Mimi natumia Lexus Rx 400h yenyewe ina speed 240k/h though body kama la hio harrier!Ivi mnaposema hii gari ina speed mnazungumzia nini? Ile 180K/h ama?
Sent using Jamii Forums mobile app
Haina jinsi kama unataka kukwepa uniformity katika magari, maana mnaweza kujikuta watu kama 20 wote mmepaki ist.Aaagh, sipati picha aisee..
Kluger inameza mkuu!! Nimeidalalia juzi,mteja katoa hela nusu! Baada ya kuitumia kidogo ananiambia nifanye mpango arudishe hata Robo tatu ya kiasi alichonipa tuli re-sell!! Hata hizo "Tako la nyani" anazozisema Mshana Jr si zote zinakula mafuta kidogo! Kuna zinazomeza kama majini!! Maana si zote ni vVti engines! Sijui mengi kuhusu hii gari ila nilimuuliza mtaalamu mmoja akaniambi kwa kifupi tu kuwa zipo ambazo ni Hybrid,na ambazo si Hybrid!! Sikumwelewa sana ila ninachoelewa ni kuwa kuna zinazokula mafuta mengi na zisizokula mengi!
Ila kuna jamaa yangu ananiambia zile Harrier za Engine ya 1MZ (Jini) ambazo ni cc 3000 ziko na uwiano mzuri kati ya bodi na nguvu,uzito wa Engine. Shida aliyoniambia ni kuwa gari inakula mafuta na engine ya 1MZ siyo nzuri kama 2AZ.Waambie tu ukweli mkuu usiwafiche, Harrier inakimbia sana ila ni nyepesi mno, yaani ni kama vile engine imezidi body....Harrier kuhama njia ni kitu kirahisi mno, na kama uko speed kali na ukakata kona haishiki chini so ni rahisi kupinduka tofauti na Sedan yoyote ile! Mtu anayependa speed kwa kweli simshauri kabisa anunue Harrier
Sent using Jamii Forums mobile app
Mie naishi Mwanza unachosema ni sahihi kabisa. Zimejaa sana zenyewe ist na spacio
Yeah hiyo sio mbaya, au mtu kama ana mapenzi makubwa na muonekano wa Harrier basi bora achukue Lexus RX330 ambazo ni Luxurious Version of Harrier, hizi ziko vizuri kwenye uwiano wa body na engine, pia zinaaminika zaidi kuliko Harrier za ToyotaIla kuna jamaa yangu ananiambia zile Harrier za Engine ya 1MZ (Jini) ambazo ni cc 3000 ziko na uwiano mzuri kati ya bodi na nguvu,uzito wa Engine. Shida aliyoniambia ni kuwa gari inakula mafuta na engine ya 1MZ siyo nzuri kama 2AZ.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mark XGari zilizomaliza vijana ni altezza na gx100......zikafatia verossa na noah
Sent using Jamii Forums mobile app
Ni gari comfortable sana na iko stable sana kwa barabara, khs kupata ajali sana labda kama ulivyosema zipo nyingi na wengi wanapenda sana kuzitumia kwa safari za masafa marefu, ila ukitembea kwa speed moderate 100km/h mpk 120 , hakuna shida....kimsingi gari yyt ukileta ujuaji mwingi inakumwaga.
Jamani ata kapicha ili wasiojua sijui km na mimi nimo tujue..Ni model ya gari ya Toyota Harrier kizazi cha vvt-i (umeme mwingi mafuta kidogo)... Huku kwetu tunaita new model... Lakini kimsingi sio new model kwa huko Japan..
Kwa kawaida Harrier ni gari zinazosifika kwa ulaji mbaya wa mafuta lakini model hii TAKO LA NYANI ni tofauti na model nyingine
Uundwaji wake umezingatia starehe zaidi, kasi, nguvu na ualji mdogo wa mafuta... Hivi vigezo vimewavutia wa bongo wengi mpaka kuifanya ndio gari ya kuuzia sura kwa sasa yani ndio gari inayouza...
Huwezi kukaa dakika kumi mahali yanapopita magari bila kuiona hii gari mpaka sasa inaelekea kuwa Kama sare ya taifa
Neno TAKO LA NYANI limetokana na hii gari taa zake za nyuma zilivyo... Yani zimekaa kama makalio ya nyani gendaeka.. Yule mwenye makalio mekundu...
Lakini ni wangapi wanajua hatari za hii gari gumzo la jiji? Kwa taarifa yako ndio gari zinazoongoza kwa ajali zikifuatiwa na Alphard. Unaweza kudhani zina tatizo lakini shida ni sisi wenyewe... Hatujazoea gari zenye take over kubwa na mwendokasi wa fasta...
Hivyo ndugu zangu kama kuna mwenye mpango wa kununua hii gari azingatie haya... Wepesi, mwendokasi na nguvu ya hii gari
Jr[emoji769]
Overspeed mkuu ni general term je kuanzia 100-120kph ni normal na 140-160kph ni overspeeding na je haina balance?
Sent using Jamii Forums mobile app