhi ya viwanda vilivyoasisiwa na mwalimu ni pamoja na General Tyre, NDC-STAMICO, shirika la reli na mahoteli yakeATC,NMC,NASACO,THB,POSTA NA SIMU,KILTEX,NAFCO,TPH, Sungura textile, Mang'ula,--Machine tools, Chakula barafu, Elimu supply, Mtava, Tanganyika Packers,- Narco, Dafco, TPC, TPDC, Bush treaker hotels, Kamata ,NMC, RTC, Tanesco,- Meco, Tameco, Mwatex , Kibaha Cashewnut Factory na vingine vyote vya korosho, Hotel kama Embassy, Agip, Kauma,Bora, Ufi, Iringa retco-mbeya retco, RTC, Pamba injinia na Tanita, Sigara na Uda.

Mashirika, mashamba, mabenki na vyanzo vya uchumi aliyoacha na au kutaifisha Nyerere havikuendelea/ havitoendelea kwa sababu tu, havikuwa, havina waendeshaji wenye kina cha muono wa kibiashara, kiviwanda, kijamii bunifu.-Ingawa viwanda vingine vilibinafsishwa kuanzia awamu ya pili ya Alhaji Hassan Mwingi na awamu ya tatu ya Benjamin Mkapa, lakini hadi leo havifanyi kazi na vile vilivyohai vinafanya shughuli zingine na si uzalishaji uliokuwa umelengwa.Vingine vimegeuzwa maghala ya kuhifadhia bidhaa.-Tanzania iliwahi kuwa na viwanda vingi na vya namna mbalimbali ambavyo lengo lake kubwa lilikuwa ni kutengeneza uwezo wa ndani wa taifa kuzalisha bidhaa mbalimbali ili kutosheleza kwa kiasi kikubwa mahitaji ya ndani ya nchi.-Lakini, kubwa zaidi katika mawazo ya Mwalimu na waasisi wa taifa letu lengo lilikuwa ni kutengeneza kile ambacho tunakiita "nguvukazi" (manpower) ya ndani ili kuchukua nafasi mbalimbali zilizokuwa zinashikiliwa na wageni.

Katika kufanya hili miaka ya mwanzo tukajitahidi sana kuwapa nafasi watanzania kushika nafasi mbalimbali za uongozi katika makampuni na mashirika mbalimbali yale ambayo tuliyajua kuwa ni "mashirika ya umma".-Hata baada ya yale yaliyoitwa mabadiliko ya uchumi bado viwanda vingi vilikufa au kudumazwa wakati kinadharia na kihalisia kumekuwa na ongezeko kubwa la watanzania wenye ujuzi na uzoefu kuliko wale walioanza baada ya Uhuru.-Ni kwa namna gani katika uchumi huu mpya bado tunaweza kufufua baadhi ya viwanda hivyo na kutafuta namna mpya ya umiliki wa viwanda vya umma kama kwa kutumia mtindo wa hisa za mojwa kwa moja kwa wananchi na taasisi binafsi za wananchi.-Serikali inaweza vipi kutengeneza mazingira yanayoweza kuboresha uendeshaji wa viwanda hivi aidha kwa mtindo wa private-public patnership au mtindo wowote ambao utahakikisha wamiliki wanapata faida, kizalishwacho ni cha ubora wa kisasa na vile vile ni endelevu.
 
Utakujaje na Lori la matunda bila kutafuta soko? Hilo swala pia linahitaji sarakasi za magufuli?
 
Mkuu Mmawia kilio chako kwa rais hakitapotea bure, kimesikika, jibu utalipata soon. Rais kasema nchi yetu ni tajiri, matunda yanayowaozeeni ndiyo utajiri wenyewe na kwa mkakati wake wa kuweka viwanda vya uzalishaji vinavyotumia mali ghafi inayopatikana hapa nchini ni wazi KILIO CHAKO kinathibitisha kuwa kuna fursa kubwa ya uwekezaji kwenye eneo hilo la usindikajia matunda. Muda si mrefu mtacheka na kukubali nchi yetu hakika ni tajiri. Viwanda vinakuja kwa fujo hadi AZAM wataanza fiitina.
 
Hivi nyerere aliwezaje kujenga viwanda vyote hivyo,?
Hela alipata Wapi?
Vingapi vinafanya kazi?
 
