Maoni yangu kuhusu kauli ya Rais kwa Vijana Na Mustakabali wa Ajira na Kujiajiri ujumbe huu uende pia kwa watunga sera.

Maoni yangu kuhusu kauli ya Rais kwa Vijana Na Mustakabali wa Ajira na Kujiajiri ujumbe huu uende pia kwa watunga sera.

PASSIONATE

Member
Joined
May 20, 2015
Posts
69
Reaction score
27
Salaam! Kwa Wote.
Awali ya yote tuzidi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kufika 2022 salama, tukiwa tunauanza mwaka tunaendelea kutafakari na kuweka malengo ya kupiga hatua kiuchumi.
Vijana wa kitanzania bado wameendelea kukumbwa na changamoto kubwa kwenye sekta ya ajira takwimu zikionyesha kila mwaka graduates kwenye ngazi mbalimbali wakizidi elfu 15(15,000). Huku kanda ya Africa Mashariki kwa nchi wanachama idadi ya wahitimu wakizidi elfu 70 (70,000) kwa nchi wanachama kwa ujumla wake.
Turudi kwenye maada mazingira ya kujiajiri kwa vijana Tanzania.
Kwanza kabisa tuanze kwa kusema ni asilimia 20% tu ya vijana waliomaliza vyuo vikuu Tanzania ndio wanaofanikiwa kujiajiri na kufikia lengo baada ya kumaliza masomo yao baada ya kuanzisha biashara zao.
Kwanza kabisa tuzungumzie mtaji(capital) wa kuanzisha biashara hapa tulenge wale vijana waliobahatika kutokea kwenye familia zenye uwezo kiuchumi ambapo kijana anapewa kiasi cha fedha kwenda kuanza biashara yake kulingana na aina ya biashara.
Tunaposema vijana wajiajiri kwanza kabisa tutazame suala la mtaji, kijana hawezi kuanzisha biashara bila ya kuwa na mtaji tusisitize hapa kwamba wanasiasa na inspirational speakers wamekua wakisisitiza vijana wajiajiri kwa sasa ikienda mbali kufikia hata mfanyakazi anayepokea mshahara akisisitiza kijana jiajiri acha uzembe anza kidogo utafanikiwa ilihali mhusika hakuwahi kuanzisha biashara.

MAJUKUMU YA SERIKALI NA WATUNGA SERA
Kwanza kabisa mitaala ya elimu ipitiwe upya, kundi kubwa la vijana wanaohitimu kidato cha 4 waingie vyuo vya kati mchujo mkubwa ufanyike kupata cream ambayo itakwenda form 5-6 ikiwezekana level ya advanced secondary school itolewe mtaala wake uongezwe hapa form 1 mpkaka form 4 na baadhi ya mambo yapelekwe chuo kikuu ili kupunguza kupoteza muda wa kijana i.e nchi zilizoendelea kwa mfano Marekani,China, Canada na nyinginezo vijana wanakua level za PHD wakiwa 25yrs(hapa tumeweka mkazo kwenye suala la elimu na mifumo yake).

KUTAMBUA VIPAJI
Shule zetu zingelenga katika kujua asili na muendelezo wa watoto kulingana na walichopewa na Mungu talanta ina nafasi kubwa ya kuondoa utegemezi tuna vijana ni wacheza mpira wazuri,wapiganaji wa ngumi,wanariadha, wacheza golf wazuri na michezo mingi mingineyo shule zetu kwa kushirikiana na wazazi wangeanzia hapa ingetufikisha mahali fulani.

JUKUMU LA SERIKALI KWA NYAKATI ZILIZOPO.
Serikali ianzishe program maalum ya kuwaandikisha vijana wote nchi nzima kila mkoa na kila wilaya vijana washindanishwe kimawazo yao kuendana na fursa zinazopatikana katika mikoa husika zipo fursa ambazo zingeweza kufanywa na vijana ila watu kutoka China wanazifanya na zingeweza kufanywa na wazawa endapo watawezeshwa ki fikra na kifedha, vijana wawekwe kwenye makundi kuendana na uwezo wao na wasajiliwe ikiwezekana wapewe mitaji bank chini ya government guarantee na kufuatiliwa kwa karibu, vipo viwanda ambavyo vingeweza kuanzishwa na kusimamiwa na vijana chini ya uangalizi wa serikali, serikali kama ya China imewezesha vijana kuja Africa na kuwapa mitaji chini ya uangalizi maalumu ikumbukwe kwamba viwanda ndio nguzo ya ajira kwenye nchi zilizoendelea(Refer to Most industrialised countries in the world) kiwanda kimoja kinaweza kuajiri mpaka watu elfu3(3000).

Tungependa kutoa mawazo zaidi sisi kama vijana japokua ni kundi linalodharaulika na kubezwa zaidi ngoja niishie hapa.
Nawasilisha hoja
 
Back
Top Bottom