Katika utendaji kazi sehemu yoyote ile hapokosi unafiki, ghiliba, usaliti na uchonganishi wa aina yoyote ile. Na haya yote yanatokea pindi pale mtu anafanya kazi ktk misingi mema, mazingira mazuri ambayo yanatetea kundi la watu fulani ambao kwa namna moja ama nyengine. Watu ambao watakuwa wanakupinga na kukusema vibaya ni wale watu ambao umegusa maslahi yao, watatumia ushawishi mkubwa, fitna nyingi, uchonganishi na uchochezi wa hali ya huu ili wakugombanishe na boss wako.
Lakini kitu kikubwa unatakiwa unatakiwa usirudi nyuma katika kutetea maslahi ya watu wako Bali unatakiwa kuongeza nguvu na spidi ili ulete haki na usawa kwa RAIA wote bila kuwaogopa hao wachonganishi kwani ukirudi nyuma utageuka jiwe.
Najua hadi dakika hii hawajaelewa nini namaanisha lakini endelea kuniazima sikio lako utanifahamu vizuri. Kipindi cha nyuma cha uongozi wa hayati Mwalimu Julius kambarage Nyerere wakati akihutubia mkutano mmoja hivi aliwahi kutoa hadithi Fulani. Hadithi ile ilikuwa hivi " kulikuwa na msichana mzuri sana mmoja katika kijiji fulani, wanaume wengi walivutika na ile uzuri wake na wakataka wampose. Binti huyu alikuwa anaishi mlimani lakini mpaka ufike kule alipo kuna vikwazo na masharti.
Waliojitokeza kwenda kumposa yule binti walikutana na bibi kizee, bibi huyu alikua anamuuliza kila mmoja utaweza kufika kule mlimani? Kuna kelele nyingi na za kutisha na unatakiwa wakati unaenda ukisikia hizi kelele usiangalie pembeni wala nyuma, ukigeuka nyuma au pembeni utakuwa jiwe.
Watu wengi walipopewa haya maagizo yaliwashinda kwani kadri walipokuwa wanamkaribia yule binti mrembo kelele zilikuwa nyingi na vishindo vikubwa wakisema huyoo huyoo mchinje mchinje. Kutokana na kelele kuwa nyingi wakawa wanageuka nyuma na kuwa mawe. Basi lile eneo la mlimani lilikuwa na mawe madogomadogo mengi sana ambao ni watu.
Siku moja kijana mmoja mdogo sana alijitoa mhanga kwenda kule mlimani kwa yule binti. Kulikuwa na vitisho vingi sana lakini yule kijana hakuangalia nyuma wala pembeni na kufanikiwa kumfikia yule binti "
Dhima ya hadithi hii ni kwamba tusiwe waoga kma tumeamua kufanya jambo fulani. Lengo langu ni kumuomba na kumsihi Mh Rais john pombe magufuli asikubali kugeuka jiwe, nadhani sasa mmeanza kupata lengo la hadithi na ninachokimaamisha.
Mh JPM ana nia ya dhati na thabiti katika kuwatumikia wananchi, ana nia na lengo la kupigania haki za wanyonge na kuwaepusha watanzania kutoka katika dhuluma, unyonyaji na ufisadi kutoka kwa baadhi ya watu wasiokuwa na nia njema na taifa hili. Wanapiga kelele nyingi,vishindo vingi ilikumkwamisha Rais wetu mpendwa ili nae ageuke Jiwe. Wakisikia Rais kafanya mazuri wanapinga,akinunua ndege wanapinga,akihakiki wafanyakazi hewa wanapinga,akitumbua wazembe na wapiga dili wanapinga lengo ni kumkwamisha Rais wetu ili nae ageuke jiwe.
Ombi langu kwa Mh Rais usikubali kugeuka jiwe kwa kelele za wabaya wasio na nia njema na thabiti kwa taifa letu, sisi wengine tupo nyuma yako kwa kila jambo. Kama ulikuwa unatumia spidi ndogo katika kuendesha nchi, ongeza mara mbili yake na wala usimuogope mtu kwani wewe ndo Nyerere, Nkurumah na Mandela uliyebakia Africa.
Prof Otieno Lumumba wa Kenya University alishawahi kusema "People are saying Nyerere is dead, but for me Nyerere is still alive, Nyerere is alive in Magufuli. What Magufuli is doing is what Nyerere did in his era, so I see Nyerere, Nkrumah and Madiba in Magufuli".
Please Rais usikubali kugeuka jiwe, watanzania tuko nyuma yako.
Na Fumbwe Rashidi Ngassa