WanaJamii,
Hii ni rai yangu kwa raisi wa Jamuhuri ya Tanzania.Maoni yangu ni yangu binafsi na sio ya mtu yeyote.Kwanza,nampongeza sana Magufuli kwa kazi nzuri anayofanya katika kuleta tija kwa taifa na sio mtu mmoja mmoja.Kuna kasoro katika kufanya na kutekeleza haya maazimio "hapa kazi tu",lakini kwa hali tuliyokuwa nayo nahisi Mungu alipenda tuanze upya kusuka nchi yetu maana ilikuwa imeisha,ikibaki kwa kipande kipande.
Kwa ufupi naweza kusema,nathani tumeona uwozo mwingi sana kwenye kila sekta.Nathani,hata wew msomaji kwa namna moja au nyingine nawewe unahusika katika kuhujumu uchumi,au kushiriki na wale wanofanya hii biashara haramu;sisi watanzania wote tu majipu na tunahitaji kutumbuana kwakweli.Hali ilifika pabaya.
kama nilivyosema,Magufuli anafanya kazi pamoja na mapungufu yake,ila kwangu naona ni sawa na kujenga nyumba juu mchanga.Kufukuza,kusimamisha,kufungana,nk hakuta leta tija kwa nchi kwa muda mrefu maana hii imekuwa sehemu ya maisha au niseme culture kwetu sisi watanzania wote.Ujanja ujanja ni mwingi sana hata katika sekta binafsi na sio tu serikalini.
Na hapa ndio namshauri Magufuli,aanze harakati za kuleta katiba ya wananchi.Katiba ya wananchi ndio itaenda na wakati huu,na kuweza kulinda maslahi ya nchi na sio chama kama ilivyo sasa.
Napenda kuona katika katiba mpya,kuna kuwa na mfumo mpya,structure mpya ya uongozi na ngazi zake ambao pia utapunguza matumizi kutokana na ukubwa wa serikali,na pia kuondoa urasimu kwenye mambo mengi.
Napendekeza,wabunge wasiwe na uongozi mwinigine;hii leo mbunge yuko kwenye bodi,waziri wa wizara fulani,na mamb mengi ambayo sioni umuhimu wao.Pia,napendekeza,maraisi wastaafu washtakiwe kwa makosa waliofanya na pia wapunguziwe nguvu waliyonayo sasa ambayo inawafanya wasiguswe.
Kuna mambo mengi sana ambayo ni ya lazima kuwepo kwenye katiba mpya maana kwa kazi anayofanya sasa,hata akifa leo,au kuondoka madarakani,nchi itarudi kwenye matatizo lukuki tuliyonayo sasa.Napendekeza "CHECK AND BALANCE SYSTEM" ndio system bora itakayofanya kazi kwa haki,ufasaha na kwa tija ya nchi tu.