Hivi kitabu cha historia, au jiografia, au sayansi, kilichosomwa na mababu zetu ndio hichohicho tunachosoma sisi leo? Si kunakuwa na edition tofauti tofauti zimepita tangu kipindi hicho cha mababu zetu?
Edition mpya haibadili quality ya kitabu bali ni maboresho, na theory na principles zitabaki kuwa ni zile zile. Kama kungekuwa na mabadiliko, hata vitu vinavyotengenezwa kwa kutumia theories na principles hizo navyo vingebadilika.
Ndege au meli zilitengenezwa karne nyingi zilizopita, na mpaka leo bado zinatengenezwa, kwa kutumia principles zilezile, lakini kitabu chenye principle hiyo leo sio kile cha karne ya 19.
Kuwa na matoleo tofauti ya vitabu hakubadili ukweli uliokusudiwa. Na hii ndio njia pekee ya kurithisha jambo toka kizazi kimoja hadi kingine. Hatutaki jamii ijayo (au kizazi kijacho) ipotoke, hivyo lazima kuwe na udhibiti wa mambo hayo (consistency).
Vivyo hivyo kwa Biblia, imerithishwa toka vizazi na vizazi, habari zilikusanywa kutoka maktaba mbalimbali na kuwekwa pamoja kwa uangalifu wa hali ya juu. Hakuna mtu aliweza kuipotosha Biblia, kwani mambo yaliyoandikwa yalishuhudiwa na watu wengi!
Hoja ya kuwapo Mungu, hoja ya neno la Mungu, tofauti ya habari za Mungu na habari zingine za watu tu, kubwa kuliko yote, kubwa kabisa, ni moja tu.
Neno la Mungu halina makosa. Neno la Mungu halibadiliki. Neno la Mungu ni ukweli wa milele.
Ukishaona neno la Mungu linaanza kubadilishwa ili liende na wakati, hapo ujue hakuna Mungu, hilo si neno la Mungu, ni neno la watu tu.
Vitabu vinavyoandikwa na watu vya historia, jiografia, sayansi etc, ni lazima vibadilishwe kwenda na muda.
Kwa sababu uelewa wetu wa mambo hayo unabadilika.
Sasa, vitabu vilivyoandikwa na Mungu kupitia watu wake kwa nini vibadilike?
Mungu kashindwa kuandika ukweli usiobadilika?
Ukichunguza sana utaona huyo Mungu hayupo, hivi ni vitabu vimeandikwa na watu tu.
Ndiyo maana vinahitaji kubadilishwa kwenda na wakati.
Na kwa mabadiliko ya sasa ya sayansi na teknolojia, vitashindwa ku keep up, ingawa bado wengi wataviamini kwa sababu saikolojia ya mtu inapenda kuwa na kitu cha kuamini.
Wewe hushangai katika vitabu vyote vya dini vya old world hakuna kitabu chochote kilichotaja bara la Amerika?
Ina maana Mungu hakujua kuna Amerika?