Maono ya Rais mama Samia kuhusu uwekezaji nchini kwenye nyuzi 360

Tatizo kubwa la wabongo ni upeo mdogo wa kufikiri, hivi watu wanafikiri kuwa faida inayipatikanwa kwa wawekezaji ni kodi tu? au Ajira tu? nje ya hapo wanahisi hakuna faida ya uwepo wao. Hizi ni akili za karne zilizopita bado wabongo zimo vichwani mwao.
 
Ajira zipi sasa unazungumzia mkuu, maana bila sekta binafsi kukua hakuna ajira na hakuna ukuaji wa sekta binafsi bila uwekezaji.
Haya ndio madhara ya kupost mambo usiyokuwa na uwezo nayo kuyajadili,

Mara hii tu umeshasahau hata umetuandikia nini.
 
Hii analysis yako mbona inaangalia pande Moja tu?

Afu ujue unaongelea pindi wanafunzi wanamaliza chuo wachache Sana na Sasa Idadi iko zaidi ya hapo.
Then huangalii na priorities za wakati ule na wakati wa Hayati.

Lakini pia usisahau ni 2012 kipindi cha JK watu walijazana Taifa kwenye interview.

Tuendelee kuchapa kazi
 
Watu wanachukulia jumla jumla kuwa uwekezaji unaongeza ajira, lakini ukweli ni kuwa uwekezaji unaweza kusababisha ajira zipotee tena kwa maelfu. Ajira inaweza kuwa ya mshahara au ya kujiajiri mwenyewe. Sasa kama umejiajiri kihalali halafu kutokana na sera za serikali unalazimishwa kuachana na shughuli uliyokuwa umejiajiri, hapo uwekezaji huo na balaa. Huko vijijini mamilioni ya wakulima wamenyang’anywa ardhi zao ili tu kupisha hao wanaoitwa wawekezaji huku wakulima hao wakikejeliwa kuwa hawazalishi kwa tija na kuwa wawekezaji hao watawaajili. Binafsi nimebahatika kuzunguka sana maeneo ya vijijini kutokana na kazi niliyokuwa naifanya. Niliwahi kufika wilaya moja nikamkuta mtu ambaye alikuwa na ekari kumi na mbili, yeye alikopa power tiller Mfuko wa pembejeo (AGTIF) kwa lengo la kulima mpunga katika shamba lake hilo, wakati huo huo aliletwa mwekezaji tena toka nje ya nchi akapewa ardhi katika kata hiyo ilia alime mpunga, kilichofanyika ni kuwa mamlaka zilichukua ardhi ya wakulima wadogo wadogo katika vijiji vinavyomzunguka mwekezaji huo na kuunganisha ili kumpatia eneo la kutosha mwekezaji huo, hivyo kupelekea wananchi hao kukosa ardhi ya kulima akiwemo huyo aliyepoteza hekta 12. Sasa fikiria huo mkopo aliochukua AGTIF aliulipaje wakati tayari shamba alilotaka kuzalishia ambalo ni mali yake amenyang’anywa? Yaani uwanyang’anye ardhi wazawa na kuwafanya manamba katika ardhi yao hiyo hiyo! Ukienda njia ya Rufiji, utaona kuna mapori mengi sana kuzunhguka vijiji na unaweza kuzani kuwa kuna ardhi kubwa sana ya kulima, lakini ukweli ni kuwa ardhi yote hiyo wamepewa hao wanaoitwa wawekezaji na ardhi hiyo hata kuilima hawailimi lakini wakati huo huo wanavijiji waliokuwa wanaimiliki ardhi hiyo wanasumbuka kwa kukosa ardhi ya kulima. Huko nyuma kabla RUBADA haijavunjwa na JPM ilikuwa ndio Karl Peters wa Tanzania katika kunyang’anya ardhi na kuidalalia. Malaki ya hekta zimeondolewa mikononi mwa wakulima na kupewa wajanja kwa mgongo wa uwekezaji, Tena huko nyuma kuna watu walikuwa wanakuja bila hata senti tano lakini baada ya kupewa ardhi wanachukua hati wanaenda benki tena za ndani ya nchi na kukopa mamilioni ya pesa na kufanyia biashara zingine kama uagizaji wa mafuta.