Wakimaliza hilo serikali itabidi itoe elekezi za bei za vyakula kwenye migahawa
 
Kama Nyumba haina ubora tafuta yenye ubora mnaongea ujinga tu mnajua gharama za Ujenzi ?
 
Ktk eneo ambalo naona Magufuli akienda kufeli ni hili la viwanda. Inabidi atumie wataalamu kweli kweli, na siyo kufanya mambo kwa pupa au kisiasa.

Wazo la kuchukua hayo mashamba na viwanda toka kwa walioshindwa kutimiza masharti yake ni zuri na naliunga mkono asilimia mia.

Ila baada ya kuvichukua, what next? hapa ndo mawazo ya wataalamu yanahitajika sana. Kwa vyo vyote itakavyokuwa sitasapoti wazo la eti serikali ndo iviendeshe. Lengo iwe kutafuta mwekezaji mpya na si serikali kufanya biashara
 
Tunajiaminisha kwa matumaini yasiyokuwepo. Baadhi ya hivyo viwanda vilivyouzwa havipo tena au teknolojia ya wakati huo imepitwa na wakati...ni nafuu kujenga viwanda vipya kuliko kuvifufua hivyo! Kumbuka tuko katika mfumo tofauti wa kisiasa; serikali si mtendaji wa biashara. Sasa sijui mnataka huyo mwenye mali yake aliyoinunua kihalali na pengine kashindwa kuiendeleza afanyeje. Basi tukimaliza hayo ya viwanda turudi kwenye nyumba pia waliozibadilisha kinyume na mikataba wazirejeshe serikalini! Itaisha kutafutana uchawi. We shuold soldier on and build new industries with appropriate today's technology
 
hapa jambo la msingi itungwe sheria ili malipo ya kodi za nyumba zifanyike on monthly basis
 
huwa naenda mkulanga mara kwa mara,sijawahi kukuta gari lenye matunda lililokaa nje siku tatu.acha uongo mkuu
 
Hilo ni soko huria bei inaratibiwa na uhitaji na Upatikanaji yaani (Demand and Supply)..
swala la kodi bado litarndelea kumuumiza mpangaji.. kwa sababu wataweka kodi ya Nyumba ambayo tayari iko compansated na hiyo kodi ya mapato..

Nini kifanyike!
Yaanzishwe makazi mapya ya kutosha ili uhitaji wa nyumba uendane na upatikanaji wake..
Kuboresha miundombinu mfano..
Mtu atoke kibamba na afike Posta kwa wakati.

Wasalaam!

Hakuna kitu kama hicho. Soko huria na holela ni vitu viwili tofauti kabisa. Pamoja na gharama za ujenzi lakini madalali wamekua washenzi sana. Wanaweka bei za hovyo kabisa. Kimsingi hawafai!
 
Tunajiaminisha kwa matumaini yasiyokuwepo. Baadhi ya hivyo viwanda vilivyouzwa havipo tena au teknolojia ya wakati huo imepitwa na wakati...ni nafuu kujenga viwanda vipya kuliko kuvifufua hivyo! Kumbuka tuko katika mfumo tofauti wa kisiasa; serikali si mtendaji wa biashara. Sasa sijui mnataka huyo mwenye mali yake aliyoinunua kihalali na pengine kashindwa kuiendeleza afanyeje. Basi tukimaliza hayo ya viwanda turudi kwenye nyumba pia waliozibadilisha kinyume na mikataba wazirejeshe serikalini! Itaisha kutafutana uchawi. We shuold soldier on and build new industries with appropriate today's technology
Sijui kama unajua moja ya masharti ya kuuziwa kiwanda au shamba kutoka serikalini ni kuliendeleza bila kubadilisha matumizi.

Kweli wabaya wa hii nchi ni watanzania wenyewe.

Mkuu unataka serikali iache kuvifuatilia hivi viwanda na mashamba wajenge vingine?
 
Kama Nyumba haina ubora tafuta yenye ubora mnaongea ujinga tu mnajua gharama za Ujenzi ?

Mkuu mtu ungetegemea azungumzie masuala ya kupunguza bei za vifaa vya ujenzi badala yake wanakimbilia kulahumu ma landlords!! Kuna uwezekano mkubwa mleta mada ana bifu na landlord wake.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom