hii fursa adimu mno, yangu ni matano
1. Nyerere alidhamiria kuijenga bongo kuwa heaven kupitia ujamaa ila wasaidizi wake baadhi aidha hawakuwa competent enough, au hawakumwelewa na dira yake nzima au labda walimwangusha i do not know so it is a big lesson to him too! namuasa asimuamini kabisa msaidizi wake yoyote (ila hii iwe moyoni tu asiiseme) na awe anawapima wasaidizi wake performance regularly (kila 3 months wampe ripoti ya kazi zao na waprove kuwa watu sahihi kwa kazi walizopewa ) na anaezembea asimuoneee aibu amuondoe haraka bila kuchelewa
2. alipe walimu vizuri na aboreshe miundombinu mashuleni na vitabu viwe vya kutosha mashuleni na viboko vifutwe! mi naamini binadamu si ng'ombe wa kupigwa pigwa ovyo. watoto wanachukia shule na elimu kupitia viboko! namuomba Afumue mitaala ya elimu ya sasa yote , awashukie watu wa taasisi ya ukuzaji mitaala watafakari mitaala yao inaleta watu wa namna gani maofisini na mitaani! kila mtoto sasa anataka kuwa msanii wa bongofleva tu! kila muajiriwa mpya anataka miezi sita tu ya ajira awe na nyumba na baloon! mi naona hii mitaala ya sasa inajenga jamii ya mafisadi na wapiga dili wa baadae tu!
3. Abane pesa zaidi ya sasa na matumizi yasiyo ya lazima serikalini yaondolewe yote , abane mianya yote ya rushwa na ufisadi , akomeshe ujambazi na ujangili vibaki historia na asijali kabisa mayowe ya watu kuwa hali ngumu kwa maana baada ya muda mrefu kidogo (maybe 2 to 3 years ) ubanaji huu wa mission town ndo utaleta matunda na faida kubwa kwa nchi na utaibua utamaduni mpya na bora kwa wabongo , utamaduni wa kufanya kazi kwa bidii bila kuchagua kazi na bila kuona aibu ya kazi yoyote ilimradi watoto na mke wapate MENU! kwasaasa kizazi hiki tumejaa uvivu, tunataka pesa za haraka haraka kwa njia za ujanja ujanja, tunapenda udalali , showing off, kupiga mizinga wapiga dili , wizi na ufisadi! na tukifika mahali hakuna baba au kijana anaona aibu kubeba zege au kuuza karanga mitaani , hapo sasa ndio penyewe mkuu akusanye kodi za kutosha kwa kila mtu hata anaeingiza 500 kwa siku alipe hata 20!
4. aondoe ushirikiano wa kiuchumi na wazungu achukue wachina! unyonyaji wa wazungu kupitia riba za mikopo yao ni sumu ya maendeleo!
5. wageni wanaoishi bongo bila vibali vya kuishi na kufanya kazi waondolewe kila ofisi warudi makwao, vitambulisho vya taifa viharakishwe! wageni ni hatari kwa usalama na uchumi wa nchi, wanachuma bongo , wanawekeza makwao!