Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Awape posho walimu wote si wakuu wa shule tu kama ilivyoanza kufanyika sasa hivi analeta ubaguzi na chuki kwani wakuu hawana kazi zaidi ya kukaa ofisini, walimu wa kawaida ndio wanaofundisha morali ya walimu inashuka na matokeo yake yatakuwa mabaya
Hilo nalo Neno.kila mtumishi ni muhimu kuwa motivated kwa njia moja au nyingine.
 
Mimi nitamuomba aseme neno moja tuu
"Nimeguswa na tetemeko la ardhi Bukoba, Poleni! "
Na roho yangu itapona! .
Pasco
Kamanda,Neno ulilolitabiri limetoka kama mada yako ilivyosema unapokuwa mjeda wa akiba.
 
Ndugu wananchi, nimeyasikia na nitayafanyia kazi "naahidi sitowaangusha" 🙂
 
Nitamwambia ahadi yake aliyoitoa Nyamongo kuhusu malipo ya fidia tarehe 11/09/2016 alipokuwa anapita kuomba ridhaa ya wananchi wa Nyamongo kuwawakilisha ikulu ya magogoni,aliwambia wananchi wa Nyamongo kuwa,sitawavumilia wawekezaji wasiojali wananchi, nikiingia ikulu tu itakapofika mwezi wa pili,wananchi wote wangelikuwa wamepewa haki zao,lakini hadi Leo ni kama ndoto,mgodi unadhurumu ardhi na kuleta madhara makubwa kwa wananchi, mgodi unatiririsha maji yenye sumu kwenye makazi ya watu,mgodi sasa hausikilizi hata unayoambiwa na serikali,hayo ndo ningemkumbusha mh Rais wetu ili anapokuja TARIME mwezi huu afike na Nyamongo ajionee mwenyewe,
Poleni sana Wananyamongo kweli picha tu zinatoa ujumbe na nazikumbuka sana.

Wanaoratibu Ahadi za Mh RAIS Ujumbe wenu huo ktk kupanga Utekelezaji wake.

Wananyamongo wanawakumbusha Ahadi ya Mh Rais
 
Na Ahadi ni Deni lazima utimize
kipindi cha uchaguzi, zile nyimbo zilikuwa na maana sanaa, "mmeipenda wenyewe, chaguo lenu wenyewe....." nadhani hapo melody imekujia malizia mwenyewe

na hii "sisiem ni ile ile oooh ni ile ile" 🙂
 
Nitamwambia asipende kuwatukana wenzake vilaz.a wakati yeye akitukanwa anawapeleka watu mahakamani.
Kuniita mi Kilaz.a kisa nawatetea wanafunzi wa UDOM waliotimuliwa aliniudhi sana.

Awache wapinzani wafanye kazi ya kueneza sera na kutafuta wanachama zaidi. Pia awaache wafanye vikao vya ndani. Nasikia polisi waliwahi kuvamia semina ya TRA wakidhani ni Ukuta.
Lugha ya staha plse jamani
 
AAche kusimanga wananchi na kuwatukana huku wakiwa na majonzi kama hawezi aachie ngazi hakulazimishwa aliomba mwenyewe
 
Urais ni cheo cha msimu miaka 5 au 10 co mingi huwezi jua ya kesho,ishi vizuri na watu,pia mchezo wa siasa hautaki hasira.
 
MH RAIS AKIKUPA NAFASI YA KUONGEA NAE LEO JAPO KWA DAKIKA MOJA TU,

JE UTAMWAMBIA NINI? PAMOJA NA...PONGEZI,USHAURI HATA MAOMBI n.k

Angalizo..maneno ya staha ni muhimu.
Nitamwambia aendelee na msimamo wake huo huo km hakuna shughuli za siasa hadi 2020, hakuna bunge kuonyeshwa "live", hakuna maandamano, hakuna kuhudhuria mikutano ya UN, AU, SADC na kadhalika maana ataokoa gharama nyingi. Kwa ufupi nitamwambia azidi kukaza bolt kila mahali ili fadha ya walipa kodi isipotee bure.
 
hii fursa adimu mno, yangu ni matano

1. Nyerere alidhamiria kuijenga bongo kuwa heaven kupitia ujamaa ila wasaidizi wake baadhi aidha hawakuwa competent enough, au hawakumwelewa na dira yake nzima au labda walimwangusha i do not know so it is a big lesson to him too! namuasa asimuamini kabisa msaidizi wake yoyote (ila hii iwe moyoni tu asiiseme) na awe anawapima wasaidizi wake performance regularly (kila 3 months wampe ripoti ya kazi zao na waprove kuwa watu sahihi kwa kazi walizopewa ) na anaezembea asimuoneee aibu amuondoe haraka bila kuchelewa

2. alipe walimu vizuri na aboreshe miundombinu mashuleni na vitabu viwe vya kutosha mashuleni na viboko vifutwe! mi naamini binadamu si ng'ombe wa kupigwa pigwa ovyo. watoto wanachukia shule na elimu kupitia viboko! namuomba Afumue mitaala ya elimu ya sasa yote , awashukie watu wa taasisi ya ukuzaji mitaala watafakari mitaala yao inaleta watu wa namna gani maofisini na mitaani! kila mtoto sasa anataka kuwa msanii wa bongofleva tu! kila muajiriwa mpya anataka miezi sita tu ya ajira awe na nyumba na baloon! mi naona hii mitaala ya sasa inajenga jamii ya mafisadi na wapiga dili wa baadae tu!

3. Abane pesa zaidi ya sasa na matumizi yasiyo ya lazima serikalini yaondolewe yote , abane mianya yote ya rushwa na ufisadi , akomeshe ujambazi na ujangili vibaki historia na asijali kabisa mayowe ya watu kuwa hali ngumu kwa maana baada ya muda mrefu kidogo (maybe 2 to 3 years ) ubanaji huu wa mission town ndo utaleta matunda na faida kubwa kwa nchi na utaibua utamaduni mpya na bora kwa wabongo , utamaduni wa kufanya kazi kwa bidii bila kuchagua kazi na bila kuona aibu ya kazi yoyote ilimradi watoto na mke wapate MENU! kwasaasa kizazi hiki tumejaa uvivu, tunataka pesa za haraka haraka kwa njia za ujanja ujanja, tunapenda udalali , showing off, kupiga mizinga wapiga dili , wizi na ufisadi! na tukifika mahali hakuna baba au kijana anaona aibu kubeba zege au kuuza karanga mitaani , hapo sasa ndio penyewe mkuu akusanye kodi za kutosha kwa kila mtu hata anaeingiza 500 kwa siku alipe hata 20!

4. aondoe ushirikiano wa kiuchumi na wazungu achukue wachina! unyonyaji wa wazungu kupitia riba za mikopo yao ni sumu ya maendeleo!

5. wageni wanaoishi bongo bila vibali vya kuishi na kufanya kazi waondolewe kila ofisi warudi makwao, vitambulisho vya taifa viharakishwe! wageni ni hatari kwa usalama na uchumi wa nchi, wanachuma bongo , wanawekeza makwao!
Ujumbe mzuri ktk kupiga hatua na kulisaidia Taifa.umefika kwa wahusika.thanks
 
1. Aangalie jinsi ya kukuza ajira kwa vijana kupitia bank ya kilimo. Mfano, badala ya bank kuendelea kuomba cashflow za mradi, dhamana nk wawe na utaratibu wa kusimamia miradi ya vijana wenye uhitaji wa mkopo kwa kuwapatia mtaalam wa fani husika kuanzia mwanzo wa mradi mpaka unasimama. Vile vile wawe na utaratibu wa kulipa fedha za mahitaji moja kwa moja kwa supplier au vibarua nk.....hapa bank itawezesha ajira kwa mwenye shamba na yule afisa mradi anaesimamia.
.2. Atoe muundo wa serikali
 
OMBI LANGU KWA MHESHIMIWA RAIS WETU DKT MAGUFULI KUHUSU MIKATABA MIBOVU YA MADINI.

