Maoni ya mahakama kabla ya hukumu

Maoni ya mahakama kabla ya hukumu

Sagungu 1914

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2016
Posts
938
Reaction score
581
Naomba kuuliza wataalamu wa Sheria,maoni yanayo tolewa mahakamani kuelekea kutolewa hukumu yenyewe ndio yanatoa hukumu itakavyo kuwa?Asante
 
Naomba kuuliza wataalamu wa Sheria,maoni yanayo tolewa mahakamani kuelekea kutolewa hukumu yenyewe ndio yanatoa hukumu itakavyo kuwa?Asante
Fafanua vizuri zaidi ili ueleweke.

Kesi inahusiana na suala gani hasa? Kesi ya Ardhi?

Maoni ya Wazee wa Baraza (Assessors) huwa yanatoa Muongozo wa awali au Mwelekeo wa namna Hukumu ya mwisho itakavyokuwa, ingawaje Hakimu anaweza akaja na Uamuzi wake ambao unatofautiana na Maoni ya Assessors
 
Leo tarehe 26.2.2025 hukumu imetoka na hakimu kampa ushindi mujibu maombi,kinacho nisikitisha na kunishangaza ni Namna gani mpinzani alivyo pata huo ushindi kwani Toka kesi inaanza mpaka kusikilizwa Kwa kesi husika hakuwa na hoja za msingi Wala vielelezo vya msingi kumwezesha kupewa ushindi,kila mtu alijua ushindi huko kwangu lakn mwisho wa siku meza ikapinduliwa,Iko hivi jamaa alikuja nyumbani mwaka 2015 akaomba awe anakaa kwenye Nyumba yetu iliyo kuwa kijijini kwetu katika vile viwanja vya operation vijiji vya mwaka 1974,akapewa kwani tunaye ukaribu,ndani ya kiwanja husika Kuna makaburi matatu na miti ya matunda(machungwa na miembe),ilipofika mwaka 2022 tukamwambia atoke akadai eneo husika ameisha pewa na serikali ya Kijiji eti sisi tumetelekeza Kwa muda mrefu,tukapelekana Baraza la kata tukamshinda akagoma kutoka,tukampeleka mahakama ya wilaya tukapeleka mashahidi wakaongea vizuri tu,zamu yake akaleta shahidi mmoja na barua Moja ya mchongo iliyo kuwa imerushwa mwaka mpaka 2010 eti ndio alikabidhiwa na serikali ya Kijiji,katika barua husika hakuna jina Wala sahihi ya mwandishi,vilevile hakuna jina Wala sahihi ya mpokeaji,istoshe alipo ombwa mitasari ya vikao na matangazo kuhusu kugawa hicho kiwanja hakuwa nayo zaidi ya hicho kielelezo kimoja.Naomba msaada wenu wa kisheria jamani nifanyeje ili niweze kupata haki yangu ya kiwanja na haki yangu ya kutunza makaburi ya ndugu zangu, asante.
 
Suala hili inavyoonekana wewe ulizembea kwa kiasi fulani, ulipaswa uwe makini wakati wote kabisa.
Kuna rushwa Sana kwenye Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya, kwenye hayo Mabaraza kinachoangaliwa zaidi ni RUSHWA wala siyo HAKI.

Kwa kuwa Hukumu ya Kesi tayari imeshatoka, unachopaswa kufanya kwa Sasa ni Kukata Rufaa katika Mahakama Kuu ili kupinga Hukumu hiyo endapo kama haukubaliani na huo Uamuzi wa Baraza la Ardhi la Wilaya.

Ili Kukata Rufaa Mahakama Kuu, kwa Sasa unatakiwa kufanya haya yafuatayo kwa kushirikiana na Wakili wako au kwa kufanya wewe Mwenyewe:-

1. Andika Barua kwenda kwa Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi la Wilaya ili Kuomba Nakala ya Hukumu (Judgement), Tuzo (Decree) pamoja na Mwenendo wa Kesi husika (Proceedings).
Hizi ni Nyaraka muhimu sana katika mchakato mzima wa Kukata Rufaa Mahakamani kuhusiana na Kesi yako.

(i) Wasilisha barua hiyo mapema sana na haraka iwezekanavyo ndani ya Siku thelathini (30) bila kukosa kuanzia siku ya Hukumu (26 Februari, 2025). Bila kukosa!

(ii) Andaa nakala (copy) mbili ya barua hizo, hakikisha kwamba wakati unapowakabidhi barua hizo nakala yako ya kumbukumbu utakayobaki nayo inagongwa muhuri wa Mahakama/Baraza la Ardhi la Wilaya ili kuthibitisha kwamba wamepokea barua yako. Zingatia Sana suala hili, la sivyo unaweza ukaishia kuhujumiwa kwa kuanzia hatua hii kwani wanaweza wakapoteZa barua yako na kisha wanadai kwamba haukuwahi kuwasilisha barua yoyote ile ya Kuomba Nyaraka hizo katika Mahakama hiyo. Hatimaye wewe unaweza ukakosa Ushahidi wa kuthibitisha kwamba uliwahi kuomba Nyaraka hizo.

(iii) Fuatilia kwa karibu Sana huko Mahakamani ili upate hizo Nyaraka mapema, ukiona haupatiwi ndani ya siku hizo 30, unapaswa uandike tena barua nyingine ili kukumbushia ombi lako hili. Barua hiyo ya kukumbushia unatakiwa uandike kabla ya Siku thelathini (30) hazijaisha kuanzia siku ilipotolewa Hukumu ya Kesi hiyo, yaani tarehe 26 Februari, 2025.

2. Ukishazipata Nyaraka hizo zote kabisa ndipo uende kwa Mwanasheria wako (Wakili) ili aweze Kukuandalia Rufaa yako na kisha wasilisha Rufaa yako katika Mahakama Kuu.

MUHIMU KUZINGATIA:-
(a) Mtafute Wakili Mzoefu kwenye haya masuala ya Ardhi, pia Wakili aliye Mwaminifu. Kwa Sasa hivi nchini Tanzania kunga janga kubwa sana la kuwepo kwa Mawakili wasiowaaminifu, wamekuwa wakinunuliwa na upande wa Pili wa washindani katika Kesi.

(b) Hakikisha kwamba Wakili wako anafanya Mapitio ya Jalada la Kesi yako (kufanya file perusal) endapo kama hakuhusika katika hatua za awali kwenye Kesi yako. Hii inaweza kumsaidia huyo Wakili katika ku-detect hujuma inayoweza kufanyika dhidi yako.
Kwa mujibu wa tafiti nyingi sana ambazo zimefanyika, Mahakimu wengi sana wamekuwa wakihujumu Kesi za Watu mbalimbali kwa kubadilisha Maelezo ya Mwenendo wa Kesi, Maelezo ya awali kuhusu Mwenendo wa Baraza/Mahakama yamekuwa yakibadilishwa ili kuchepusha HAKI za Watu na kupendelea upande usiostahili, Rushwa ndio sababu za majanga yote haya.

Hata wewe mwenyewe binafsi pia unaweza kuandika barua nyingine ya Kuweza kufanya mapitio ya Jalada la Kesi yako.
NB:Kwa scenario ya Kesi yako na kutokana na Mazingira ya rushwa jinsi yalivyo kwenye hayo Mabaraza ya Ardhi, yawezekana kabisa huenda umehujumiwa na/au utaweza kuhujumiwa kwenye Kesi hiyo ili iendelee kushindwa.
Kwenye Mabaraza ya Ardhi ya Wilaya kuna rushwa Sana.
Tafiti nyingi sana zimefanyika na nyingi zaidi Kati hizo zimethibitisha Ukweli kuhusu suala hili.
 
Asante sana boss,ubarikiwe,yaani mpaka nashindwa kuelewa hakimu kahukumu hii kesi Kwa kumpa mpinzani wangu ushindi Kwa Sheria ipi,nimeumia sana nikiwa kama binadamu,sijui hayo makaburi na miti iliyomo ndani ya kiwanja itakuaje kisheria.
 
Back
Top Bottom