Unalalamika kuwa wamachinga wamezidi, umachinga ,mwingine ni matokeo ya watu kupoteza ardhi zao sasa inabidi wafanye uchuuzi, bodaboda, umalaya, mama ntilie (sio kama nadharau kazi hizo la hasha) kwa sababu hizo sekta hazijai zinampokea yeyote anayekuja kujiunga nazo ingawa soko linakuwa halipanuki.

Pia watu wanasema wakati wa JK kulikuwa na pesa mtaani lakini hawajiulizi kuwa zilikuwa pesa halali? Wizi, ufisadi na ubadhirifu wa pesa za umma na uuzaji wa madawa ya kulevya ulichangia katika ukuaji uchumi, hivyo uchumi wa wakati huo haukuwa halisi. Wewe inaweza kuwa hukuwa unaiba lakini manufaa ya wizi yalikufikia kupitia mnyororo wa wizi. Mathalani afisa au mfanyabiashara akishahomola atakuja mtaani kwako na kukupa kazi ya kumjengea au utamuuzia nguo bei juu au atawahonga nyumba zake ndogo mamilioni hivyo watu wengine kunufaika kama vile saluni za urembo nk. Lakini vile vile kulikuwa na watu kibao wanaumia kwa kukosa dawa, pensheni, na huduma zingine sababu sehemu kubwa ya pesa imeibwa. Kwa sasa hata mambo yakilegezwa vipi pesa haziwezi kurudi kama wakati wa JK unless wizi/ufisadi urudi upya kwa kasi. Kuna afisa mmoja wa kawaida kabisa asiye na cheo ilikuwa kila mwisho wa wiki lazima aende kwa ndege kwao Mwanza na kurudi jumapili au jumatatu asubuhi ila wakati wa JPM alikuwa haendi licha ya kuwa kazi yake haikubadilika.

Kiwango cha ukopaji hakiwezi kulingana kwa kila Rais aliyetawala, lakini ni wazi marais wote watano walikopa ila JPM alipoingia alikuta deni kubwa tayari, ukopaji wake haukusababisha deni liwe kubwa, na hayo madeni ya nyuma yanaongezeka riba, hivyo unaweza kuona deni limeongezeka wakati wa JPM lakini sehemu kubwa ya ongezeko hilo ni riba za nyuma kuliko deni jipya. Ukitaka kukosoa hili chukua data kila Rais aliyeingia madarakani alikuta deni shilingi ngapi na alipoondoka aliacha shilingi ngapi.

Watu wamevamia mjadala na wakati hawaelewi undani wa mambo na vilevile chuki binafsi dhidi ya JPM.
 
Kwenye Ile Interview ya Takukuru
 
Mkuu tumerudi tena kwenye nchi ya hoja kwa hoja. Kwa mkuu anayedhani ana hoja au ushuauri wa maana huu ndio wakati. Ambaye hatutumia wakati huu huenda asipate tena fursa ya kutoa hoja yake kwa ufasaha katika kipindi fulani na kubaki kulia lia.
Kinachonishangaza ni kuwa na nyie mlikuwa mnajua hatukuwa kwenye mwelekeo sahihi. Hilo tu ndilo linalonishangaza.
 
Mkuu rcm
RUBADA - Rufiji Basin Development Authority

Hii inahusikaje na kunyanganya Ardhi?
 
Suala la kwanza kujiuliza hapa ili mada yako iwe fikirishi zaidi na kuweza kupata majibu sahihi kwa muktadha sahihi wa hoja yako naomba kuchagiza yafuatayo;

Moja, can a foreign investor own land in Tanzania!?

Mbili, can a foreign investor obtain right of occupancy and or derivative right of occupancy in Tanzania!?

Kama majibu yote yatakuwa ndio basi cha kujiuliza ni kwamba utaratibu upoje chini ya Kituo cha Uwekezaji?
 
Hivi huko si ndiyo tulikotoka na bado kodi ilikuwa 800m?
Umemjibu vizuri sana,huko ndipo tulipotoka,nakumbuka Muhongo alipigia debe vitalu wapewe wageni,ilikuwa kelele nchi nzima kwamba vitalu wapewe wazawa,leo tunataka kurudi kule tena

Nafikiri tunahitaji wawekezaji wa kuja kutoa elimu iliyo bora maana naona shida yetu ni Elimu basi🤣🤣🤣
 
Nakumbuka kuhusu SGR Nape na yule mbunge wa Nzega mjini walisema inabidi tuwape wawekezaji,Magufuli akasema waleteni hata sasa hivi waje wajenge🤣🤣🤣,hakuna wawekezaji wa maana
 
Wewe inaelekea unataka watu waporwe hela zao kwa kisingizio cha ukusanyaji kodi
 
Mkuu rcm
RUBADA - Rufiji Basin Development Authority

Hii inahusikaje na kunyanganya Ardhi?
Kwa mujibu wa sheria iliyounda RUBADA, ardhi yote katika bonde la Kilombero iliwekwa chini ya RUBADA bila kujali kuwa kuna mamilioni ya watu kuanzia Kilombero hadi Rufiji walikuwa wanaishi na kumiliki maeneo hayo. Hivyo ilikuwa akitokea mwekezaji anahitaji sehemu yoyote ya ardhi RUBADA wanaitwaa ardhi hiyo toka kwa wananchi na kumuuzia/kumpa mwekezaji huyo bila kujali kuwa wananchi pia wanaihitaji ardh ihiyo wananchi watake wasitake.
 
Kwa akili yangu ndogo sina pingamizi wawekezaji wa nje kukaribishwa na kuwa na haki ya kuchagua waajiriwa wao wa kigeni kwenye key positions maana ndo wenye mali. Vibali via kz vitolewe kwa kuzingatia sheria ya Employment of non-citizens. Lakini kwa kutathmini nadhani tungeanza na meza ya majadiliano na EAC na SADC ili watanzania wawe na fursa anazotoa hapa nyumbani kwa wawekezaji wageni. South Africa 🇿🇦 tu tunaelewa jinsi zenophobia imewatesa ndugu zetu. Lazima tuelewe rules of the game giving and taking au watu wetu ndo wataumia.
 
Namba 3 hilo sio tatizo Tanzania tu bali ni africa nzima especially kusini mwa jangwa la sahara.

Ni kweli tunapaswa kujirekebisha au zitungwe sheria kali kwa ajili ya hii changamoto.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Ukweli mtupu, suala hili watu wanalichukulia poa tu.
 

Hapo kwenye kwenye ajira kama watakwenda kwa utaratibu wa Mama alivyosema wa muwekezaji kuja au kuleta watu awatakao kwa sababu yeye ndio mwenye hela basi usitegemee kuna mtanzania atapewa ajira kwenye hizo nafasi!
Huo utaratibu wa mwekezaji kuja kufanya atakavyo haupo nchi yeyote duniani!
 
Mkuu
Sio Kwamba Ardhi iliwekwa RUBADA kwa ajili ya kulinda mazingira ya maji na sio kwa ajili ya kupewa wawekezaji

Maana hizi Authority za mamlaka za Maji hazitofautiani katika mambo ya ardhi ,
 
Dada Theodora
How can u relate zenophobia na vibali vya kazi? Sio Kwamba Soko la ajira linaongozwa na competitive ya labour force sio upendeleo??
 
Aliyesema aje afanye "atakavyo" nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…