Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Sote tunaelewa kuwa mkutano wa Berlin wa mwaka 1984 ndio ulioigawa Afrika kuwa katika mipaka tuliyo nayo leo. Mkutano huo uliitishwa na Otto von Bismarck ili kuigawa Afrika miongoni mwa mataifa ya Ulaya ambayo tayari yalikuwa yana infleunce Afrika kwa nia ya kuondoa conflicts. Ujerumani ilikuwa na influence katika sehemu tatu: Cameroon, Namibia na hapa kwetu Deutsch-Ostafrika.
Nia kuu ya Bismark ilikuwa ni kuigawa sehemu ya Afrika kusini mwa jangwa la Sahara katika vipande vinavyoanzia bahari ya Atlantic na kuishia bahari ya Hindi. Plani yake ilikuwa ni kuwa kuanzia Cameroon hadi Zanzibar ingekuwa nchi moja chini ya Ujerumani, halafu kuanzia Congo Brazaville hadi Msumbiji ya kasikazini ingekuwa nchi moja chini ya Ubelgiji, na kuanzia Angola hadi Mozambique ingekuwa nchi moja chini ya Ureno, halafu sehemu nyingine yote ya kusini mwa Afrika ingebaki chini ya Uingereza. Kwa plani hiyo Ramani ya Africa leo hii ingekuwa hivi:
Plani hiyo haikukubaliwa na mataifa mengine ya Ulaya hasa Mfalme Leopord wa Ubeligiji hakutaka kupoteza sehemu ya Kongo ambayo alikuwa amejimilikisha yeye binafsi, na halafu kukawa na ubishi mwingine kuhusu mgawanyo ambao ungeiweka Kenya, Uganda, sehemu ya kaskazini mwa Kongo, Central African Republic, Chad na na Nigeria chini ya mamlaka moja. Ukawa mvutano mkali kati ya Uingereza na Ufaransa. Mwingereza hakutaka kupoteza Uganda kwa vile ndicho chanzo cha mto Nile, na Mfaransa naye hakutaka kupoteza kipande chochote cha Afrika kwani kama plani hiyo ingeendelea, mfaransa angebaki mikono mitupu.
Halafu snag nyingine ikawa ni kuwa Waingereza nao hawakutaka kupoteza sehemu ya Zambia na Zimbabwe kwa vile ilikuwa inamilikiwa na kampuni ya Rhodes ambayo ilikuwa imeanzisha migodi kule. Kwa hiyo plani nzima ya Bismarck ikafeli, ndipo wakaamua kukata vipande vipande tuvionavyo leo. Hata hivyo Bismarck hakutaka kusindwa kirahisi, badala yake akaishawishi Uingereza ikubali kuchukua visiwa vya Zanzibar ili wabadilishane na visiwa vya Heligoland, na vile vile wabadilishe mpaka wa Namibia ili ufikie mto Zambezi, akijua kuwa kwa kutumia mto Zambezi angeweza kufikia bahari ya Hindi kirahisi bila kuzunguka Cape of Good Hope. Kwa hiyo Mpaka wa Nambia ukabidilishwa na kuwa na kale kasehemu kembamba kanakofikia mto Zambezi kama ionekanvyo kwenye ramani hapa.
Wakati huo Uingereza ilikuwa inajua kuwa mto Zambezi hauwezi kutumika kwa usafiri wa meli kwa vile kulikuwa na Victoria falls mpakani mwa Zambia na Zimbabwe, ila wakawakubalia wajerumani haraka haraka kusudi wabaki na umiliki Kenya, Uganda, Zambia na Zimbabwe ambazo walikuwa na hatari ya kupoteza kwenye mkutano huo.
Sijui kama plani ya Bismarck ingefanikiwa huenda siku moja tungetawaliwa na Paul Biya, au Mobutu au Ngueso. Vile vile watu maarufu kama Roger Milla, Diblo Dibala, Abeti Maskini na Ndungidi wangekuwa watu wetu.