Maono ya Rais mama Samia kuhusu uwekezaji nchini kwenye nyuzi 360

Dada Theodora
How can u relate zenophobia na vibali vya kazi? Sio Kwamba Soko la ajira linaongozwa na competitive ya labour force sio upendeleo??
Ni twin issues. Angalia utoaji wa vibali vya kz SA ni strict mno na ndo maana wageni wengi wanafanya kz kinyemela hasa pale ni informal sector. Zenophobia prescribes on their issuance of workpermits na wanasema kabisa wageni wanachukua kz zao. Lkn ukienda kusoma SA utapata kibali kusoma lkn parttime job ngumu sana.

SA wanautaratibu wa kutoa takwimu mara kwa mara za ajira za wazawa - blacks, colored, white, disabled, gay etc
 
Ila Nadhani suala la SA ni controversial katika Zenophobia na vibali vya kazi. Kuna vitu vya kujiuliza je watu wetu hapa mfumo wa elimu unawafanya waajirike?
 
Mkuu
Sio Kwamba Ardhi iliwekwa RUBADA kwa ajili ya kulinda mazingira ya maji na sio kwa ajili ya kupewa wawekezaji

Maana hizi Authority za mamlaka za Maji hazitofautiani katika mambo ya ardhi ,
Usichanganye mamlaka za mabonde ya maji anbazo ziko nane: kazi zake ni kulinda vyanzo vya maji, kutoa vibali vya matumizi ya maji mfano unataka kuchimba kisima, kufanya kilimo cha umwagiliaji. RUBADA iliundwa kwa ajili ya kuendeleza bonde la mto Rufiji kuanzia mto Ruaha kule kilombero mto rufiji hadi unaooingia baharini na kazi yske ilikuwa kutafuta hao wanaiitwa wawekezaji kwa ajili ya kulitumia bonde kulima mazao. Hivyo walipokuwa wakienda kwa wananchi walikuwa wanaenda kibabe na kwa vitisho kuwa sheria inasrma wao ndio wamiliki wa bonde hilo bila kujali watu wameishi maeneo hayo tangu karne kadhaa nyuma. Kwa kweli kuna wananchi wameumizwa sana kwa kunyang"anywa ardhi maeneo hayo. Ukitaka ushahidi ju ya hili soma ripoti za HAKIARDHI ( Ngo) baadhi zinapatikana mtandaoni.

Nakumbuka mkurugenzi wake mmoja hapa mwishoni mwishoni alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya kuchukua rushwa ili kuwapa ardhi hao wawekezaji hasa ya Rufiji.
 
Ila Nadhani suala la SA ni controversial katika Zenophobia na vibali vya kazi. Kuna vitu vya kujiuliza je watu wetu hapa mfumo wa elimu unawafanya waajirike?
Elimu yetu ina mapungufu tena siyo madogo lakini informal sector si wanajiajiri? Hizo fursa hasa ndo shida huko. Kwetu hata vibali vya kz wanapewa expatriate salonists lkn huko aisee, ni shida.
 
Mkuu nakubaliana na wew kwa asilimia kubwa sana,
Ishu kubwa ni kuwaruhusu hawa wawekezaji wa njee, ndo wana mitaji mikubwa na wana skill ya business

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya Halmashauri kujipangia maendeleo gani zilifanya?
Je anaenda kubadili sheria za kodi au maneno ya kisiasa tu sheria ni zile zile?
 
Nakumbuka haki ardhi walikumbwa Sana na hili since 2013....ukisoma majarida yao utapata maarifa
 
Elimu yetu ina mapungufu tena siyo madogo lakini informal sector si wanajiajiri? Hizo fursa hasa ndo shida huko. Kwetu hata vibali vya kz wanapewa expatriate salonists lkn huko aisee, ni shida.
Lakini Hoja yako nikuwa lazima tulinde ajira za ndani lakini lazima policy ziendane na soko linasemaje au Sio Dada Theodora
 
Lakini Hoja yako nikuwa lazima tulinde ajira za ndani lakini lazima policy ziendane na soko linasemaje au Sio Dada Theodora
On Point. Na tuko tayari kudialogue na nchi nyingine majirani kwenye labour's market policies for symbiotic relations.
 
On Point. Na tuko tayari kudialogue na nchi nyingine majirani kwenye labour's market policies for symbiotic relations.
Lakini Diplomasia ya uchumi ni muhimu sana angalia mipaka ya Tanzania na kenya kaskazini juu ya mahindi.
 
Baada ya Halmashauri kujipangia maendeleo gani zilifanya?
Je anaenda kubadili sheria za kodi au maneno ya kisiasa tu sheria ni zile zile?
Rudi kijijini kwako kaangalie yaliyofanyika kabla ya 2015
 
Wakati wa mkapa, mwinyi na Nyerere ilikuwa inakusanywa kiasi gani kwa kila mmoja wao kwa mwezi
 
Leo, Mh. Rais amekutana na Wawekezaji kutoka China ambao wameahidi kufanya uwekezaji mkubwa Tanzania kwa kufungua Industrial parks na kuwekeza kwenye kutengeneza Magari, Simu na Madawa Miongozi mwa mambo mengine.

Siku chache zilizopita tulishauri wawekezaji hasa kutoka China washawishiwe kuwekeza nchi hasa kwenye maeneo hayo hapo juu halafu wafanyabiasha kutoka nchi nyingine za kiafrika waje kununilia Tanzania badala ya kwenda China ambapo tutapata faida za aina nyingi.

Tunampongeza Mhe. Rais kwa hatua hii ambayo itasaidia kuzalisha ajira kwa vijana na tunamuombea kila la heri.
 
Wakati wa Jakaya wawekezaji walikuwa kibao ,tulipata nini?,acheni masihara na hii nchi,sana tutarudi kuwa shamba la bibi tu.

Bila kukazia suala la mikataba kwa umakini dhidi ya wawekezaji kwa taifa na kukusanya kodi bila mzaha kama alivyofanya hayati Magufuli ni bure tu.
Mfano kampuni ya Barrick Gold Mine na kina Acasia walikuwepo ,hatukupata kodi stahiki na walikuwa wakipora tu,usishangae kampuni zikajaa kodi usizione
 
Miradi gani ya maana halimashauri hizo zilifanya ?,ebho !,
Magufuli ndani ya muda mfupi tu tumeona matokeo ,
Kipindi cha Jakaya halishauri gani zilifanya miradi ya maana ?,acheni ujinga
 
Mkuu, ungesoma kwanza hoja zilizotolewa kwenye bandiko la msingi ndio uchangie. Majibu ya maswali yako yote yalishajibiwa kwenye post Na. 1.

Pia ni ajabu kama wewe huoni umuhimu wa kukuza uwekezaji na kukua kwa uchumi. Nadhani ni suala la uelewa tu.
 
Miradi gani ya maana halimashauri hizo zilifanya ?,ebho !,
Magufuli ndani ya muda mfupi tu tumeona matokeo ,
Kipindi cha Jakaya halishauri gani zilifanya miradi ya maana ?,acheni ujinga
Kwa namna unavyoandika kama bata anakunya, inaonekana kabisa wewe siyo mtu MAKINI. Kuendelea na mjadala huu na wewe tutakuwa tunakuumiza bure.

Tafuta majukwa ya darasa la 7, Ila hapa siyo pako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…