Watu wanachukulia jumla jumla kuwa uwekezaji unaongeza ajira, lakini ukweli ni kuwa uwekezaji unaweza kusababisha ajira zipotee tena kwa maelfu. Ajira inaweza kuwa ya mshahara au ya kujiajiri mwenyewe. Sasa kama umejiajiri kihalali halafu kutokana na sera za serikali unalazimishwa kuachana na shughuli uliyokuwa umejiajiri, hapo uwekezaji huo na balaa. Huko vijijini mamilioni ya wakulima wamenyang’anywa ardhi zao ili tu kupisha hao wanaoitwa wawekezaji huku wakulima hao wakikejeliwa kuwa hawazalishi kwa tija na kuwa wawekezaji hao watawaajili. Binafsi nimebahatika kuzunguka sana maeneo ya vijijini kutokana na kazi niliyokuwa naifanya. Niliwahi kufika wilaya moja nikamkuta mtu ambaye alikuwa na ekari kumi na mbili, yeye alikopa power tiller Mfuko wa pembejeo (AGTIF) kwa lengo la kulima mpunga katika shamba lake hilo, wakati huo huo aliletwa mwekezaji tena toka nje ya nchi akapewa ardhi katika kata hiyo ilia alime mpunga, kilichofanyika ni kuwa mamlaka zilichukua ardhi ya wakulima wadogo wadogo katika vijiji vinavyomzunguka mwekezaji huo na kuunganisha ili kumpatia eneo la kutosha mwekezaji huo, hivyo kupelekea wananchi hao kukosa ardhi ya kulima akiwemo huyo aliyepoteza hekta 12. Sasa fikiria huo mkopo aliochukua AGTIF aliulipaje wakati tayari shamba alilotaka kuzalishia ambalo ni mali yake amenyang’anywa? Yaani uwanyang’anye ardhi wazawa na kuwafanya manamba katika ardhi yao hiyo hiyo! Ukienda njia ya Rufiji, utaona kuna mapori mengi sana kuzunhguka vijiji na unaweza kuzani kuwa kuna ardhi kubwa sana ya kulima, lakini ukweli ni kuwa ardhi yote hiyo wamepewa hao wanaoitwa wawekezaji na ardhi hiyo hata kuilima hawailimi lakini wakati huo huo wanavijiji waliokuwa wanaimiliki ardhi hiyo wanasumbuka kwa kukosa ardhi ya kulima. Huko nyuma kabla RUBADA haijavunjwa na JPM ilikuwa ndio Karl Peters wa Tanzania katika kunyang’anya ardhi na kuidalalia. Malaki ya hekta zimeondolewa mikononi mwa wakulima na kupewa wajanja kwa mgongo wa uwekezaji, Tena huko nyuma kuna watu walikuwa wanakuja bila hata senti tano lakini baada ya kupewa ardhi wanachukua hati wanaenda benki tena za ndani ya nchi na kukopa mamilioni ya pesa na kufanyia biashara zingine kama uagizaji wa mafuta.
Unalalamika kuwa wamachinga wamezidi, umachinga ,mwingine ni matokeo ya watu kupoteza ardhi zao sasa inabidi wafanye uchuuzi, bodaboda, umalaya, mama ntilie (sio kama nadharau kazi hizo la hasha) kwa sababu hizo sekta hazijai zinampokea yeyote anayekuja kujiunga nazo ingawa soko linakuwa halipanuki.
Pia watu wanasema wakati wa JK kulikuwa na pesa mtaani lakini hawajiulizi kuwa zilikuwa pesa halali? Wizi, ufisadi na ubadhirifu wa pesa za umma na uuzaji wa madawa ya kulevya ulichangia katika ukuaji uchumi, hivyo uchumi wa wakati huo haukuwa halisi. Wewe inaweza kuwa hukuwa unaiba lakini manufaa ya wizi yalikufikia kupitia mnyororo wa wizi. Mathalani afisa au mfanyabiashara akishahomola atakuja mtaani kwako na kukupa kazi ya kumjengea au utamuuzia nguo bei juu au atawahonga nyumba zake ndogo mamilioni hivyo watu wengine kunufaika kama vile saluni za urembo nk. Lakini vile vile kulikuwa na watu kibao wanaumia kwa kukosa dawa, pensheni, na huduma zingine sababu sehemu kubwa ya pesa imeibwa. Kwa sasa hata mambo yakilegezwa vipi pesa haziwezi kurudi kama wakati wa JK unless wizi/ufisadi urudi upya kwa kasi. Kuna afisa mmoja wa kawaida kabisa asiye na cheo ilikuwa kila mwisho wa wiki lazima aende kwa ndege kwao Mwanza na kurudi jumapili au jumatatu asubuhi ila wakati wa JPM alikuwa haendi licha ya kuwa kazi yake haikubadilika.
Kiwango cha ukopaji hakiwezi kulingana kwa kila Rais aliyetawala, lakini ni wazi marais wote watano walikopa ila JPM alipoingia alikuta deni kubwa tayari, ukopaji wake haukusababisha deni liwe kubwa, na hayo madeni ya nyuma yanaongezeka riba, hivyo unaweza kuona deni limeongezeka wakati wa JPM lakini sehemu kubwa ya ongezeko hilo ni riba za nyuma kuliko deni jipya. Ukitaka kukosoa hili chukua data kila Rais aliyeingia madarakani alikuta deni shilingi ngapi na alipoondoka aliacha shilingi ngapi.
Watu wamevamia mjadala na wakati hawaelewi undani wa mambo na vilevile chuki binafsi dhidi ya JPM.