Usiku wa leo,wa tarehe 14,siku ya jumapili kuelekea jumatatu.
Nilipata maono katika ndoto.
Niliona mji mmoja ambapo watu walikuwa wakisherehekea ama wakiburudika katika hoteli pembeni ya bahari,ghafla nikaona wimbi moja kubwa sana likija upande wa hoteli na nikaona likiwafunika watu waliokuwa ufukweni na majengo yote,ni kama ilivyokuwa tsunami ,na upande mwingine wa makazi niliona madhara ya hilo wimbi,kwa kuwa sasa yalikuwa zaidi ya moja yakija makubwa na wakina mama walipoteza maisha yao,akina baba,walipoteza maisha yao,na nikaona na watoto waliokufa na watoto wengine waliobaki wakiwatafuta mama zao wasiwaone mpaka wakawa wanachukuliwa na watu wengine..
Kwa kweli ni tukio la kutisha nililoliona.
Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha joel 2 kuwa siku za mwisho bwana atamwaga roho yake na wazee wataota ndoto,vijana wataona maono,na katika mathayo 24 neno linasema mtasikia habari za matetemeko mahali na mahali,na kutakuwapo na dhiki kubwa ambayo haijawahi tokea tangu mwanzo wa ulimwengu mpaka sasa.
Enyi kizazi hichi tubuni dhambi zenu na mpate kumrudia Bwana kwa sababu Huu ndio ule mwisho uliotabiliwa
mtakaposikia hayo yametokea ndipo mtajua kuwa bwana amenena kupitia kinywa cha mtumishi wake.
Shalom..
Kama ilivyoandikwa Mungu hataliacha neno la mtumishi wake lidondoke chini ndivyo ilivyokuwa kwa huu unabii alioutoa kupitia kinywa cha mtumishi wake.
Ambapo katika mji wa niger kumetokea mafuriko makubwa na yameua zaidi ya watu 20 na watu zaidi ya 75000 kukosa makazi.na waathirika wakubwa ni watoto.katika maono niliona wimi kubwa likija na katika habari ni kuwa mto niger ulifurika na kusababisha madhara hayo.
Hii ni ishara ya siku za mwisho kama ilivyo katika kitabu cha joeli 28 neno la Mungu linasema wazee wataota ndoto na vijana kuona maono siku za mwisho.
Mungu anapotoa nabii ni kwa ajili ya kujifunza na kugeuka,,tubuni mkapate kusamehewa dhambi zenu.Yesu yuaja
Niger: Flooding Devastates Niger - allAfrica.com
na
Niger asks for foreign help for flood victims | Fox News
CC;
Bishanga Mamndenyi Lady doctor Madame B Passion Lady mimisa charminglady C6 Elizabeth Dominick
Heaven on earth Chocs Judgement Arushaone Erickb52