econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 25,522
- 40,795
Kwa press ya Jana ya Lema amekiri kwa kauli zake kwamba yeye ni dalali na anataka CHADEMA irudi kwenye udalali.
1. Kwanza kabisa, Lema kanishtua sana aliposema ya kwamba alikutana na Makamu wa Rais pamoja na Mwanasheria Mkuu wa serikali. Nimeshangaa sana, kwa sababu hata machawa wa CCM na wanachama wa CCM kupata access ya Makamu wa Rais sio jambo dogo. Inakuwaje Kiongozi wa kamati Kuu wa CHADEMA anapata access ya haraka na Makamu wa Rais Tena kwa Njia ya simu. Ina maana mawasiliano yao yamekuwa cleared na TISS. Na kama yapo cleared na TISS basi Lema anajuana na TISS.
Hivyo basi, kama Lema anawasiliana na TISS usalama wa Chama upo hatarini na pia ni rahisi yeye kufanya udalali. Yani katika kipindi ambacho chama kipo kwenye mapambano makali na serikali, Lema yeye ana mawasiliano na TISS. Hii ni hatari sana kwa CHADEMA. Pia nani atameamini Tena Lema? Siri za chama zipo open sana kwa TISS. Huu ni uthibitisho Lema ni dalali mkubwa maana kuongea tu na viongozi wakubwa serikali kuhusu kutoa viongozi Gerezani huo ni udalali.
2. Pili, nimeshangaa Lema kudai kwamba siasa za chuki hazitakisaidia chama cha CHADEMA. Nikawa najiuliza, kati ya CHADEMA na CCM nani ana siasa za chuki?. CCM hii ambayo imemfukuza kwa aibu Dr Nchimbi kisa hotuba yake ya Katiba mpya. CCM hii iliyomteka na kumpoteza Balozi wa Nchi? Hivi kwa madhira na mateso waliyofanyiwa CHADEMA, Kuna haja ya kuwa na upendo kwa CCM? Jibu ni hapana. Viongozi wangapi wa CHADEMA wameuawa huko mikoani?. Viongozi wangapi wa CHADEMA wapo Gerezani?. Kwake Lema ni kwamba CHADEMA na wanaharakati wanafanya siasa za chuki, lakini CCM wanafanya siasa za upendo. Kwangu, naliona kama tusi.
Ni tusi kwa sababu, wanaoonewa hutaki wareact, wakireact ni chuki, ila wanaonea wengine ndio unaona wanaonewa kwa siasa za chuki. Yani CCM kwa Lema inaonewa kwa siasa za chuki kutoka kwa CHADEMA na wanaharakati. Kwa kweli Lema kanishangaza sana. Lema, amesahau CCM walivyomtesa Arusha enzi hizo na walivyosababisha mauaji ya wanachama wa CHADEMA wakati wa uchaguzi wa Meya wa Arusha 2010?. Leo anawalaumu CHADEMA? Aiseeh!!! Kuwaambia CHADEMA wawe na upendo kwa ibilisi shetani CCM ni ujinga wa Hali ya juu na udalali wa Hali ya juu.
3. Mwisho, Lema anadai ya kwamba mazungumzo ndio Njia Bora. Lema anasahau sana, ya kwamba Mwenyekiti Lissu alitoa pendekezo la mazungumzo kwa CCM. Mh Lissu aliomba CCM na serikali yake wazuie uchaguzi mkuu kwa mwaka Mmoja, ili wakubaliane jinsi ya kuendesha uchaguzi mkuu. Cha kusikitisha CCM wakagoma kabisa na hata Kuna vyama vya upinzani vikadai CHADEMA wanataka CCM wabaki madarakani. Inakuwaje Leo Lema anawataka CHADEMA wafanye mazungumzo na CCM ambao hawakutaka mazungumzo hapo awali ?
Ningekuwepo karibu ningemuuliza Lema kama anakumbuka mazungumzo kati ya CHADEMA (kipindi cha Mbowe) na CCM yaliishia wapi? Mazungumzo ya CUF na CCM yaliishia wapi? Ni hiyo CCM ilikuja kumaliza CUF kabisa wakakimbilia ACT. Lazima Lema ajue ya kwamba kwenye mazungumzo yoyote yale, CCM wataangalia madaraka yao pekee. Wao lengo lao ni kuyatunza madaraka basi, hata kama ni kuua watu, mazungumzo sio issue kwao.
Kwa kuhitimisha, Lema amekiri mwenyewe kuwa ni dalali na angependa CHADEMA wafanye siasa za udalali. Niwashauri CHADEMA watupilie mbali ujinga wa Lema na waendelee na msimamo wao. Maana wakiyumba kwa msimamo wao, ni ushindi kwa CCM . Kukubali mazungumzo na CCM ni kama kujifunga goli wenyewe, kabla ya CCM haijaanza kuwafunga.