Mh. Rais mama samia anaamini kwamba wawekezaji wakija kwa wingi nchini watachangia ukuaji wa uchumi kwa kasi ambapo kwa sasa kinachowakwamisha ni complications zisizo na ulazima, kodi zisizo rafiki na vibali vya kazi kwa wawekezaji.
Kuna watu wanajenga hoja kwamba mtizamo huu wa Mh.Rais utaikosesha nchi mapato na pia utoaji wa vibali vya kazi kwa wageni/ wawekezaji utaathiri ajira za wenyeji.
Naomba kujibu hoja hizi kulingana na ufahamu wangu na wengine wanaweza kuongezea.
Kuhusu kodi
1. Kampuni za kigeni zikiwekewa mazingira rafiki ya kuwekeza nchini, hata kama hazitozwi kodi kubwa katika hatua za awali, kutokana na operesheni zake, hatimaye kuna kodi za aina mbalimbali zitakuja kulipwa.
Kwa mfano, kampuni itaajiri watu kibao, watalipa PAYE, bidhaa zinazozalishwa zitalipiwa VAT, wafanyakazi wa kampuni watakuwa wanapata kipato ambapo watafanya manunuzi ya bidhaaa ambapo watakuwa wanalipa kodi kupitia manunuzi na.k
Hivyo hii itasaidia kukusanya kodi kidogo kidogo lakini kutoka kwenye vyanzo vingi hivyo kuwa na win win situation.
2. Wawekezaji wakiwa wengi kutakuwa na 'economic diversification' na hii itakuwa na positive multiple effects kwenye uchumi wetu.
3. Makampuni yatakayowekeza nchini yatauza bidhaa kwenye nchi nyingine pia, kwa hiyo watu watakuja hapa nchini kununua bidhaa wapeleke kwao. Kwa mfano makampuni ya china ya simu, magari na.k yakiwekeza tanzania yatauza africa nzima, hivyo badala ya wafanyabiashara wa kiafrika kwenda guanzhou, watajaa Tanzania na watalala kwenye mahoteli yetu na kununua matikiti yetu ya mkuranga. Tunapata pesa na kodi.
4. Watanzania kujifunza kutoka kwa wawekezaji. Haya makampuni yakija kwa wingi, tutapata fursa ya kujifunza teknologia n.k. wadogo zetu hawatahangaika sana kuzunguka kutafuta field atachement na lile tatizo la kuwa na na engineers wasioweza kutengeneza chochote kotokana na kusoma theories tu litapungua.
Kuhusu ajira.
1. Makampuni haya hayataajiri wageni tu bali pia wenyeji hasa kwenye nafasi za kazi za jumla kama uhasibu, manunuzi, utawala. Na.k top management pekee ndio watakuwa wenye kampuni au waliochaguliwa na wenye kampuni.
Hili ni muhimu kwa sababu zifuatazo
1. Hakuna mwekezaji yoyote makini anayeweza kukubali kumkabidhi kampuni mtu asiyemjua awe ndio mfanya maamuzi kwa mtaji wa mabilioni. Hata kama ni wewe huwezi kufanya hiyo labda kama una bet mtaji.
2. Waafrica wengi tuna kosa baadhi ya skills za msingi kwenye maeneo flani. Kwa mfano kwenye electronics, ukweli bado tuko nyuma sana na tuliwahi kuyauliza makampuni kadhaa ya electronics kwamba kwa nini wasiwekeze afrika kwa kuwa kuna soko kubwa? Jibu lilikuwa kwamba africa hakuna raslimaliwatu yenye skills nzuri kwenye electeonics na hawaruhusu wachina kuwekeza na kufanya wenyewe kwenye maeneo hayo.
3. Changamoto ya uaminifu. Moja ya shida kubwa inayotukabili wa Tanzania ni suala la uaminifu. Ni rahisi sana kupata mtu mwenye elimu, lakini kupata watu wa aminifu si jambo la kitoto. Kama huamini wekeza pesa mahali halafu weka mbongo azisimamie halafu ulete mrejesho. Kwa hiyo ni vigumu kumlazimisha mwekezaji kuweka meneja asiyemjua vizuri. Hata hivyo kwenye eneo hili bado tunayo fursa ya kujifanyia self improvement na kufanya vizuri.
Kwa ujumla kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji nchini kama alivyosema mh. Rais Samia kuna faida kwa pande zote na tunahitaji wawekezaji kuliko wanavyotuhitaji.
N.b: Mada hii inazungumzia wawekezaji toka nje.
Nami naona nichangie kuhusu hizo hoja zako:
Suala la makampuni toka nje kuja kuwekeza ndani ya nchi halitokani na kuangalia jambo moja bali mambo kadhaa.
Mosi umedai kuwa kampuni zikiwekewa mazingira ya kutolipa kodi bado kuna faida nchi itapata, Uamuzi huo unaweza kuua kampuni zingine ambazo ni za wazalendo au za nje lakini ziliingia awali na tayari zinafanya kazi katika sub sector hiyo hiyo ambayo kampuni mpya toka nje inasamehewa kodi. Kumbuka kama kampuni mbili zote zinauza katika soko hilo hilo lakini mmoja halipi kodi na mwingine analipa kodi maana yake mmoja atauza ghali na mwingine atauza kwa bei rahisi hivyo kuondoa ushindani halali na kupelekea kampuni inayolipa kodi kufa au kushindwa kupanua shughuli zake. Hii itasababisha serikali ikose kodi toka makampuni yaliyokuwepo awali ( VAT, income tax, corporate tax nk.), ajira katika makampuni hayo kupotea. Mfano hai ni Dangote yeye alipewa tax concessions nyingi ambazo viwanda vingine vya cement kama twiga, Tanga na Mbeya havikupewa hivyo kuviathiri sana viwanda hivyo. Concession yeyote inatakiwa itolewe kwa sub sector nzima sio kumpoendelea mwekezaji mmoja.
Pili, Economic diversification unayodai itakuwepo inaweza isiwepo kama ilivyokuwepo awali katika sub sector hiyo hiyo kutegemeana ujio wa kampuni mpya umepunguza kiasi gani kampuni zilizokuwepo awali. Mfano katika biashara ya daladala kama wakiondolewa wote akapewa mwekezaji mmoja tu kama jinsi BRT ilivyokuwa inaelekea maana yake wenye daladala wapatao elfu tatu wanaondolewa na kipato kinachogusa familia zao wanaofikia elfu kumi na nane (chukulia familia ina watu 6) kitapotea, ada za watoto elfu 12 zitakosekana (familia moja watoto 4), school uniforms za watoto zitapotea nk.
Tatu, umedai makampuni yatauza nje Africa nzima hivyo tutapata pesa nchi kupitia multiplier effect; sio kweli kabisa. Elewa katika suala zima la uwekezaji yaani foreign direct investments (FDI) kuna uwekezaji wa aina mbili hivi: Kuna wale wanaotarget soko la ndani ya nchi ambao ndio wengi zaidi; wuwekezaji wa aina hiyo ndio huo athari zake nimezitaja hapo juu. Aina ya pili ya uekezaji ni Platform seeking FDIs ambao ndio hao unaodai wewe kuwa watawekeza na kuuza Africa nzima. Aina hii ya pili ni ngumu kuipata katika mazingira yetu kwa sababu wawekezaji hao wanaangalia mambo mengi na sio sula la kodi tu. Mfano anajua kuwa kutokana na kuwa na jumuiya za kiuchumi kama EAC na SADC kama akiwekeza katika nchi yeyote kati ya hizo atakuwa na access ya kuuza bidhaa zake katika nchi zote wanachama wa umoja huo mithili ya mtu anayezalisha bidhaa Dodoma anavyoweza kuuza Tanzania nzzima. Hivyo kabla ya kuchagua awekeze nchi gani kwa ajili ya soko hilo tajwa ataangalia vigezo vingi kama miundombinu iliyopo (barabara za uhakika,, reli, bandari, umeme, mawasiliano ya simu, intenet); utulivu wa kisiasa, kama kuna wafanyakazi wenye ujuzi (skilled labour) predictability of taxes regimes, gharama za kuzalisha/kufanya biashara, mfano kama unit moja ya umeme kwako ni ghali kuliko Kenya au Africa Kusini ina maana akizalishia hicho kitu hapa anaweza kushindwa kukiuza nje maana kuna kampuni nyingine inaweza kuwekeza kule Kenya kwenye gharama nafuu za kufanya biashara hivyp kumfanya ashiundwe kushindana katika soko la EAC au SADC. Hivyo ndugu yangu kama ni mfuatiliaji mzuri wa haya mambo ya kiuchumi utaona wazi ni rahisi kwa mwekezaji anayetarget soko la SADC kuwekeza Africa kusini au yule anayetarget soko la EAC kuwekeza Kenya kuliko Tanzania. Nchi ikiwa siyo compitetive kwa vigezo nilivyovitaja basi mwekezaji inayoweza kumpata ni katika extraction sector kama vile madini, gesi na mafuta. Na hapo msipokuwa makini ndipo mnalizwa kama tulivyoshuhudia mikataba mibovu ya madini iliyoingiwa na serikali ya awamu ya nne.
Nne, Kwa kuwa sio rahisi kupata platform seeking FDIs, tunaoweza kuwapata ni wachimbaji madini, mafuta na gesi basi tunaweza tusifaidike na rasilimali zetu tusipokuwa makini. Lakini pia tutapata wawekezaji wa soko la ndani ambao watazalisha bidhaa zao na kuuza kwa shilingi lakini mwisho wa siku baada ya kupata faida watataka kuhamisha faida yao nje ya nchi. Hapo ndipo mtanange unapokuja kuwa itabidi pesa ya kigeni tuliyopata kwa kuuza korosho, pamba, kahawa ndio tuwaruhusu wachenji faida yao na kuondosha nchini. Hii inasababisha kuwepo na high demand ya pesa za kigeni kwa sababu kumbuka tunazihitaji pesa za kigeni kwa ajili ya kununulia madawa, mafuta na vitu vingine muhimu. Hivyo inaweza kupelekea shilingi kushuka thamani. Soko la ndani ni vizuri wawekezaji wa ndani wakadominate kwani wao fedha ya kigeni wanayohitaji ni ya kununulia mashine na labda malighafi na sio profit repatriations
Hata hivyo nakupongeza umechambua critically, debate za namna hii ni nzuri.