Kwanza napenda kumpongeza sana Mheshimiwa Rais wetu Mpendwa Dkt John Pombe Magufuli kwa kazi nzito na kubwa ya kufumua mfumo aliokuta na kutengeneza mfumo mpya unaoendana na matakwa yetu wananchi ya muda mrefu. Mheshimiwa Rais amejitahidi sana kutumbua majipu na kuziba mirija ya ufujaji wa mali za umma,watu waliokuwa wanakwepa kodi katika awamu hii wamedhibitiwa kwelikweli, hilo ni jambo zuri sana kwani limepelekea mapato ya serikali kuongeza maradufu ukilinganisha na awamu zilizopita.Pamoja na kufunua mifumo mbalimbali na kukutana na uozo mbalimbali Raisi wetu hajasita kuchukua hatua ndio maana nampongeza kwa hilo.

Jambo la pili, Namuomba sana Mheshimiwa Rais wetu Mpendwa Dkt John Pombe Magufuli sasa ajielekeze katika kufumua mikataba yote ya madini ambayo ilikwisha kusainiwa nyuma, kwani mikataba hiyo ni yakinyonyaji na imekuwa inalikosesha taifa letu mapato mengi sana.Nchi yetu imebarikiwa sana na Mwenyezi Mungu, haipendezi hata kidogo serikali kuendelea kuongeza kodi kwa wananchi wanyonge huku madini yetu yakiachwa vilevile. Katika bajeti iliyosomwa na serikali mwaka huu binafsi sijaona ongezeko la kodi katika sekta ya madini. Namuomba sana Mheshimiwa Rais wetu sasa anze kutumbua majipu yote yaliyopo katika madini yetu,kwani huku ndiko kuna ufisadi mkubwa sana na serikali yetu kupitia kwenye madini ndiko inakoibiwa sana. Ninapendekeza katika mikataba ya madini watanzania tunufaike kwa 60% huku wawekezaji wao wachukue 40% ya mapato yanayotokana na madini kwa mwezi nasio kama sasa ambapo sisi ni 4% tu ndio tunanufaika huku wawekezaji wao wakichukua 96%,ndio maana nasema hii mikataba ni yakinyonyaji sana.Haiwezekani kabsa madini ni yakwetu ila kwa sababu wao wawekezaji wanamitambo ya kisasa ya kuchimbia madini yetu ndio wachukue 96% huku sisi tukiachiwa 4% ya mapato yatokanayo na madini kwa mwezi. Mheshimiwa Rais wetu Mpendwa Dkt John Pombe Magufuli, ninakuomba ufumue mikataba yote ya madini ili tuanze upya.. Kutokana na mikataba mibovu ndio maana sekta ya madini imekuwa inachangia mapato kwa kiasi kidogo sana ukilinganisha na sekta ya utalii ambayo ndio inaongoza kwa kuchangia pato kubwa la taifa kwa mwaka.

Mwisho, namuomba sana Mheshimiwa Rais wetu Mpendwa Dkt John Pombe Magufuli asijekuogopa kwa hili la kufumua na kusuka upya mikataba yote ya madini kwani Watanzania wazalendo tuko nae bega kwa bega tunamuombea sana.

Mungu ibariki Tanzania.
Mungu mbariki Mheshimiwa Rais wetu Dkt Magufuli na viongozi wengine wa serikali pamoja na watanzania wote wapenda amani na maendeleo. Amen!!!.


Wako,
Abel Magembe Lugimba.
Mbunge wa Akiba-Jimbo la Kalambo,Rukwa (2020-2025).
 
Ninawasiwasi na waliostructure JD ya Rais wa Tz make vitu muhimu kama kuangalia mikataba mibovu ni kimya tu
 
Siku Magufuli akiwagusa wawekezaji wa madini Tanzania haitokuwa na muda na kuwa kama Congo. Magufuli ni kikatuni lakini hao jamaa ndio Wahuni.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom