Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,186
- 7,492
Mh. Rais mama samia anaamini kwamba wawekezaji wakija kwa wingi nchini watachangia ukuaji wa uchumi kwa kasi ambapo kwa sasa kinachowakwamisha ni complications zisizo na ulazima, kodi zisizo rafiki na vibali vya kazi kwa wawekezaji.
Kuna watu wanajenga hoja kwamba mtizamo huu wa Mh.Rais utaikosesha nchi mapato na pia utoaji wa vibali vya kazi kwa wageni/ wawekezaji utaathiri ajira za wenyeji.
Naomba kujibu hoja hizi kulingana na ufahamu wangu na wengine wanaweza kuongezea.
Kuhusu kodi
1. Kampuni za kigeni zikiwekewa mazingira rafiki ya kuwekeza nchini, hata kama hazitozwi kodi kubwa katika hatua za awali, kutokana na operesheni zake, hatimaye kuna kodi za aina mbalimbali zitakuja kulipwa.
Kwa mfano, kampuni itaajiri watu kibao, watalipa PAYE, bidhaa zinazozalishwa zitalipiwa VAT, wafanyakazi wa kampuni watakuwa wanapata kipato ambapo watafanya manunuzi ya bidhaaa ambapo watakuwa wanalipa kodi kupitia manunuzi na.k
Hivyo hii itasaidia kukusanya kodi kidogo kidogo lakini kutoka kwenye vyanzo vingi hivyo kuwa na win win situation.
2. Wawekezaji wakiwa wengi kutakuwa na 'economic diversification' na hii itakuwa na positive multiple effects kwenye uchumi wetu.
3. Makampuni yatakayowekeza nchini yatauza bidhaa kwenye nchi nyingine pia, kwa hiyo watu watakuja hapa nchini kununua bidhaa wapeleke kwao. Kwa mfano makampuni ya china ya simu, magari na.k yakiwekeza tanzania yatauza africa nzima, hivyo badala ya wafanyabiashara wa kiafrika kwenda guanzhou, watajaa Tanzania na watalala kwenye mahoteli yetu na kununua matikiti yetu ya mkuranga. Tunapata pesa na kodi.
4. Watanzania kujifunza kutoka kwa wawekezaji. Haya makampuni yakija kwa wingi, tutapata fursa ya kujifunza teknologia n.k. wadogo zetu hawatahangaika sana kuzunguka kutafuta field atachement na lile tatizo la kuwa na na engineers wasioweza kutengeneza chochote kotokana na kusoma theories tu litapungua.
Kuhusu ajira.
1. Makampuni haya hayataajiri wageni tu bali pia wenyeji hasa kwenye nafasi za kazi za jumla kama uhasibu, manunuzi, utawala. Na.k top management pekee ndio watakuwa wenye kampuni au waliochaguliwa na wenye kampuni.
Hili ni muhimu kwa sababu zifuatazo
1. Hakuna mwekezaji yoyote makini anayeweza kukubali kumkabidhi kampuni mtu asiyemjua awe ndio mfanya maamuzi kwa mtaji wa mabilioni. Hata kama ni wewe huwezi kufanya hiyo labda kama una bet mtaji.
2. Waafrica wengi tuna kosa baadhi ya skills za msingi kwenye maeneo flani. Kwa mfano kwenye electronics, ukweli bado tuko nyuma sana na tuliwahi kuyauliza makampuni kadhaa ya electronics kwamba kwa nini wasiwekeze afrika kwa kuwa kuna soko kubwa? Jibu lilikuwa kwamba africa hakuna raslimaliwatu yenye skills nzuri kwenye electeonics na hawaruhusu wachina kuwekeza na kufanya wenyewe kwenye maeneo hayo.
3. Changamoto ya uaminifu. Moja ya shida kubwa inayotukabili wa Tanzania ni suala la uaminifu. Ni rahisi sana kupata mtu mwenye elimu, lakini kupata watu wa aminifu si jambo la kitoto. Kama huamini wekeza pesa mahali halafu weka mbongo azisimamie halafu ulete mrejesho. Kwa hiyo ni vigumu kumlazimisha mwekezaji kuweka meneja asiyemjua vizuri. Hata hivyo kwenye eneo hili bado tunayo fursa ya kujifanyia self improvement na kufanya vizuri.
Kwa ujumla kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji nchini kama alivyosema mh. Rais Samia kuna faida kwa pande zote na tunahitaji wawekezaji kuliko wanavyotuhitaji.
N.b: Mada hii inazungumzia wawekezaji toka nje.
===========
UPDATE
==========
Leo tarehe 2I/04/2021, Mh. Rais Mama Samia amekutana na wafanyabiashara kutoka China ambao wameahidi kuwekeza Tanzania kupitia Kampuni zao zaidi ya 800. Kulingana na taarifa iliyotolewa, wanakusudia kuwekeza kwenye viwanda vya Magari, Simu, Madawa n.k
Ni hatua nzuri sana ambayo itasaidia kukuwa kwa uchumi wetu na kutengeneza ajira nyingi kwa vijana. Tumuungeni mkono na Mungu atubariki sote.