Maoni yangu kuhusu gari aina ya Harrier maarufu "Tako la Nyani"


Kuna jamaa mmoja wa comoro alikuwa anauza yake Milion 10 nikaja nikakutana na mzungu mmoja anauza yake anatafuta hela ya kuondoka kwao milion 6..... Hii gari kwa speed ndiyo mahali pake
Haukusumbui? Yani mkuu nilioinunua kwa mtu sijui iligusa maji control yake ikawa inajipiga stata yenyewe nikaona hapa kuna siku nitakuta imekanyaga vichwa watoto
 
Binafsi Huwa Nalikubali sana Vanguard aisee acha Kabisa....limekaa kaa kama Gaidi Fulani....hata Uniwekee Harrier na Vanguard halafu uweke Hela Kwenye Harrier ntachagua Vanguard.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilimsaidia jamaa yangu kuitoa hiyo gari bandarini alikua kakwama, tukawa tumekubaliana nimpe gari yangu ndogo na ela kiasi maana mambo yalimwendea kombo kidogo,
Baada ya kuanza kuliendesha kama mwezi niliponea kupiga chini, nilibadili makubaliano akamuuzia jamaa mwingine, maana kwa nnavyojijua ile gari ingekuja niacha kilema km sio kuniua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hizi gari zina share same engine na MARK X ZIO, unaweza kutoa uzoefu wowote juu ya mark x zio?
 
Liendeshe siku moja..pita nalo hata barabara ya vumbi afu urudi tena na mrejesho
Nilishaliendesha Dar to Songea zaidi ya mara tano nilijikuta natumia akili nyingi sana, maana mimi napenda sana mbio, lakini lenyewe ukifika 140 unaona kabisa linataka kupaa. Nimebaki zangu na GX 110 ndo mpango mzima natembea hadi namaliza kisahani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…