Maono ya Rais mama Samia kuhusu uwekezaji nchini kwenye nyuzi 360

Asante sana kwa bandiko zuri, umeongea uhalisia kabisa.
Ni heri kuwa na taxbase kubwa ambayo inakuwa charged fair Tax kulikokuwa na taxbase ndogo na kuitax unrealistic taxes.
Uko sahihi sana mkuu. Ukikusanya mfano tsh. 100 kwa wawekezaji 1000 unakuwa unepata pesa kuliko ukikusanya 1000 kwa wawekezaji 10 halafu pengine 5 wakakimbia, halafu na zile faida nyingine nyingine pia unakosa.

Mfano ukifuga ng'ombe wa maziwa, pamoja na kuwa lengo kubwa ni maziwa, lakini ukimtunza pia unapata samadi na baadae nyama na ngozi. Sasa ukitaka kukwepa gharama za matunzo na kuforce upate maziwa ndio tatu kwa siku ng'ombe akafa, then ndio nini sasa? Kwa hiyo kinachotakiwa ni win win. Mwekezaji apate na nchi tupate pia. Win win. Kwa hiyo mwelekeo unatia moyo sana
 
Mh. Rais mama samia anaamini kwamba wawekezaji wakija kwa wingi nchini watachangia ukuaji wa uchumi kwa kasi ambapo kwa sasa kinachowakwamisha ni complications zisizo na ulazima, kodi zisizo rafiki na vibali vya kazi kwa wawekezaji.

Kuna watu wanajenga hoja kwamba mtizamo huu wa Mh.Rais utaikosesha nchi mapato na pia utoaji wa vibali vya kazi kwa wageni/ wawekezaji utaathiri ajira za wenyeji.

Naomba kujibu hoja hizi kulingana na ufahamu wangu na wengine wanaweza kuongezea.

Kuhusu kodi
1. Kampuni za kigeni zikiwekewa mazingira rafiki ya kuwekeza nchini, hata kama hazitozwi kodi kubwa katika hatua za awali, kutokana na operesheni zake, hatimaye kuna kodi za aina mbalimbali zitakuja kulipwa.

Kwa mfano, kampuni itaajiri watu kibao, watalipa PAYE, bidhaa zinazozalishwa zitalipiwa VAT, wafanyakazi wa kampuni watakuwa wanapata kipato ambapo watafanya manunuzi ya bidhaaa ambapo watakuwa wanalipa kodi kupitia manunuzi na.k

Hivyo hii itasaidia kukusanya kodi kidogo kidogo lakini kutoka kwenye vyanzo vingi hivyo kuwa na win win situation.

2. Wawekezaji wakiwa wengi kutakuwa na 'economic diversification' na hii itakuwa na positive multiple effects kwenye uchumi wetu.

3. Makampuni yatakayowekeza nchini yatauza bidhaa kwenye nchi nyingine pia, kwa hiyo watu watakuja hapa nchini kununua bidhaa wapeleke kwao. Kwa mfano makampuni ya china ya simu, magari na.k yakiwekeza tanzania yatauza africa nzima, hivyo badala ya wafanyabiashara wa kiafrika kwenda guanzhou, watajaa Tanzania na watalala kwenye mahoteli yetu na kununua matikiti yetu ya mkuranga. Tunapata pesa na kodi.

4. Watanzania kujifunza kutoka kwa wawekezaji. Haya makampuni yakija kwa wingi, tutapata fursa ya kujifunza teknologia n.k. wadogo zetu hawatahangaika sana kuzunguka kutafuta field atachement na lile tatizo la kuwa na na engineers wasioweza kutengeneza chochote kotokana na kusoma theories tu litapungua.

Kuhusu ajira.

1. Makampuni haya hayataajiri wageni tu bali pia wenyeji hasa kwenye nafasi za kazi za jumla kama uhasibu, manunuzi, utawala. Na.k top management pekee ndio watakuwa wenye kampuni au waliochaguliwa na wenye kampuni.

Hili ni muhimu kwa sababu zifuatazo

1. Hakuna mwekezaji yoyote makini anayeweza kukubali kumkabidhi kampuni mtu asiyemjua awe ndio mfanya maamuzi kwa mtaji wa mabilioni. Hata kama ni wewe huwezi kufanya hiyo labda kama una bet mtaji.

2. Waafrica wengi tuna kosa baadhi ya skills za msingi kwenye maeneo flani. Kwa mfano kwenye electronics, ukweli bado tuko nyuma sana na tuliwahi kuyauliza makampuni kadhaa ya electronics kwamba kwa nini wasiwekeze afrika kwa kuwa kuna soko kubwa? Jibu lilikuwa kwamba africa hakuna raslimaliwatu yenye skills nzuri kwenye electeonics na hawaruhusu wachina kuwekeza na kufanya wenyewe kwenye maeneo hayo.

3. Changamoto ya uaminifu. Moja ya shida kubwa inayotukabili wa Tanzania ni suala la uaminifu. Ni rahisi sana kupata mtu mwenye elimu, lakini kupata watu wa aminifu si jambo la kitoto. Kama huamini wekeza pesa mahali halafu weka mbongo azisimamie halafu ulete mrejesho. Kwa hiyo ni vigumu kumlazimisha mwekezaji kuweka meneja asiyemjua vizuri. Hata hivyo kwenye eneo hili bado tunayo fursa ya kujifanyia self improvement na kufanya vizuri.

Kwa ujumla kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji nchini kama alivyosema mh. Rais Samia kuna faida kwa pande zote na tunahitaji wawekezaji kuliko wanavyotuhitaji.

N.b: Mada hii inazungumzia wawekezaji toka nje.

Uzi wenye mchango mzuri, sina shaka na ulichoandika kwenye uzi huu.
 
Wakati wa JK huo si ndio ujinga uliokuwa unafanyika na kodi ilikuwa ni 800bn kwa mwezi wastani, SSH hana maoni, kodi lazima ikusanye kwa sheria kama anaona kodi ni kubwa abadilishe sheria, vinginevyo anatengeneza mazingira ya wafanyabiashara kukataa kulipa kodi halali kabisa.

Acha upotoshaji usio na tija yoyote. Wakati wa Magufuli kilikuwa na upikwaji mkubwa wa data kiasi huwezi kujua kwa uhakika kodi yake ilikuwa ngapi. Pia kodi za halmashauri ziko kwenye mfuko mkuu, hivyo figure inaweza kuwa kubwa sasa, na sio lazima iwe makusanyo makubwa. Kama mwezi Desemba mwaka jana Magufuli alisema ATCL imeingiza faida ya 28b, wakati ripoti ya CAG juzi imeonyesha tofauti, hapo unaamini nini?
 
Uzi wenye mchango mzuri, sina shaka na ulichoandika kwenye uzi huu.
Shukuran mkuu. Tumuunge mkono mama pale anapofanya vizuri ili hata pale patakapokuwa na kasoro wadau wakishauri iwe ni rahisi kuchukukuliwa serious.

Ikumbukwe hata kiongozi awe mzuri na awe na nia nzuri kiasi gani, kama hataata support ya kutosha kutoka kwa waliomzunguka na anaowaongoza, hawezi kufanikiwa sana, kwa hiyo ni jukumu la watu wema wanapoona kuna jambo jema linafanyika au linataka kufanyika wasaidie kuongezea nguvu kulingana na mazingira na uwezo wa kila mmoja.
 
Asante sana kwa bandiko zuri, umeongea uhalisia kabisa.
Ni heri kuwa na taxbase kubwa ambayo inakuwa charged fair Tax kulikokuwa na taxbase ndogo na kuitax unrealistic taxes.
Mawazo chanya kama haya ndiyo yawe yaruhusiwa huku kwa jukwaa.
 
Mh. Rais mama samia anaamini kwamba wawekezaji wakija kwa wingi nchini watachangia ukuaji wa uchumi kwa kasi ambapo kwa sasa kinachowakwamisha ni complications zisizo na ulazima, kodi zisizo rafiki na vibali vya kazi kwa wawekezaji.

Kuna watu wanajenga hoja kwamba mtizamo huu wa Mh.Rais utaikosesha nchi mapato na pia utoaji wa vibali vya kazi kwa wageni/ wawekezaji utaathiri ajira za wenyeji.

Naomba kujibu hoja hizi kulingana na ufahamu wangu na wengine wanaweza kuongezea.

Kuhusu kodi
1. Kampuni za kigeni zikiwekewa mazingira rafiki ya kuwekeza nchini, hata kama hazitozwi kodi kubwa katika hatua za awali, kutokana na operesheni zake, hatimaye kuna kodi za aina mbalimbali zitakuja kulipwa.

Kwa mfano, kampuni itaajiri watu kibao, watalipa PAYE, bidhaa zinazozalishwa zitalipiwa VAT, wafanyakazi wa kampuni watakuwa wanapata kipato ambapo watafanya manunuzi ya bidhaaa ambapo watakuwa wanalipa kodi kupitia manunuzi na.k

Hivyo hii itasaidia kukusanya kodi kidogo kidogo lakini kutoka kwenye vyanzo vingi hivyo kuwa na win win situation.

2. Wawekezaji wakiwa wengi kutakuwa na 'economic diversification' na hii itakuwa na positive multiple effects kwenye uchumi wetu.

3. Makampuni yatakayowekeza nchini yatauza bidhaa kwenye nchi nyingine pia, kwa hiyo watu watakuja hapa nchini kununua bidhaa wapeleke kwao. Kwa mfano makampuni ya china ya simu, magari na.k yakiwekeza tanzania yatauza africa nzima, hivyo badala ya wafanyabiashara wa kiafrika kwenda guanzhou, watajaa Tanzania na watalala kwenye mahoteli yetu na kununua matikiti yetu ya mkuranga. Tunapata pesa na kodi.

4. Watanzania kujifunza kutoka kwa wawekezaji. Haya makampuni yakija kwa wingi, tutapata fursa ya kujifunza teknologia n.k. wadogo zetu hawatahangaika sana kuzunguka kutafuta field atachement na lile tatizo la kuwa na na engineers wasioweza kutengeneza chochote kotokana na kusoma theories tu litapungua.

Kuhusu ajira.

1. Makampuni haya hayataajiri wageni tu bali pia wenyeji hasa kwenye nafasi za kazi za jumla kama uhasibu, manunuzi, utawala. Na.k top management pekee ndio watakuwa wenye kampuni au waliochaguliwa na wenye kampuni.

Hili ni muhimu kwa sababu zifuatazo

1. Hakuna mwekezaji yoyote makini anayeweza kukubali kumkabidhi kampuni mtu asiyemjua awe ndio mfanya maamuzi kwa mtaji wa mabilioni. Hata kama ni wewe huwezi kufanya hiyo labda kama una bet mtaji.

2. Waafrica wengi tuna kosa baadhi ya skills za msingi kwenye maeneo flani. Kwa mfano kwenye electronics, ukweli bado tuko nyuma sana na tuliwahi kuyauliza makampuni kadhaa ya electronics kwamba kwa nini wasiwekeze afrika kwa kuwa kuna soko kubwa? Jibu lilikuwa kwamba africa hakuna raslimaliwatu yenye skills nzuri kwenye electeonics na hawaruhusu wachina kuwekeza na kufanya wenyewe kwenye maeneo hayo.

3. Changamoto ya uaminifu. Moja ya shida kubwa inayotukabili wa Tanzania ni suala la uaminifu. Ni rahisi sana kupata mtu mwenye elimu, lakini kupata watu wa aminifu si jambo la kitoto. Kama huamini wekeza pesa mahali halafu weka mbongo azisimamie halafu ulete mrejesho. Kwa hiyo ni vigumu kumlazimisha mwekezaji kuweka meneja asiyemjua vizuri. Hata hivyo kwenye eneo hili bado tunayo fursa ya kujifanyia self improvement na kufanya vizuri.

Kwa ujumla kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji nchini kama alivyosema mh. Rais Samia kuna faida kwa pande zote na tunahitaji wawekezaji kuliko wanavyotuhitaji.

N.b: Mada hii inazungumzia wawekezaji toka nje.
Chawa mnakazi sana kuji-adjust na mwelekeo mpya wa nchi
 
Shukuran mkuu. Tumuunge mkono mama pale anapofanya vizuri ili hata pale patakapokuwa na kasoro wadau wakishauri iwe ni rahisi kuchukukuliwa serious.

Ikumbukwe hata kiongozi awe mzuri na awe na nia nzuri kiasi gani, kama hataata support ya kutosha kutoka kwa waliomzunguka na anaowaongoza, hawezi kufanikiwa sana, kwa hiyo ni jukumu la watu wema wanapoona kuna jambo jema linafanyika au linataka kufanyika wasaidie kuongezea nguvu kulingana na mazingira na uwezo wa kila mmoja.

Kwa huu mwanzo wa mama tunamuunga mkono, japo tunajua yeye ni zao la wizi wa kura. Kimsingi nampa siku 100 ili kumpa tathmini ya haki ya awali. Lakini so far mama tunamuunga mkono ili afanye vyema zaidi.
 
Chawa mnakazi sana kuji-adjust na mwelekeo mpya wa nchi
Mkuu tumerudi tena kwenye nchi ya hoja kwa hoja. Kwa mkuu anayedhani ana hoja au ushuauri wa maana huu ndio wakati. Ambaye hatutumia wakati huu huenda asipate tena fursa ya kutoa hoja yake kwa ufasaha katika kipindi fulani na kubaki kulia lia.
 
Mh. Rais mama samia anaamini kwamba wawekezaji wakija kwa wingi nchini watachangia ukuaji wa uchumi kwa kasi ambapo kwa sasa kinachowakwamisha ni complications zisizo na ulazima, kodi zisizo rafiki na vibali vya kazi kwa wawekezaji.

Kuna watu wanajenga hoja kwamba mtizamo huu wa Mh.Rais utaikosesha nchi mapato na pia utoaji wa vibali vya kazi kwa wageni/ wawekezaji utaathiri ajira za wenyeji.

Naomba kujibu hoja hizi kulingana na ufahamu wangu na wengine wanaweza kuongezea.

Kuhusu kodi
1. Kampuni za kigeni zikiwekewa mazingira rafiki ya kuwekeza nchini, hata kama hazitozwi kodi kubwa katika hatua za awali, kutokana na operesheni zake, hatimaye kuna kodi za aina mbalimbali zitakuja kulipwa.

Kwa mfano, kampuni itaajiri watu kibao, watalipa PAYE, bidhaa zinazozalishwa zitalipiwa VAT, wafanyakazi wa kampuni watakuwa wanapata kipato ambapo watafanya manunuzi ya bidhaaa ambapo watakuwa wanalipa kodi kupitia manunuzi na.k

Hivyo hii itasaidia kukusanya kodi kidogo kidogo lakini kutoka kwenye vyanzo vingi hivyo kuwa na win win situation.

2. Wawekezaji wakiwa wengi kutakuwa na 'economic diversification' na hii itakuwa na positive multiple effects kwenye uchumi wetu.

3. Makampuni yatakayowekeza nchini yatauza bidhaa kwenye nchi nyingine pia, kwa hiyo watu watakuja hapa nchini kununua bidhaa wapeleke kwao. Kwa mfano makampuni ya china ya simu, magari na.k yakiwekeza tanzania yatauza africa nzima, hivyo badala ya wafanyabiashara wa kiafrika kwenda guanzhou, watajaa Tanzania na watalala kwenye mahoteli yetu na kununua matikiti yetu ya mkuranga. Tunapata pesa na kodi.

4. Watanzania kujifunza kutoka kwa wawekezaji. Haya makampuni yakija kwa wingi, tutapata fursa ya kujifunza teknologia n.k. wadogo zetu hawatahangaika sana kuzunguka kutafuta field atachement na lile tatizo la kuwa na na engineers wasioweza kutengeneza chochote kotokana na kusoma theories tu litapungua.

Kuhusu ajira.

1. Makampuni haya hayataajiri wageni tu bali pia wenyeji hasa kwenye nafasi za kazi za jumla kama uhasibu, manunuzi, utawala. Na.k top management pekee ndio watakuwa wenye kampuni au waliochaguliwa na wenye kampuni.

Hili ni muhimu kwa sababu zifuatazo

1. Hakuna mwekezaji yoyote makini anayeweza kukubali kumkabidhi kampuni mtu asiyemjua awe ndio mfanya maamuzi kwa mtaji wa mabilioni. Hata kama ni wewe huwezi kufanya hiyo labda kama una bet mtaji.

2. Waafrica wengi tuna kosa baadhi ya skills za msingi kwenye maeneo flani. Kwa mfano kwenye electronics, ukweli bado tuko nyuma sana na tuliwahi kuyauliza makampuni kadhaa ya electronics kwamba kwa nini wasiwekeze afrika kwa kuwa kuna soko kubwa? Jibu lilikuwa kwamba africa hakuna raslimaliwatu yenye skills nzuri kwenye electeonics na hawaruhusu wachina kuwekeza na kufanya wenyewe kwenye maeneo hayo.

3. Changamoto ya uaminifu. Moja ya shida kubwa inayotukabili wa Tanzania ni suala la uaminifu. Ni rahisi sana kupata mtu mwenye elimu, lakini kupata watu wa aminifu si jambo la kitoto. Kama huamini wekeza pesa mahali halafu weka mbongo azisimamie halafu ulete mrejesho. Kwa hiyo ni vigumu kumlazimisha mwekezaji kuweka meneja asiyemjua vizuri. Hata hivyo kwenye eneo hili bado tunayo fursa ya kujifanyia self improvement na kufanya vizuri.

Kwa ujumla kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji nchini kama alivyosema mh. Rais Samia kuna faida kwa pande zote na tunahitaji wawekezaji kuliko wanavyotuhitaji.

N.b: Mada hii inazungumzia wawekezaji toka nje.
Nami naona nichangie kuhusu hizo hoja zako:

Suala la makampuni toka nje kuja kuwekeza ndani ya nchi halitokani na kuangalia jambo moja bali mambo kadhaa.

Mosi umedai kuwa kampuni zikiwekewa mazingira ya kutolipa kodi bado kuna faida nchi itapata, Uamuzi huo unaweza kuua kampuni zingine ambazo ni za wazalendo au za nje lakini ziliingia awali na tayari zinafanya kazi katika sub sector hiyo hiyo ambayo kampuni mpya toka nje inasamehewa kodi. Kumbuka kama kampuni mbili zote zinauza katika soko hilo hilo lakini mmoja halipi kodi na mwingine analipa kodi maana yake mmoja atauza ghali na mwingine atauza kwa bei rahisi hivyo kuondoa ushindani halali na kupelekea kampuni inayolipa kodi kufa au kushindwa kupanua shughuli zake. Hii itasababisha serikali ikose kodi toka makampuni yaliyokuwepo awali ( VAT, income tax, corporate tax nk.), ajira katika makampuni hayo kupotea. Mfano hai ni Dangote yeye alipewa tax concessions nyingi ambazo viwanda vingine vya cement kama twiga, Tanga na Mbeya havikupewa hivyo kuviathiri sana viwanda hivyo. Concession yeyote inatakiwa itolewe kwa sub sector nzima sio kumpoendelea mwekezaji mmoja.

Pili, Economic diversification unayodai itakuwepo inaweza isiwepo kama ilivyokuwepo awali katika sub sector hiyo hiyo kutegemeana ujio wa kampuni mpya umepunguza kiasi gani kampuni zilizokuwepo awali. Mfano katika biashara ya daladala kama wakiondolewa wote akapewa mwekezaji mmoja tu kama jinsi BRT ilivyokuwa inaelekea maana yake wenye daladala wapatao elfu tatu wanaondolewa na kipato kinachogusa familia zao wanaofikia elfu kumi na nane (chukulia familia ina watu 6) kitapotea, ada za watoto elfu 12 zitakosekana (familia moja watoto 4), school uniforms za watoto zitapotea nk.

Tatu, umedai makampuni yatauza nje Africa nzima hivyo tutapata pesa nchi kupitia multiplier effect; sio kweli kabisa. Elewa katika suala zima la uwekezaji yaani foreign direct investments (FDI) kuna uwekezaji wa aina mbili hivi: Kuna wale wanaotarget soko la ndani ya nchi ambao ndio wengi zaidi; wuwekezaji wa aina hiyo ndio huo athari zake nimezitaja hapo juu. Aina ya pili ya uekezaji ni Platform seeking FDIs ambao ndio hao unaodai wewe kuwa watawekeza na kuuza Africa nzima. Aina hii ya pili ni ngumu kuipata katika mazingira yetu kwa sababu wawekezaji hao wanaangalia mambo mengi na sio sula la kodi tu. Mfano anajua kuwa kutokana na kuwa na jumuiya za kiuchumi kama EAC na SADC kama akiwekeza katika nchi yeyote kati ya hizo atakuwa na access ya kuuza bidhaa zake katika nchi zote wanachama wa umoja huo mithili ya mtu anayezalisha bidhaa Dodoma anavyoweza kuuza Tanzania nzzima. Hivyo kabla ya kuchagua awekeze nchi gani kwa ajili ya soko hilo tajwa ataangalia vigezo vingi kama miundombinu iliyopo (barabara za uhakika,, reli, bandari, umeme, mawasiliano ya simu, intenet); utulivu wa kisiasa, kama kuna wafanyakazi wenye ujuzi (skilled labour) predictability of taxes regimes, gharama za kuzalisha/kufanya biashara, mfano kama unit moja ya umeme kwako ni ghali kuliko Kenya au Africa Kusini ina maana akizalishia hicho kitu hapa anaweza kushindwa kukiuza nje maana kuna kampuni nyingine inaweza kuwekeza kule Kenya kwenye gharama nafuu za kufanya biashara hivyp kumfanya ashiundwe kushindana katika soko la EAC au SADC. Hivyo ndugu yangu kama ni mfuatiliaji mzuri wa haya mambo ya kiuchumi utaona wazi ni rahisi kwa mwekezaji anayetarget soko la SADC kuwekeza Africa kusini au yule anayetarget soko la EAC kuwekeza Kenya kuliko Tanzania. Nchi ikiwa siyo compitetive kwa vigezo nilivyovitaja basi mwekezaji inayoweza kumpata ni katika extraction sector kama vile madini, gesi na mafuta. Na hapo msipokuwa makini ndipo mnalizwa kama tulivyoshuhudia mikataba mibovu ya madini iliyoingiwa na serikali ya awamu ya nne.

Nne, Kwa kuwa sio rahisi kupata platform seeking FDIs, tunaoweza kuwapata ni wachimbaji madini, mafuta na gesi basi tunaweza tusifaidike na rasilimali zetu tusipokuwa makini. Lakini pia tutapata wawekezaji wa soko la ndani ambao watazalisha bidhaa zao na kuuza kwa shilingi lakini mwisho wa siku baada ya kupata faida watataka kuhamisha faida yao nje ya nchi. Hapo ndipo mtanange unapokuja kuwa itabidi pesa ya kigeni tuliyopata kwa kuuza korosho, pamba, kahawa ndio tuwaruhusu wachenji faida yao na kuondosha nchini. Hii inasababisha kuwepo na high demand ya pesa za kigeni kwa sababu kumbuka tunazihitaji pesa za kigeni kwa ajili ya kununulia madawa, mafuta na vitu vingine muhimu. Hivyo inaweza kupelekea shilingi kushuka thamani. Soko la ndani ni vizuri wawekezaji wa ndani wakadominate kwani wao fedha ya kigeni wanayohitaji ni ya kununulia mashine na labda malighafi na sio profit repatriations

Hata hivyo nakupongeza umechambua critically, debate za namna hii ni nzuri.
 
Sio kila mwekezaji ni genuine ,

Wengine ni janja janja tu, wanakuja kwa malengo yaliyojificha moja wapo ikiwa kupata ardhi yetu ili wachukulie mikopo kwenye mabenki yao huko nje na kuendelea na mambo mengine

Tusipokua makini tunaweza kuta sehemu kubwa ya ardhi yetu ipo rehani kwenye mabenki ya nje hiyo ni threat kwa national security.
Hiki ni kitu cha kuzingatia kwenye hii sera lkn haimaanishi tuache kuvutia wawekezaji
 
Wakati wa JK huo si ndio ujinga uliokuwa unafanyika na kodi ilikuwa ni 800bn kwa mwezi wastani, SSH hana maoni, kodi lazima ikusanye kwa sheria kama anaona kodi ni kubwa abadilishe sheria, vinginevyo anatengeneza mazingira ya wafanyabiashara kukataa kulipa kodi halali kabisa.
Mkuu wewe unafanya shughuli gani?
 
Mkuu RMC hakuna mahali nimesema kampuni zisilipe kodi, wala hamna mtu anayesema hivyo. Kwani kwa nini wasilipe? Ni vizuri kuelewa muktadha wa hoja, vinginevyo tunaweza kupotosha hoja kwa makusudi au kwa bahati mbaya.
 
Angalia na. 1 katika maelezo yako umeandika: hata kama hazitozwi kodi kubwa....
Hii maana yake ni kupunguziwa kodi na inaweza kuwa hata 0 percent. Kumbuka kuna kampuni katika sub sector hiyo hiyo zinalipa fully. Ndio maana nikasena concession yeyote ile inatakiwa kugusa makampuni yote katika sub sector hiyo.
 
Kodi kubwa, kupunguza kodi, na O kodi ni vitu vitatu tofauti kabisa mkuu. Ni sawa na mtu akuambie usile chumvi nyingi sana kwa wakati mmoja, halafu wewe useme ' sana nisipokula chumvi kabisa........' Unakuwa umehama kabisa kwenye mantiki na hivyo hoja zote unazojenga baada ya hapo zinakuwa zimesha divert kwenye hoja ya msingi.

Halafu pia sijakuelewa vizuri, kwa nini unadhani kwamba katika muktadha wa hoja ya msingi, wengine watalipishwa kodi wengine hawatalipa? Yaani kwa nini unawaza hivyo?

Halafu kuhusu hoja kuwa uwekezaji huvutiwa na vitu vingi, sio kitu kimoja upo sahihi kabisa. Ila si tumesema tanzania kuna mazingira mazuri ya uwekezaji isipokuwa mifumo michache tu ndio inatukwamisha? Anyway! Nakubaliana na wewe kwamba inawezekana pia kuna mambo mengine ya kuboresha vile vile, basi ndio tuyaseme sasa na kwamba yanaboreshwaje!

Tusikate tamaa kiujumla jumla tu hivyo. Mimi naamini tunaweza kushawishi MNC's kuwekeza Tz na bidhaa zikauzwa Africa nzima kutokea hapa.
 
Mfano china pamoja na mafanikio makubwa waliyonayo kiuchumi, wamekuwa wakiyavutia makampuni ya nje na hasa marekani kuwekeza kwa kasi china. Mfano kwenye mji wa shanghai na shenzhen kumejaa makampuni ya electronics ya marekani. Na makampuni hayo yamechangia pakubwa kukuza uchumi wa china na kutengeneza ajira za kutosha.

Kwa hiyo nadhani sasa tunaenda kwenye muelekeo mzuri sana kisera ambapo karibuni tunaweza kupata mafanikio ya kutia moyo.
Masahihisho tu kidogo kwenye andiko lako kuu...

Kwamba, pamoja na kuwa tunazungumza sana juu wawekezaji toka nje, lakini tusisahau kuwa ni muhimu sisi kama nchi kupitia serikali yetu, tuka encourage wazawa pia kuwekeza hapa nchini. Ni kwa kupitia wazawa hawa wanaweza kutengeneza Investment partnership na wawekezaji toka nchi za zingine..

Tatizo moja lilikuja na kukua kwa kasi huku likishashadiwa na aliyekuwa kiongozi mkuu wa nchi ni kutengeneza investment uncertainty kwa nchi kutokutabirika ktk misimamo na maamuzi yake. Hii ni sumu kwa investor yeyote kuwekeza ktk nchi ya namna hii...

¶ Kuhusu maoni yangu ya jumla kwa mjadala huu, naweza kusema haya;

1. Kwamba, binafsi najaribu sana kufikiri na kujiuliza swali hili, kuwa, hivi ni sababu gani za kisheria na kisera zinazofanya kiwanda mfano cha General Tyre - Arusha kushindwa kuamuka na kuanza uzalishaji tena?

Inawezekana sisi kama nchi tumeshindwa kutumia watu wetu na utaalamu wetu kukiendesha kiwanda hiki...

Sasa, je hakuna watu ingalau wenye uwezo kushawishi kampuni kubwa za nje za kutengeneza matairi kama KUMHO nk kukichukua kiwanda hiki na kuendeleza uzalishaji kwa manufaa ya nchi na watu wetu? Duuh, mimi hufikiri sana na sipati jibu na sanasana mwisho wa siku unaishia kusema tu kuwa ni ukosefu wa siasa safi na uongozi bora...!

2. Binafsi natamani sana kuona kampuni kubwa kama za kutengeneza vifaa vya ki - electronics kama simu,kompyuta, friji nk; magari, zinaingia nchini na kuanza kuwekeza..

Inashangaza sana sisi Tanzania uwekezaji mkubwa toka nje ktk kipindi cha Magufuli ni kwenye makampuni ya michezo ya ku - bet pekee. Hii ni aibu na hatari sana...!!
 
Kodi kubwa, kupunguza kodi, na O kodi ni vitu vitatu tofauti kabisa mkuu. Ni sawa na mtu akuambie usile chumvi nyingi sana kwa wakati mmoja, halafu wewe useme ' sana nisipokula chumvi kabisa........' Unakuwa umehama kabisa kwenye mantiki na hivyo hoja zote unazojenga baada ya hapo zinakuwa zimesha divert kwenye hoja ya msingi.

Halafu pia sijakuelewa vizuri, kwa nini unadhani kwamba katika muktadha wa hoja ya msingi, wengine watalipishwa kodi wengine hawatalipa? Yaani kwa nini unawaza hivyo?

Halafu kuhusu hoja kuwa uwekezaji huvutiwa na vitu vingi, sio kitu kimoja upo sahihi kabisa. Ila si tumesema tanzania kuna mazingira mazuri ya uwekezaji isipokuwa mifumo michache tu ndio inatukwamisha? Anyway! Nakubaliana na wewe kwamba inawezekana pia kuna mambo mengine ya kuboresha vile vile, basi ndio tuyaseme sasa na kwamba yanaboreshwaje!

Tusikate tamaa kiujumla jumla tu hivyo. Mimi naamini tunaweza kushawishi MNC's kuwekeza Tz na bidhaa zikauzwa Africa nzima kutokea hapa.
Kodi kubwa, kutolipa kodi na zero tax ni kitu hicho hicho ila rates ndio tofauti. Unapomwambia investor njoo lakini corporate tax utalipa 0 percent au machine zako za uzalishaji utalipa 0 percent import/ custom duty lakini katika sub sector hiyo hiyo kuna mzawa au kampuni ya nje iliingia zamani inalipa kodi hizo hapo ndio utofauti ninaousema. Ukitaka kuwa sawa unaweka level ground katika sub sector hiyo kusudiwa sio kufanya discrimination kwa kisingizio cha uwekezaji ndipo yale madhara niliyoyasema yanapojitokeza.

Pili kuhusu FDIs ni vizuri ukasoma kwanza nadharia za uchumi zilizopo kuhusu uwekezaji wa MNCs kwani hayo niliyoyasema yameandikwa sana. Sio suala la kushawishi tu kama unavyodhani.
 
Kwani wawekezaji wa nje kwa kawaida huuziwa ardhi?
Wanapewa derivative right of occupancy ambayo inatosha kuwa collateral ukizingatia kwamba muda unakua ni 33,66 na 99 years.

Hakuna anayekataa investors kuja nchini ila swala hapa ni kuwa tunawakaribisha vipi, ukizingatia kwamba kuna ulazima wa kulinda ajira za vijana wetu kwani tusipozilinda tutawafanya kuwa manamba kwenye nchi yao na elimu yao itakua haina faida, tutatengeneza kizazi ambacho kimekandamizwa kwa muda na siku wakichoka hapata kalika hapa.

Kodi ni tamu ndio ila tusifanye hivyo at the expence of our national security.
 
Ajira zipi sasa unazungumzia mkuu, maana bila sekta binafsi kukua hakuna ajira na hakuna ukuaji wa sekta binafsi bila uwekezaji.
 
Back
Top Bottom