Maoni yangu: Lema ni dalali na anataka CHADEMA irudi kwenye udalali

Maoni yangu: Lema ni dalali na anataka CHADEMA irudi kwenye udalali

Kuna mambo mengi ya kushitua katika hii inayoitwa Press ya huyu jamaa:

1. Kasema alimtafuta Nchimbi na Mufti ili waongee kuhusu taasisi yao ya Chadema je alikua na baraka za Viongozi wa Chama chake?? hivi pale CCM mtu au Mjumbe wa Kamati kuu anaweza kujifanyia maamuzi ya kwenda kuonana na mtu yeyote wa Chadema bila kuwasiliana na uongozi wake wa juu umpe kauli za chama au umuelekeze msimamo wa Chama? tunaona hata UKraine kuna Vita kuna mjumbe wa Rais Trump anaitwa Steve Witkof..Wewe Lema ulikua mjumbe wa chama au ulijiamulia mwenyewe kufanya kazi ya kupita huko na huku na je mlichoongea kiliwasaidia nini kama Chama??

2. Lema kasema Alimnunulia Makamo wa Mkiti pikipiki kama nakumbuka Mbowe pia alisema alimpa Lissu Nyumba tukiunganisha doti ina maana nyie mkimsaidia mtu lazima mmtangaze, sijui lengo ni kuonyesha nyie ni wema au mna hela au vipi!! katika hili Lema unaweza kutuambia unafanya biashara gani inayokuingizia kipato?? inayokuwezesha kuishi mana wewe sio Mbunge na hatujui biashara yako ni ipi...

3. Ulisema mwenyewe kwamba Mmoja wa Ndugu wa mliokamatwa alikuja kukuona je mtu huyo alikuja kukuona wewe pekee au wote?? na mtu huyo alikuja ili mridhiane au alitumwa ili awatoe jela?? hapa nina mashaka na hii kauli ulitaka kuhalalisha nini?? umesema pia ulishangaa kesi ya Ugaidi ina dhamana kwanini hukukataa kupewa dhamana wakati huo unakuja kusema unashangaa leo???

4. Lema pia tusaidia kujibu swali hili ulisema Mange amesababishia watu wengi kufa!! hivi Mange ndio anaua watu kumbe?? anateka watu anaiba mauchaguzi huyu dada kumbe ni mtu mshenzi kiasi hiki>?? yaani wewe Lema wa kusema watu wanaouliwa kwasababu ya Mange? wewe kwa hiyo Press yako wabaya wako sio wanaua au kuteka watu ila Mange anaefanya harakati na wananchi ndio wabaya wako...

5. Ushauri kwako Lema tamaa na madaraka havikai pamoja, lazima mmoja aharibie mwingine, CCM sio wajinga wanajua kama huna kazi na huna kipato huwezi kuwa na msimamo njaa huwezi kuidhibiti wewe ni msaliti wa chama na wananchi na hili linaharibu taswira ya sisi watu wa Kilimanjaro tunaonekana ni wasaliti na tusioaminika!!! kwa mantiki hii wewe una machaguo mawili ama ujitoe na kujiuzulu maana umesema mliongea na Sugu kasema amechoka mnatajana wenyewe maana team yenu mliyopanga safu za uongozi ndio mko na akina Sugu hii ni dhambi unataja wenzio mnaohujumu pamoja...

6. Kuhusu Mbowe alipiga kampeni akashindwa uchaguzi halali ila kwa kuwa siasa nyie ni dili na sio kusaidia watu mnasingizia amestaafu Siasa hivi ukistaafu ndio usiende hata kuwapa wenzio pole katika madhila wanapitia?? yeye pia si alikua jela angejisikiaje watu wasingeenda?? huyu ni mtu wa dili na anawaza chadema kama mali yake binafsi wote nyie ni watu wa dili mnatumia mnachoita maridhiano muendelee kuibia nchi hakuna kingine!! ni aibu kuona watu wazima mnawaona wananchi kama vilaza na kuanza utapeli wa kusema Mange kasababisha watu kufa.....

Lema bila wewe siasa zitaendelea tena vizuri sana...bila wewe chadema itakuepo wewe na SUgu na wenzenu wote nyie sio wakubwa kuliko taasisi angalia CCM wanafukuza watu na maisha yanaendelea na Chadema wakikufukuza ujue ndio dili zako zimeisha maana hautakua na relevance so CCM hawatakua na haja na wewe tena.... Aibu iwe kwenu na kizazi chanu wasaliti wote mnaoiumiza Tanganyika....
Umeongea kwa uchungu sanaa
 
Kwa hivyo wewe unaamini Lema ni dalali kwa kuwa candid.

Kutumia ukweli wake kufanya spinning kama huyu mheshimiwa alivyofanya.

Uongozi wa upinzani sio kazi nyepesi; yote tisa muhimu ni uhuru wa mwenyekiti kwanza by ‘hooks or by crooks’. Mengine baadae.
Uhuru Gani wa Mwenyekiti wakati hukumu kesho kutwa? Mwenyekiti mwenyewe kasema hataki huruma kama wanata kumnyonga wamnyonge tu. Tusimtumie Mwenyekiti kama sababu ya udalali.
 
ni mjinga pekee anayesema Lema ana njaa na Hana KAZI haumjui Lema uliza tu usaidike,mmachame asiwe na KAZI😂😂😂😂
Kazi yake si ndio hiyo ya udalali wa siasa. Zamani inadaiwa na CCM alikuwa mwizi wa magari.
 
Mbona hilo jibu rahisi sana jibu kazi au biashara anayofanya utuondoe huo ujinga!! kuwa machame sio akili ndio mana mnauza utu wenu na kuwasaliti wenzenu huko chadema kisa njaa njaa zenu..
Kweli kabisa. Lema ni mfanya biashara ya udalali kama kaka yake Mbowe.
 
Back
Top Bottom