Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Kwa ubora wa rais tulienae nakubaliana na wewe kabisa kwa asilimia kubwa tu. Hivi vichwa viwili vinatosha kabisa kuendesha nchi hii, yani rais na PM wake tu.

Ila kwa kuwa rais kaapa kuilinda katiba ya nchi, lazima afanye uteuzi wa mawaziri na manaibu kama katiba inavyo elekeza.
Na aendelee kutumia ilani na sera za ukawa maana ndy anawasomesha # lumumbaz
 
Huu ni mtazamo wangu. Napendekeza hawa mawaziri wasiwepo awepo waziri mkuu tu ambaye atakuwa anawakilisha shughuli za serikali bungeni. Mimi naona mawaziri wako kisiasa zaidi, maana raisi wetu anajaribu kupunguza matumizi ni bora kusiwepo na baraza la mawaziri ili tusonge mbele.

Ni maoni yangu tu.

Ni wazo zuri. Kwa hiyo ikifika kipindi cha Bunge la bajeti makatibu waende bungeni kuwasilisha bajeti zao, au vipi.
 
Ni wazo zuri. Kwa hiyo ikifika kipindi cha Bunge la bajeti makatibu waende bungeni kuwasilisha bajeti zao, au vipi.
Yap. Na itakuwa vizuri sana ili kazi ziende mbele.
 
Yap. Na itakuwa vizuri sana ili kazi ziende mbele.

Ila wewe jamaa sasaivi jukwaa la intelligence sijui unaliogopa au vipi.
Mbona kule hufiki tena Mr? Njoo bana uwepo wako ni wa muhimu.
 
Mh. Rais awashughulikie wafanyakazi wa serikali wenye vyeti feki na wale wote wanaotumia cheti kimoja kwa watu wawili na wote wameajiriwa serikalini.
Hawa wanazuia ajira kwa wasomi wengine wenye vyeti vyao halali. Wako wengi mno serikalini.
 
Serikali ya Dr. Magufuli ninaomba imtoe Paul Makonda kwenye nafasi ya u-DC kwa kuwa aliwahi kutuhumiwa kufanya kosa la kumshalilisha Jaji Warioba.
Na uchunguzi ukibainika kuwa alitenda kosa hilo basi afikishwe mahakamani.

Pia Dr. Harison Mwakyembe asichaguliwe kwenye Baraza la Mawaziri lijalo kwani alikiuka kiapo cha kulinda siri za Baraza la mawaziri kwa kuweka hadharani mambo yaliyozungumzwa ndani ya serikali na baraza la mawaziri wakati wa kampeni.
 
Binafsi naumia sana kuendesha nchi kwa maamuzi binafsi,BOT wamekuwa vinara wa matumizi na uchapaji fedha ambazo hazikidhi matakwa na ubora wa matumizi,ukiangalia sarafu ya sh 500 imeingia kwenye mzunguko na baada ya miezi chache haiko tena,pia noti mpya kuanzia sh 500~10,000 zilitengenezwa chini ya kiwango hivyo kuingiza hasara taifa kutokana na kuhitaji marekebisho ya kila mara,hii ni kama hujuma kwa uchumi wetu,tafadhari mh. rais naomba uliangalie hili kwa macho matatu
 
Kwa kasi aliyonayo si ajabu Ukawa wakapendekeza ichapishwe noti yenye ubora na yenye kichwa cha Magufuli ili tubaki na kumbukumbu!
 
Kwa kasi aliyonayo si ajabu Ukawa wakapendekeza ichapishwe noti yenye ubora na yenye kichwa cha Magufuli ili tubaki na kumbukumbu!

Hakika mkuu,mi nakiri kuwa nilikuwa nampinga sana jamaa lakina kwa sasa namkubari kwa 99.99%
 
bot ifutwe kuanzishwe chombo kingine jina hili lishakuwa na mikosi ndicho chanzo cha kuporomoka kwa shilling
 
Jaman wanabody mnamjua huyu mtu Andy magufuli kwani alikua anafanyaga kazi wapi sio BOT naomba mnisaidie
 
Kwani zile sarafu za 500 ziko wapi, ziliondolewa au ?
Zile sarafu za sh 500 kuna watu walikuwa wanazinunua sh 4000 kwa moja, sijui walikuwa wanazipeleka wapi ila ilikuwa inasemekana walikuwa wanazitumia kama silver
 
Binafsi naumia sana kuendesha nchi kwa maamuzi binafsi,BOT wamekuwa vinara wa matumizi na uchapaji fedha ambazo hazikidhi matakwa na ubora wa matumizi,ukiangalia sarafu ya sh 500 imeingia kwenye mzunguko na baada ya miezi chache haiko tena,pia noti mpya kuanzia sh 500~10,000zilitengenezwa chini ya kiwango hivyo kuingiza hasara taifa kutokana na kuhitaji marekebisho ya kila mara,hii ni kama hujuma kwa uchumi wetu,tafadhari mh. rais naomba uliangalie hili kwa macho matatu

Mkuu hizo noti zimefanyiws marekebisho gani na lini?
 
Mkuu hizo noti zimefanyiws marekebisho gani na lini?

Pole mkuu kama hujui,pesa inapochakaa huwa kunadawa zinawekwa na kuwa reprented tena,sasa hizi pesa kutokana na kuchakaa mapema ,zinahitaji gharama kubwa kuwa reprented mara kwa mara,nadhan umeelewa mkuu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom