Maoni yangu kuhusu gari aina ya Harrier maarufu "Tako la Nyani"

Maoni yangu kuhusu gari aina ya Harrier maarufu "Tako la Nyani"

Kluger inameza mkuu!! Nimeidalalia juzi,mteja katoa hela nusu! Baada ya kuitumia kidogo ananiambia nifanye mpango arudishe hata Robo tatu ya kiasi alichonipa tuli re-sell!! Hata hizo "Tako la nyani" anazozisema Mshana Jr si zote zinakula mafuta kidogo! Kuna zinazomeza kama majini!! Maana si zote ni vVti engines! Sijui mengi kuhusu hii gari ila nilimuuliza mtaalamu mmoja akaniambi kwa kifupi tu kuwa zipo ambazo ni Hybrid,na ambazo si Hybrid!! Sikumwelewa sana ila ninachoelewa ni kuwa kuna zinazokula mafuta mengi na zisizokula mengi!
Nyingi sio hybrid bei ya hybrid na Harrier nyingine nitofauti hybrid ni mkasi zaidi
 
Hicho kigari kiliwahi kutaka ligi njia ya bagamoyo Msata, kiukweli ni doro tu mbele myama Brevis, maana kila akijaribu kusogea anaambulia kula moshi tu.., hamna kitu hapo
Mkuu,gari za chini zenye engine kubwa hasa hizi familia ya Brevis,Mark X,Verossa,Athlete ziko chini zinashika sana njia kwa hiyo hata kama kuna kona kutokana na uzito wake,zinachanja mbuga sana. Ila hata hivyo,hizo Harrier nazo ukiondoa kwa sababu ziko juu zinaweza kuwa na kuyumba kidogo,nazo zinatembea sana. Siku zote Sedan ikiwa na uwezo,siyo gari ya kuichezea hata kidogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hicho kigari kiliwahi kutaka ligi njia ya bagamoyo Msata, kiukweli ni doro tu mbele myama Brevis, maana kila akijaribu kusogea anaambulia kula moshi tu.., hamna kitu hapo
Hizo harrier tuachie michepuko, brevis 300 inanifaa zaidi kuuzia sura hapa mjini
 
Kiuhalisia Harrier haina starehe yoyote ile ukitaka starehe inabidi ununue Lexus RX 330 hio ndo luxury version ya harrier ila harrier imependwa na watu wengi sababu Tanzania watu tunaishi kwa kuigana sana mfano wa gari zikizowahi kupendwa Tanzania ni GX ,100, GX110, Mark X, Altezza sasa hivi Crown zimevamiwa sana
Umesema kweli kabisa kaka,, Tanzania watu wananunua magari kwa kuigana na sio kwa kuangalia mahitaji,,
 
Mkuu,gari za chini zenye engine kubwa hasa hizi familia ya Brevis,Mark X,Verossa,Athlete ziko chini zinashika sana njia kwa hiyo hata kama kuna kona kutokana na uzito wake,zinachanja mbuga sana. Ila hata hivyo,hizo Harrier nazo ukiondoa kwa sababu ziko juu zinaweza kuwa na kuyumba kidogo,nazo zinatembea sana. Siku zote Sedan ikiwa na uwezo,siyo gari ya kuichezea hata kidogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Waambie tu ukweli mkuu usiwafiche, Harrier inakimbia sana ila ni nyepesi mno, yaani ni kama vile engine imezidi body....Harrier kuhama njia ni kitu kirahisi mno, na kama uko speed kali na ukakata kona haishiki chini so ni rahisi kupinduka tofauti na Sedan yoyote ile! Mtu anayependa speed kwa kweli simshauri kabisa anunue Harrier

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila 300 si zile zenye 3000cc? Duuh, hatari sana
Kwa wazoefu tunaweza kupanga vipi ulaji wa mafuta wa gari hizi kuanzia linalokula sana hadi la nafuu
1. Verossa 1G cc 1980
2. Veross 1JZ/2JZ cc 2500
3. Brevis cc 2500 na cc 3000(1JZ/2JZ)-D4
4. Mark X cc 2500 na 3000
5. Crown Athlete na Crown Royal Saloon cv 2500 na 3000.
Please kwa wajuzi watuambie na ukiondoa Athlete,Mark X huwa na shida gani? Naona kama gari iko poa sana. Mwenye ujuzi atujuze

Sent using Jamii Forums mobile app
 
53186701_1694478164031982_709294491516796928_n.jpg

Kuna jamaa mmoja wa comoro alikuwa anauza yake Milion 10 nikaja nikakutana na mzungu mmoja anauza yake anatafuta hela ya kuondoka kwao milion 6..... Hii gari kwa speed ndiyo mahali pake
3056987_orig.jpg
Speed na mitochi kila kona. Utaishia kutajirisha wazee wa kurushiana picha kwa whatsapp kwenye road barrier ya mbele
 
Alafu nyingi niza rangi nyeusi
Ni model ya gari ya Toyota Harrier kizazi cha vvt-i (umeme mwingi mafuta kidogo)... Huku kwetu tunaita new model... Lakini kimsingi sio new model kwa huko Japan..
Kwa kawaida Harrier ni gari zinazosifika kwa ulaji mbaya wa mafuta lakini model hii TAKO LA NYANI ni tofauti na model nyingine
Uundwaji wake umezingatia starehe zaidi, kasi, nguvu na ualji mdogo wa mafuta... Hivi vigezo vimewavutia wa bongo wengi mpaka kuifanya ndio gari ya kuuzia sura kwa sasa yani ndio gari inayouza...
Huwezi kukaa dakika kumi mahali yanapopita magari bila kuiona hii gari mpaka sasa inaelekea kuwa Kama sare ya taifa
Neno TAKO LA NYANI limetokana na hii gari taa zake za nyuma zilivyo... Yani zimekaa kama makalio ya nyani gendaeka.. Yule mwenye makalio mekundu...
Lakini ni wangapi wanajua hatari za hii gari gumzo la jiji? Kwa taarifa yako ndio gari zinazoongoza kwa ajali zikifuatiwa na Alphard. Unaweza kudhani zina tatizo lakini shida ni sisi wenyewe... Hatujazoea gari zenye take over kubwa na mwendokasi wa fasta...
Hivyo ndugu zangu kama kuna mwenye mpango wa kununua hii gari azingatie haya... Wepesi, mwendokasi na nguvu ya hii gari

Jr[emoji769]
 
Back
Top Bottom