Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Nakubaliana nawe...Magufuli aje na special programme ya kuvutia taaluma za vijana na wazee wa Diaspora..awawekee mazingira mazuri na atengeneze serious "pulling factors"...tuwe na database kabisa ya kujua nani yupo wapi na amebobea katika taaluma ipi..kabla ya expatriate kupata kazi hapa tanzania, lazima tuwe tumekosa mtu wa ndani ya tz na hata diaspora..
 
Ukiona mtu ameikimbia nchi yake na kwenda kufanya kazi ughaibuni, ujue huyo sio mzalendo hafai
 
Je, atafanya makosa kama alivofanya JK kumrudisha J.Mbatia kwenye duru za siasa? Nia ya ccm ni kuufifidha upinzani kwa gharama yeyote ile.... Ngoja tusubir muda uamue coz ameshafungua kesi...
 
Hata hivyo Maghufuli kama uko seriou kwa sababu hata watangulizi wako walianza hivi hivi
1.Tutajie mali zako na madeni yako sasa ili siku ukitoka utueleze umetoka na nini
2.Pia ndani ya siku sitini waliobeba fedha kwa viroba pale STANIBIC zile za ESCROW watajwe majina yao na wafunguliwe kesi haraka.
3.Singasinga wa ESROW awe wa kwanza kuhudhuria kesi ya mafisadi shahidi awe Mh Kaulila
3.Mh Kafulila alidishiwe Ubunge wake haraka

Mmmmh,ngumu kumeza iyo ndugu
 
Kula hawatoacha kula kwani kuna baadhi yao hawategemei mishahara bali wanafanya na biashara za magendo ikiwemo nyara za serikali na ukwepaji wa kodi. Hivyo kuzuia moja kwa moja ni ngumu labda watapunguza.
 
Mawazo yenu sio mabaya lkn siasa ya kibongo haina wapambanaji wa ukwel ni walewale kila siku
 
Huyo Kafulila hakuwa na lolote la maana....mara kumi Zitto kuliko Kafulila.
 
Huyo wachu hana mana yoyote, ndio mana huku jimboni tumempiga chini.
 
Tunaunga mkono mpango wako wa kubana matumizi ya serikali ili fedha hizo zikatumike katika kuwasaidia watanzania.
Kuna kundi ambalo ningependa serikali yako kwa kushirikiana na bunge iliangalie,hili ni la wastaafu wa ngazi za juu ambao hata baada ya kustaafu wanaendelea kulamba asilimia 75 ya mshahara wa aliyeko madarakani.Watu hawa wakiwa madarakani hugharamiwa kila kitu na serikali hivyo posho zao na mishahara hawaitumii kabisa na hawakatwi kodi.Baada ya kustaafu wanapata mafao makubwa lakini pia huendelea kulipwa asilimia 75.

Mh Rais,watu hawa ni wengi kwa sasa na hawafi mapema kiukweli,baada ya kustaafu wanaishi zaidi ya miaka 30 na hii ni kutokana na maisha mazuri na huduma bora za afya wanazopata wakiwa madarakani na baada ya kutoka.Wao wakiugua hutibiwa nje na familia zao.

Kutokana na hilo napendekeza baada ya wao kustaafu waendelee kulipwa asilimia 10 tu ya mshahara wa aliyeko madarakani kutoka asilimia 75.
in a long run tutakuwa tumeokoa pesa nyingi sana!

Sasa hua mnailalamikia nini serikali kama inafanya hvyo kwa wananchi?watumishi wote wastaafu ni waTanzania,wanatendewa vyema maisha bora afu we tena unalaumu,taratibu mpaka tutafikia na kupewa hata wale ambao hawakusoma na kufanya kazi,ndo maana unasikia huko ulaya kuna mataifa yanatoa posho kwa raia au huduma za afya bure na elimu,sasa hii ni nchi changa na bado inajitahidi kufanya hayo afu unaleta lawama.sisi waTanzania kwa kweli MUNGU atusaidie
 
Huyo Kafulila hakuwa na lolote la maana....mara kumi Zitto kuliko Kafulila.

Kafulila kateketezwa na Zito baada ya kumwomba ahamie ACT akagoma wakatibuana wakawa maadui wakubwa ndipo Zito akala njama na ccm za kumhujumu kwa njia za kimafia ilkiwemo Goli la mkono.
 
Huyo wachu hana mana yoyote, ndio mana huku jimboni tumempiga chini, anayempenda amchukue akawe mme wake.

Hakupigwa chini kwa kura bali Zito na ccm ndiyo wamemhujumu kwa kupenyeza Goli la mkono.
 
Mhe Rais Magufuli,
Ni mapema mno kusema lolote kwa sasa LAKINI naomba niseme in advance. Tunajua kuwa Mhe. Kafulila amefungua kesi Mahakama Kuu huko Tabora kupinga matokeo ya ubunge katika jimbo lake. Endapo hatafaulu katika rufaa hiyo, nakuomba kwa kutumia mamlaka yako ya kikatiba uturudishie kijana huyu katika Bunge letu tukufu. Kila Mtanzania anaweza akakumbuka mchango wake kwenye Bunge lililopita.
Ninakuombea mema katika nafasi yako hiyo mpya na nikupongeze kwa ulivyoanza kazi.
Mtiifu,
Oikos

Ugonvi wake na Zito ndiyo umemletea majanga inaelekea alikuwa hajui kuwa Zito ni ccm na akiamua lolote juu yake litawezekana. na sasa Zito yupo busy kuihujumu hiyo rufaa yake mpaka Kafulila ashindwe tena ili aende kumpigia magoti na kuhamia ACT haraka.
 
Mh Rais,watu hawa ni wengi kwa sasa na hawafi mapema ...
Kutokana na hilo napendekeza kulipwa asilimia 10 tu ya mshahara wa aliyeko madarakani !
Good point! eti hawafi haraka he he!!
Hahaha hawafi mapema
wewe jamaa kwahiyo ulitaka wafe???? anyway u have good idea.
Kumbe ni walipwe 10% ili wafe mapema ili serikali iokoe fedha za kuwalipa wastaafu hao?!.
Kama lengo ni wafe mapema baada ya kustaafu, unamaanisha use ya watu hao imemalizika rasmi baada ya kukoma kwa utumishi wao wa umma, ukimaanisha they are better dead than alive?!, hivyo sasa hawana use yoyote bali wanatia hasara tuu?!.

Kwa vile life expectancy ya Mtanzania ni miaka 53 tuu, na umri wa kustaafu ni miaka 60, then ili kuokoa fedha za kuwalipa wastaafu hawa, unaonaje kama serikali ikiweka mekanisim kuhakikisha life ya wastaafu hawa ends at 60 ili mtu akistaafu tuu pia uwe ndio mwisho wa maisha yake, hivyo kutoingizia kabisa hasara serikali yetu?!. (This is very possible kupitia well set cyanide capsules na polonium 360!)

Pasco
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom