Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
hahahaaa ccm Uzi kama huu wanapita mbali aisee...maana waliko ni maumivu tu...kimwili wanajifanya wanamuunga mkono rais lkn moyoni wako kinyume naye....najua watakuja na povu la kujitakasa ..ukweli majipu hadi pale pale
 
Bahati nzuri ni majipu yale yale yaliyopigiwa kelele na Chadema na baadaye Chadema hiyo hiyo ikaanza kuyatetea
 
Hahahaaa kunajipu moja hv liko skioni kwa mkuu wa kaya ..yaani lenyewe tembo wakiliona tu wanapiga yowe..daah mkuu wa kaya cjui halioni? ha
 
Umaarufu wa Magufuli ulikuwa juu kipindi walipokuwa mapacha watatu, JohnMagufuli,Kasim Majaliwa ,Ombeni Sefue,ilikuwa kama neyma,suarez na messi
Mpaka watu wakaona hakuna haja ya kuwa na mawaziri
alipoanza teuzi tu watu wakaanza kuguna ,
kila anapoteua watu wanaguna mmmmmm
sasa chunusi zinatumbuliwa majipu yanaachwa
amebaki messi peke yake,majaliwa hajulikani aliko
mama samia nae kaibukia mwenge wakati tulitarajia mwenge huoungewekwa makumbusho
katibu mkuu kiongozi mpya hata sura yake watu hawamjui
Mkuu maneno yako mazito sana tena sana
 
Mkuu maneno yako ni mazito sana tena sana naona emejaribu kuangalia tulipotoka na tulipo mara ya mwisho mm kumuona balozi kijazi nilikuwa india ubalozini ila tangu apakia mzigo yake kwenye kontena lake la futi 20 sijamuona tena sijui bado yupo likizo
 
Mh Rais wetu, ukweli huu mchungu lakini ndio ukweli mkuu unaoweza kulisaidia taifa hili nakuwa na future nzuri.
AJIRA KWENYE TAASISI NYETI ZA NCHI HII ZIPITIWE UPYA NA IKIWEZEKANA AJIRA MPYA ZITANGAZWE KWA USIMAMIZA NA MCHUJO WAKITAALAMU ULIO WAZI, MH Rais vilaza wanaligharimu taifa na hatutaweza kufika popote.
Mh Rais nikisema vilaza namaanisha watu wasiona na uwezo kuanzia kitaaluma,kiutendaji na kimaadili, mkuu vilaza hawa ndio washauri,watoa maamuzi na watendaji na mbaya zaidi wamejaa kwenye zile taasisi nyeti zenye msukumo kwenye uchumi wa taifa hili.MKUU UKILIACHA HILI MIAKA 10 ITAPITA KAMA NDOO YA MAJI ILIYOTOBOKA. MKUU UNDA HARAKA TAASISI YA KUFUATILIA HILI KWA MAANA YA KUSAILI TENA UPYA WATENDAJI WA TAASISI MBALIMBALI NYETI KUANZIA JUU MPAKA CHINI HUKO...

MKUU HILI NI LA HARAKA SANA, UKILAZA KWENYE MIFUMO YETU NDIO CHANZO KIKUU CHA MENGI YANAYOTUSIBU, HATUNA WATU SERIOUS NA COMPETENT WAKUTOSHA KWENYE MIFUMO YETU.
 
Mfumo wetu wa elimu pia kama kiwanda cha kuzalisha serious and competent people umeoza vibaya na mpaka sasa hakuna juhudi zozote za kuufufua, mfumo wetu wa elimu kama kiwanda cha kuzalisha watu makini sasa kwa kiasi kikubwa unazalisha uozo ambao ndio huja kwenye ngazi ya uongozi na utawala na matokeo yake tunakosa serious people kwenye mifumo ambao wanaweza kuwa wabunifu na washauri wazuri kwa taifa.. shida zetu nyingi utaona zinasababishwa na incompetent tulionao. Wafanyakazi wengi kuanzia ngazi za juu mpaka chini kwenye halmashauri ni kamlete ambao hawajui wakifanyacho kwenye maofisi zaidi ya kuzogoa tu na kusaini posho... Lakini ukiwaita kwenye vikao ukawauliza ni kipi tunaweza fanya kama wilaya au mkoa usonge mbele ni kuangalia chini na kuvunja vidole, inatia uchungu kwakweli..
 
Well said mkuu! Waliopata ajira kwa ngono (wanawake),waliopata ajira kimjomba mjomba,walionunua vyeti,walioghushi vyeti,waliotoa rushwa,waliopitia kwa sangoma n.k. Na katika msako huo waanzie Jeshi la Polisi kisha idara ya afya na ualimu.
 
Mh Rais wetu, ukweli huu mchungu lakini ndio ukweli mkuu unaoweza kulisaidia taifa hili nakuwa na future nzuri.
AJIRA KWENYE TAASISI NYETI ZA NCHI HII ZIPITIWE UPYA NA IKIWEZEKANA AJIRA MPYA ZITANGAZWE KWA USIMAMIZA NA MCHUJO WAKITAALAMU ULIO WAZI, MH Rais vilaza wanaligharimu taifa na hatutaweza kufika popote.
Mh Rais nikisema vilaza namaanisha watu wasiona na uwezo kuanzia kitaaluma,kiutendaji na kimaadili, mkuu vilaza hawa ndio washauri,watoa maamuzi na watendaji na mbaya zaidi wamejaa kwenye zile taasisi nyeti zenye msukumo kwenye uchumi wa taifa hili.MKUU UKILIACHA HILI MIAKA 10 ITAPITA KAMA NDOO YA MAJI ILIYOTOBOKA. MKUU UNDA HARAKA TAASISI YA KUFUATILIA HILI KWA MAANA YA KUSAILI TENA UPYA WATENDAJI WA TAASISI MBALIMBALI NYETI KUANZIA JUU MPAKA CHINI HUKO...

MKUU HILI NI LA HARAKA SANA, UKILAZA KWENYE MIFUMO YETU NDIO CHANZO KIKUU CHA MENGI YANAYOTUSIBU, HATUNA WATU SERIOUS NA COMPETENT WAKUTOSHA KWENYE MIFUMO YETU.
Mtatapatapa sana enzi ya huyu mkubwa!
 
Hao vilaza ndo mtaji mkubwa kabisa wa ccm, sababu hawahoji chochote, na ni rahisi kuwa control. Nani amekwambia anataka ukweli serikalini huko? kama unataka kutumia weledi nenda private, kule ni kutekeleza maagizo tu, na kupiga kimya, bila kusahau kujaza fomu ya kiapo kwa makonda. Hivi mtu umeapa kuwa mtiifu kwa mkuu wa mkoa unategemea output itoke wapi?
 
Mtatapatapa sana enzi ya huyu mkubwa!

Sio kutapatapa mkuu ila ukweli lazima usemwe, Mh Magufuri anajaribu kuonyesha nia kwahiyo lazima tujaribu kumshauri yale yaukweli maana tunaona kama anajaribu kupotoshwa na tatizo la msingi kufumbiwa macho..
 
tuanze na elimu kwanza. Ndalichako kalewa sifa. awasikilizi wadau juu ya matatizo ya elimu hapa nchini na namna ya kutatua...
 
Well said mkuu! Waliopata ajira kwa ngono (wanawake),waliopata ajira kimjomba mjomba,walionunua vyeti,walioghushi vyeti,waliotoa rushwa,waliopitia kwa sangoma n.k. Na katika msako huo waanzie Jeshi la Polisi kisha idara ya afya na ualimu.

Mkuu ukilaza ni tatizo kubwa sana linaloitafuna nchi hii lakini halisemwi.
 
tuanze na elimu kwanza. Ndalichako kalewa sifa. awasikilizi wadau juu ya matatizo ya elimu hapa nchini na namna ya kutatua...

Kinachotia uchungu mpaka sasa utawala uko kimya na hakuna juhudi zozote zakuamsha elimu yetu iliyolala.
Elimu ni kama kiwanda cha kuzalisha watendaji bora wanaoweza kulisaidia taifa.
 
Kwanza napenda kuonesha masikitiko yangu kwakuwa kuna mamilioni ya makada wa CCM yetu wasioijua Katiba ya chama chetu. Wapo walioiona. Wapo walioigusa. Wapo walioisoma. Wengi hawaielewi. Makada kwa mamilioni wapowapo tu. Hawaijui Katiba ya chama inasema nini na kwa nani. Nasikitika sana.

Rais Magufuli ameingia madarakani na mtazamo wa kukataa mazoea. Anataka watu wabadilike. Wafanye yanayotakiwa na sheria na taratibu zake. Anataka wananchi na hata wanachama wa CCM wawe na mtazamo mpya. Wafuate Katiba ya chama na ya nchi.

Kuna mpango wa kumkabidhi Uenyekiti wa CCM Taifa Rais Magufuli. Kumkabidhi kimazoea na si kikatiba. Katiba ya CCM ya mwaka 1977,Toleo la 2012 inataka Mwenyekiti achaguliwe. Si kukabidhiwa cheo fulani. Ni ibara ya 118 yote ya Katiba ya CCM yetu inayomzungumzia Mwenyekiti wa Taifa.

Ibara tajwa inamtaja Mwenyekiti kama kiongozi mkuu na msemaji mkuu wa CCM. Inatamka kuwa Mwenyekiti huchaguliwa na mkutano mkuu wa CCM Taifa kwa miaka mitano na kwa vipindi viwili. Ibara inasema wazi kuwa Mwenyekiti aweza kuondolewa kwa azimio la theluthi mbili za wajumbe wa Tanzania Bara na wa Zanzibar kwenye mkutano mkuu wa Taifa. Mwenyekiti,ibara inasema,ni mwenyekiti wa mkutano mkuu wa taifa,halmashauri kuu ya taifa na kamati kuu ya halmashauri kuu.

Hakuna mahali ambapo Mwenyekiti anapatikana kwa njia ya kukabidhiwa. Kikatiba. Katiba ya CCM inataka Mwenyekiti achaguliwe. Rais asikubali mazoea yanayokiuka katiba ya chama. Akatae kukabidhiwa. Kam anautaka Uenyekiti,agombee na kuchaguliwa kikatiba. Shime makada wenzangu wa CCM,tujitokeze wakati wa uchaguzi kugombea Uenyekiti!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Ni wazo zuri sana mzee Tupatupa wa Lumumba, ila wakija hapa wataacha kujibu hoja wataanza kulinganisha na vyama vya upinzani ambavyo ndiyo vinakuwa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom