Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Sawa unatumbua majipu kwa mafisadi hata unawapeleka mahakamani.Lakini watanzania wengine wanakosa gani mpaka kupunguza mzunguko wa pesa na kuwafanya waishi maisha magumu mitaani?

Kwanini usifanye mambo kwa uwiano uliosawa unatumbua majipu, unabana matumizi yasiyo na lazima hiyo ni sawa, lakini pia mzunguko wa pesa unatakiwa uwepo ili maisha yaendelee.

Mh.Raisi Tafadhali liangilie hili kwa umakini mkubwa vinginevyo utaanza kuzalisha Diasporas.
 
Sawa unatumbua majipu kwa mafisadi hata unawapeleka mahakamani.Lakini watanzania wengine wanakosa gani mpaka kupunguza mzunguko wa pesa na kuwafanya waishi maisha magumu mitaani?Kwanini usifanye mambo kwa uwiano uliosawa.Unatumbua majipu, unabana matumizi yasiyo na lazima hiyo ni sawa, lakini pia mzunguko wa pesa unatakiwa uwepo ili maisha yaendelee.Mh.Raisi Tafadhali liangilie hili kwa umakini mkubwa vinginevyo utaanza kuzalisha Diasporas.

Fanya kazi kwa bidii pesa ipo. Usitarajie kufanya kazi kwa kiwango ulichokizoea na ukaendelea kupata pesa uliyoizoea. Ili upate pesa ni lazima ufanye kazi haswa, na hapa ndipo maendeleo yanapotokea. No more free money, thamani ya pesa unayoipata ni lazima ionekane bwana Jackal. Usiwe na hofu lakini, muda si mrefu utazoea na utajifunza kufanya kazi kwa juhudi kubwa na maarifa ili uweze kupata pesa.
 
Sawa unatumbua majipu kwa mafisadi hata unawapeleka mahakamani.Lakini watanzania wengine wanakosa gani mpaka kupunguza mzunguko wa pesa na kuwafanya waishi maisha magumu mitaani?Kwanini usifanye mambo kwa uwiano uliosawa.Unatumbua majipu, unabana matumizi yasiyo na lazima, lakini pia mzunguko wa pesa unatakiwa uwepo ili maisha yaendelee!

Nashukuru mkuu kwa kuliona hilo, maana hali si nzuri kwetu huku wa hali ya kawaida, ....... basi ajaribu kulipa hawa wanaoidai serikali!
 
Nashukuru mkuu kwa kuliona hilo, maana hali si nzuri kwetu huku wa hali ya kawaida, ....... basi ajaribu kulipa hawa wanaoidai serikali!

Ongezeni juhudi na maarifa mtaona kama hamtopata pesa, tatizo wajanja wajanja wa mijini mlishazoea pesa za bwerere. Jitumeni, kuweni wabunifu, Nawahakikishieni kuwa hakuna pesa utakayoipata bila kufanya kazi inayowiana na thamani ya hiyo pesa. TULISHAZOEA VIBAYA SANA, NI LAZIMA SASA TUBADILIKE.
Nchi yoyote iliyoendelea duniani, sifa kubwa ni kwamba wananchi wake wanafanya kazi haswa
 
Utafanya kazi wakati pesa imeshikiliwa utalipwaje? Hujui sasa hivi idara na mashirika ya serikali wamesimamisha malipo. Miradi mingi imesimama hata ile ya halali.Sasa huo mzunguko wa pesa utatoka wapi?
Fanya kazi kwa bidii pesa ipo. Usitarajie kufanya kazi kwa kiwango ulichokizoea na ukaendelea kupata pesa uliyoizoea. Ili upate pesa ni lazima ufanye kazi haswa, na hapa ndipo maendeleo yanapotokea. No more free money, thamani ya pesa unayoipata ni lazima ionekane bwana Jackal. Usiwe na hofu lakini, muda si mrefu utazoea na utajifunza kufanya kazi kwa juhudi kubwa na maarifa ili uweze kupata pesa.
 
Jana kwenye taarifa ya habari ya saa mbii usiku kulikuwa na taarifa ya habari kuhusu kutenguliwa kwa nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mama Anne Kilango Malecela. Pengine uamuzi wako hukuifanyia tafakari kubwa juu ya suala hili. Wewe huwa unasema msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Mimi binafsi NAKUSHAURI umrejeshee Mhe. Mkuu wa Mkoa cheo chake. Kazi ya Ukuu wa Mkoa ni cheo cha kisiasa siyo ya utendaji. Mhe.Mkuu wa Mkoa anapelekewa taarifa na Katibu Tawala wa Mkoa.Waliotakiwa kuwajibishwa hapa ni Katibu Tawala wa Mkoa, Wakurugenzi Watendaji na Maafisa Utumishi wa Hlmashauri husika. Ninayekushauri hujui umri wangu lakini tumeona mengi na tumepitia kwenye uongozi wa Serikali. Narudia tena mrejeshee Mhe. Anne Kilango Malecela wadhifa wake. Wewe ni Rais unaweza kufanya masahihisho wakati wowote na hakuna wa kukuhoji. Mungu akubariki sana.
 
Ulimwelewa lakini Rais? Alisema kuwa licha ya mkuu wa mkoa kufahamishwa kuwa kuna watumishi hewa baada ya uhakiki uliofanywa tena, RC hakuwachukulia hatua walio chini yake ambao walimdanganya. Akasubiri Rais ndo achukue hatua. Matokeo yake kachukuliwa yeye. Uzembe wake ndio umemponza Anne Kilango
 
Mh.Raisi hapa anatoa ONYO Kwa ye yote uliyepewa Dhamana ukazembea kwa namna ye yote ile iwe umedanganywa Atakuondoa tu.Awamu hii si ya lelemama Uliapa na Uliahidi .Viapo vya Awamu ya Tano ni vya kwelikweli siyo cha kuletea mchezo mchezo Dola na kwani Mwenyezi Mungu alikuwa shahidi wa kiapo chako
 
Mheshimiwa Rais ni imani yangu hujambo na unaendelea vizuri na majukumu yako barabara ya kuileta nchi kwenye mstari, ambapo lengo likiwa kila mtanzania anufaike kiuchumi kulingana na raslimali nyingi mungu alizotujalia.

Kuhusu wewe kutengua uteuzi wa RC shinyanga, mengi yanasemwa na wadau mbali mbali. Mimi huko siendi, ispokua naamini mpaka umefikia hatua hiyo umejiridhisha.

Namheshimu Mama Ana Kilango sana. Ni mpambanaji mzuri katika kuijenga nchi zidi ya mafisadi.
Ameteleza pengine kwa kushauriwa vibaya na wasaidizi wake nayeye kuchelewa kuchukua hatua sitahiki zidi yao.

Kuvunjika kwa koleo si mwisho wa ujenzi. Mama Kilango bado ni hazina kubwa inayohitajika.

Miezi michache ijayo mungu akijalia penye uhai, utakua mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi taifa. Pindi utakapokabidhiwa wadhifa huo Naomba utakapokua unaunda secretarieti ya Chama, huyu Mama mpe nafasi.
Naamini atasaidia kuimarisha nidhamu ya Chama kusimamia serikali kwa kua amekwisha umwa na nyoka.
Nawasilisha mheshimiwa Rais.
 
Mh Magufuli mimi ni mwananchi wa kawaida ila kupia hapa nadhani ujumbe utakufikia baba rais. Tumbua majipu mpaka vipele vyote wizara ya fedha, Hazina na wahasibu wote,kuna watu waliokufa mpaka leo wapo kwenye payroll, mishahara hewa kibao.

Pia yale mafungu ya stahili za wakurugenzi pitia na malipo yote ya kwenye mawizara nina uhakika utatumbua majipu mpaka utalia mwenyewe kuna watu walioshindikana huko maserikalini wanakula pesa zako kama haupo kabisa mh rais wanacheza na system tu wanajipatia pesa kiulani baba wakati huku wananchi tunahenyeka na maisha magumu.
Mkuu basi bwana inatosha mbona hivyoo kwani unaugomvi na nani mpaka yakutoke yote hayo
 
Kuna jambo limenitatiza, nimekutana na kisa ambacho kimsingi kimenishangaza na sielewi usahihi wake, mwanzoni wa utawala wa JPM tuliahidiwa kupunguziwa ada kwa shule binafsi kwa maana ya serikali kutoa bei ya ADA ELEKEZI ambazo shule binafsi zinatakiwa kutoza wazazi au wanafunzi, kwa mshangao nimepewa taarifa kuwa mwanangu kasimamishwa masomo kwa sababu mzazi anatakiwa alipe gharama ya kuagiza walimu toka Uganda!!!!🙁🙁 jukumu ambalo ni la mmiliki wa shule husika hebu nisaidieni mchango wa mawazo ndugu zangu
 
Pole sana.....badala ya mtoto kukaa nyumbani hebu mhamishie Shule ya kata fasta
 
Ada elekezi bado haijatoka hivyo wapaswa kufata vile wanavyotaka wao. Ukiona gharama zao hazikupendezi basi muamishie mwanao kwenye shule nyingine.

Pia nashangaa shule anayosoma mwanao wanaagiza walimu kutoka UGANDA ambao kiukweli hawapo such competent. Elimu yao ipo chini ukilinganishwa na ya Tanzania pamoja na Kenya.
 
Kuna jambo limenitatiza, nimekutana na kisa ambacho kimsingi kimenishangaza na sielewi usahihi wake, mwanzoni wa utawala wa JPM tuliahidiwa kupunguziwa ada kwa shule binafsi kwa maana ya serikali kutoa bei ya ADA ELEKEZI ambazo shule binafsi zinatakiwa kutoza wazazi au wanafunzi, kwa mshangao nimepewa taarifa kuwa mwanangu kasimamishwa masomo kwa sababu mzazi anatakiwa alipe gharama ya kuagiza walimu toka Uganda!!!!🙁🙁 jukumu ambalo ni la mmiliki wa shule husika hebu nisaidieni mchango wa mawazo ndugu zangu
Kama hamna hela pelekeni watoto wenu shule za serikali,siyo mnapeleka private then mnaanza kulialia stupid
 
Kumekuweko tabia ya taasisi za serikali zisizo na ofisi kupanga majengo ya watu binafsi.Hili nalo ni jipu.Wakati huo huo unakuta taasisi zingine za serikali mfano NHC,PPF,NK zina majengo ambayo hayana wapangaji au kuna taasisi zina maofisi yanayotumiwa chini ya kiwango.

Hili nalo ni jipu la kutumbua.Kama kuna taasisi inataka majengo ya ofisi inabidi kwanza iangalie taasisi zingine za serikali kama hazina kwanza badala ya kujiamulia tu kwenda kupanga kwa majengo ya watu binafsi kwa bei za kifisadi.
 
Magufuli rais wangu niblazma kasikia maneno yako...
Na lazma atachukulia suala hilo kwa uzito wa juu...!!!
 
Hv ameshashauriwa kuhusu kulitumbua Liligumi na wote walio nyuma/mbele yake...kama bado naomba ushauri wa bure ukufikie rais....hili dubwana linaloitwa LUGUMI ukiliacha litakusumbua uhai wako wa urais....litumbue mapema mno pamoja na wote wanaohusika nalo na hapo utakuwa umejijenhea heshima Kubwa kwa jamii na lolote litakalojitokeza hapo baadae itakuwa rahisi sana kulitumbua...mh ukilikalia hili dubwana kimya litakocost uhai wako wote wa urais...ni Ushauri tu lakini unaweza kuuchukua au kuuacha..
 
Umaarufu wa Magufuli ulikuwa juu kipindi walipokuwa mapacha watatu, JohnMagufuli,Kasim Majaliwa ,Ombeni Sefue,ilikuwa kama neyma,suarez na messi
Mpaka watu wakaona hakuna haja ya kuwa na mawaziri
alipoanza teuzi tu watu wakaanza kuguna ,
kila anapoteua watu wanaguna mmmmmm
sasa chunusi zinatumbuliwa majipu yanaachwa
amebaki messi peke yake,majaliwa hajulikani aliko
mama samia nae kaibukia mwenge wakati tulitarajia mwenge huoungewekwa makumbusho
katibu mkuu kiongozi mpya hata sura yake watu hawamjui
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom