Ni kama vile hayana umhimu vile lakini usiombe!
Serikali ikiwapendeza yawekeni kwenye utaratibu!
Kama hujawahi kuuguliwa au kuuguza huwezi kunielewa kirahisi!
Iko hivi mwaka Jana wakati nikiuguza mzee wangu kabla hajatwaliwa! Yapo mambo yaliniumiza sana!
Ni vigumu kuyaelezea yote hapa!
Lakini naomba kusemea jambo moja la vyoo vya wagonjwa hospitalini!
Ukiachilia hospitals chache, asilimia kubwa ya hospitals Tanzania zinavyoo vya kuchuchumaa!
Yamkini vijana na wenye afya wanaweza chukulia hili lipo sawa!
Lakini ni changamoto kubwa sana kwa wazee na vibonge wanapokuwa kwenye hali ya kuugua, magoti hupungukiwa sana nguvu za kuweza kuchuchumaa mda mrefu!
Hivyo hali ya kujisaidia hawa watu wazima imekuwa inachangia sana homa kupanda kutokana na kushindwa kunyanyuka wakiwa chooni wanapochuchumaa
Kama mjuavyo ugonjwa huja popote ukiwa mkoa wowote! Ni vyema kukawa na sheria inayolazimisha hosipitali zote za serikali na binafsi lazima kuwepo kwa choo cha kukaa kwa wazee na wale wasiojiweza! Ili kuondoa adha na aibu kwa wagonjwa!
Ebu chukulia mfano mzazi anaeuguzwa na watoto wake wa jinsia tofauti! Akishindwa kunyanyuka chooni mtoto inabidi akamsaidie!..INAUMIZA
Hii inawaumiza sana wagonjwa kisaikolojia na huchangia sana kukata tamaa (pia huongeza hofu ya ugonjwa kwao kiasi cha kupunguza hata kinga za mwili)
Hili jambo juu juu linaonekana kama halihitaji ulazima vile! Lakini kiuhalisia linaumiza sana!
Serikali kupitia wizara ya afya naomba mliwekee sheria hili kila kituo cha afya iwe cha serikali au binafsi lazima wawe na vyoo vya kukaa! Na ukaguzi ufanyike Mara kwa Mara kama vyoo hivyo vinatumika!
Kukua ni kuzeeka!
Tusitumie matamko! Tuweke utaratibu wa kudumu!