Maono ya kutisha kupitia ndoto ya usiku wa jumapili

Maono ya kutisha kupitia ndoto ya usiku wa jumapili

Chimbuvu

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2012
Posts
4,401
Reaction score
2,345
Usiku wa leo,wa tarehe 14,siku ya jumapili kuelekea jumatatu.
Nilipata maono katika ndoto.
Niliona mji mmoja ambapo watu walikuwa wakisherehekea ama wakiburudika katika hoteli pembeni ya bahari,ghafla nikaona wimbi moja kubwa sana likija upande wa hoteli na nikaona likiwafunika watu waliokuwa ufukweni na majengo yote,ni kama ilivyokuwa tsunami ,na upande mwingine wa makazi niliona madhara ya hilo wimbi,kwa kuwa sasa yalikuwa zaidi ya moja yakija makubwa na wakina mama walipoteza maisha yao,akina baba,walipoteza maisha yao,na nikaona na watoto waliokufa na watoto wengine waliobaki wakiwatafuta mama zao wasiwaone mpaka wakawa wanachukuliwa na watu wengine..
Kwa kweli ni tukio la kutisha nililoliona.
Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha joel 2 kuwa siku za mwisho bwana atamwaga roho yake na wazee wataota ndoto,vijana wataona maono,na katika mathayo 24 neno linasema mtasikia habari za matetemeko mahali na mahali,na kutakuwapo na dhiki kubwa ambayo haijawahi tokea tangu mwanzo wa ulimwengu mpaka sasa.
Enyi kizazi hichi tubuni dhambi zenu na mpate kumrudia Bwana kwa sababu Huu ndio ule mwisho uliotabiliwa
mtakaposikia hayo yametokea ndipo mtajua kuwa bwana amenena kupitia kinywa cha mtumishi wake.
Shalom..

Kama ilivyoandikwa Mungu hataliacha neno la mtumishi wake lidondoke chini ndivyo ilivyokuwa kwa huu unabii alioutoa kupitia kinywa cha mtumishi wake.
Ambapo katika mji wa niger kumetokea mafuriko makubwa na yameua zaidi ya watu 20 na watu zaidi ya 75000 kukosa makazi.na waathirika wakubwa ni watoto.katika maono niliona wimi kubwa likija na katika habari ni kuwa mto niger ulifurika na kusababisha madhara hayo.
Hii ni ishara ya siku za mwisho kama ilivyo katika kitabu cha joeli 28 neno la Mungu linasema wazee wataota ndoto na vijana kuona maono siku za mwisho.
Mungu anapotoa nabii ni kwa ajili ya kujifunza na kugeuka,,tubuni mkapate kusamehewa dhambi zenu.Yesu yuaja

Niger: Flooding Devastates Niger - allAfrica.com

na Niger asks for foreign help for flood victims | Fox News

CC; Bishanga Mamndenyi Lady doctor Madame B Passion Lady mimisa charminglady C6 Elizabeth Dominick Heaven on earth Chocs Judgement Arushaone Erickb52
 
Last edited by a moderator:
Heaven on earth
nimeshangaa sana kuona hayo maneno yametoka kwa Chimbuvu daah
kumbe usimdharau mtu ambaye humjui.

Ninachoomba kwa Mungu siku zote ni kufa kwema
kwa kuwa .......one day i should die............
Mamndenyi mie mwenyewe nawazaga kama wewe

leo mambo ya bendi ameweka kando,yuko
kimaono tu.........
 
Last edited by a moderator:
"kila nikikifiri kiiiiifooooo machozi hunitokaaaaaaaaaa...."
Them Mushrooms wameimba!
 
Paloma peke yangu aise siogopi kufa,
najitahidi sana kuwaza nikifa leo nitakuwa nimewaachia watoto wangu
kitu gani ili kesho wasiyumbe sana na maisha,
vinginevyo siogopi kufa aise.

"kila nikikifiri kiiiiifooooo machozi hunitokaaaaaaaaaa...."
Them Mushrooms wameimba!
 
Last edited by a moderator:
Mamndenyi kwani nini mbaya?
Halafu mbona chitchat siioni ktk new posts za mobile mpaka uingie kwenye sub forum?


Heaven on earth
nimeshangaa sana kuona hayo maneno yametoka kwa Chimbuvu daah
kumbe usimdharau mtu ambaye humjui.

Ninachoomba kwa Mungu siku zote ni kufa kwema
kwa kuwa .......one day i should die............
 
Last edited by a moderator:
Mungu hapendi kifo, ndio maana 1wakorintho 15;26 inasema 'adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti' kwa hiyo kifo ni adui wa Mungu


"kila nikikifiri kiiiiifooooo machozi hunitokaaaaaaaaaa...."
Them Mushrooms wameimba!
 
Paloma peke yangu aise siogopi kufa,
najitahidi sana kuwaza nikifa leo nitakuwa nimewaachia watoto wangu
kitu gani ili kesho wasiyumbe sana na maisha,
vinginevyo siogopi kufa aise.
Mamndenyi mwenzio naogopa kifo jamani...
sitakagi hata kuwazia
 
Last edited by a moderator:
Mungu huwa anawatumia watu ambao wapo ktk saturation point ambapo hawajui nini ni nini,,mfano Musa alikimbilia kwa mjomba yake na wakati akichunga kondoo ndio akakutana na mgeuko wake.abraham alikuwa kwa baba yake hana mbele wala nyuma na Mungu alimgeuza kuanzia hapo.

kupigwa chini kubaya.... Madame B mrudishe ktk Saccos tu,maana sijui
ka utabiri atauweza!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom