Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Tumeona kasi ya kutisha umefanya kazi kubwa mkiwa wawili wewe na pm wako, ushauri wangu hakuna haja yakuwa na mawaziri kazi zao zifanywe na makatibu wakuu wa wizara. Mswada ubungeni na sheria itungwe kuwaruhusu makatibu wakuu wafanye kazi za mawaziri, kupunguza gharama zisizokuwa na msingi.
 
Naanza na wachache;

1. Shubashi Patel

2. Salum Mpuchu

3. RA

4. R1

5. Home Shopping Centre

6. GMS

Ongeza unao wajua

Eneo Lingine kwenye upotevu wa kodi ni kwenye NGOs hasa International NGOs


Experts wote wa kwenye NGOs za kimataifa.
Yaani fedha wanazozipata hapa Tanzania wanaingiziwa kwenye account zao huko huko Ulaya na wanalipwa fedha nyingi sana kutoka Tanzania.usipojipanga watakwambia wako exempted .lakini ukweli ni kwamba NGOs iko exempted lakini siyo mapato ya mishahara ya wafanyakazi.mbona wabongo wanawakata kodi

Pili kuna vikamputi vingi au watu binafsi wa nje wanafanya consultancy Tanzania na wanalipwa madola mengi sana.ila wanazituma moja kwa moja kwenye account zao huko nje na kodi nyingi sana inapotea.hawa wanaingia nchini kwa kivuli cha utalii .lakini wakiwa nchini wanafanya hizo shughuli za kujiingizia hela.wachache sana wanao weza kulipia CTA.lakini siyo kodi ya mapato.halafu tatizo letu tunawaogopa sana wazungu na wao wanalijua hilo.kwamba hawawezi ulizwa zaidi ya work permit.ambao wengi wanazo.ila kuhusu kodi siyo rahisi.wengine watakwambia kuna bi lateral agreement ya double taxation kwa hiyo kodi inalipwa kwao.lakini mara nyingi huwa ni uongo.

Labda serikali ingetuambia tupeleke wapi hiyo taatifa ya wakwepa kodi
 
Bilioni 97 zimeokolewa hadi sasa. Hii ni pesa ya mlipa kodi ambayo ingetumiwa kwa safari za nje na watumishi wa umma.

Ukiwa unaendelea kumdhihaki Dkt Magufuli hapa, yeye anaendelea kubana mianya ya upigaji hela iliyokuwa ikitumiwa na watendaji wa serikali na kuzidisha nguvu zaidi katika makusanyo ya kodi. Lengo ni kutimiza kila ahadi aliyoahidi wakati wa kampeni.

Hadi sasa navyoandika hapa, shule zote nchini kuanzia darasa la 1 hadi kidato cha nne zimepewa waraka wa kupigwa marufuku kuchangisha wanafunzi michango ya aina yoyote ile. Mwanao akikuomba hela ya mchango kuanzia sasa ujue anataka kukuingiza mjini tu.

#HapaKaziTu
Mkuu HAMY-D ni kweli unachosema na hata mimi siwezi kubeza.lkn na mimi km binadamu,najaribu kuonyesha hofu yangu. Nadhani hata ww unajua km madudu haya yanayoibuliwa yapo kila wizara ikiwemo hiyo niliyoitaja..! Hapo ndo wengine tunapata maswali,kwa nini haikuwezekana kukomesha hiyo hali ktk hiyo wizara?? Km ni wakubwa zake walikuwa tatizo,ndo maana natamani aende huko..! Hii nchi ni yetu sote.
 
Last edited by a moderator:
Tue wakweli tu haweziii na hta kuwachukulia hatua mafisadi walio karibu nae pia hawezii na hli neno mtalikumbuka muda ukifika
 
Jukwaa kama hili halitaki majungu. Mje na facts, onyesheni vielelezo kuwa fulani na fulani hawalipi kodi. Otherwise Haya ni majungu, umbea usiokubalika.
 
Wengine ni makampuni ya viongozi wa kisiasa wakiwemo marais wastaafu, mawaziri, wabunge na viongozi waandamizi serikalini, mashirika ya umma na vyama vya siasa. Hawa makampuni yao hayalipi kodi ya serikali inayostahili kwa kutumia nyadhifa zao. Hawa ni wakwepa kodi wakubwa.
 
Koleba

Sina ushabiki na chama chochote.

Sijakuelewa? Ina maana maovu yanayofanyika tannesco ww huyaoni?!
 
Last edited by a moderator:
Ujinga wa Watanzania ni mzigo kwa hili taifa.

Watu kuona NHC inasimamisha maghorofa nchi nzima eti ndio Mchechu anapiga kazi.

Tuelewe kuwa pesa ya kujenga hiyo mighorofa imekopwa benki kwa dhamana ya nyumba za NHC ilizorithi kutoka Registra of Building (ROB) au msajili ya majengo ambayo thamani yake nchi nzima ni trilion 1.5

Sasa hivi NHC ina madeni makubwa sana kwenye mabenki na njia pekee ya kuyalipa ni mpaka hizo nyumba ziuzwe tena kwa faida iliyopangwa na sio vinginevyo. Je, nyumba zinauzika? Hili ndilo swali la msingi.

Taarifa rasmi ya NHC imetolewa (wengi hampendi kusoma na kama mnapenda basi hamjui wapi pakupata taarifa sahihi) inaonyesha kuwa majengo mengi ya NHC hasa ya mikoani HAYAUZIKI.

Hii maaana yake nini, mikopo ya mortgage ambayo NHC imechukua uwa ni ya muda mrefu, na inalipwa kila mwezi, kwa sasa Mchechu anatumia pesa ya makusanyo ya kodi za nyumba kulipa madeni ya benki kwa matarijio kuwa nyumba za NHC baadae zinaweza kuuzika. Ila hilo haliwezekani kwa kuwa nyumba za NHC ni ghali mno na watu wengi mikoani hawana vipato vya kutosheleza kununua nyumba za NHC.

Mchechu kwa kuona anaumbuka akaamua kuingia makubaliano na mabenki ili yakopeshe wanunuzi wa nyumba za NHC mkopo wa nyumba...mbaya zaidi hii jitihada yake haijazaa matunda kwa sababu riba za mabenki ni kubwa na wananchi wengi hawawezi kumudu kuzilipa. Hivyo mortgage finance bongo haina dili.

NHC ni time bomb. Dkt Magufuli amtoe Mchechu haraka ili tupate mtu mwingine wa kuliendeleza shirika letu kwa approach tofauti. Huenda likawa na tija kwa wananchi. Maana hadi leo hatusikii NHC kutangaza nyumba za bei nafuu...nyumba za bei nafuu kwao NHC ni million 48. Sasa kweli mTanzania wa chini atamudu hii!?
 
Huyu ni rais wa watanzania wote na anachofanya ni kurejesha misingi ya uwajibikaji iliyopotea. Habagui na anatenda na kutugusa mioyo watanzania. Hakika tumepata tulichokuwa tunakisubiria kwa muda mrefu.

Tumuunge mkono rais wetu atufikishe kwenye Tanzania ya maziwa na asali.
 
Mheshmiwa Magufuli, naomba utumbue jipu la Idara ya Uhamiaji la kutoa vibali vya kazi kiholela kwa wageni.
 
haswaaaaaaa...swadakta na wagen kujilimbikizia mavyeo ya juu wazawa vyeo chini
 
Inawezekana ndio maana watu wengine walikaona wajiingize walau kwenye udiwani ili wapate huruma za Chama wakianza kushughukiliwa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom